Hiki ndicho kibanda kilichoandaliwa kwa ajili ya kufanyia tambiko ya mila kwa mwili wa John kabla ya kuagwa na kuzikwa.
MJI wa Kigamboni umegubikwa na majonzi
mazito na vilio kutawala kila kona kufuatia kijana aliyefahamika kwa
jina la John Thobias Joseph (19), dereva wa bodaboda maeneo ya Magogoni
Kigamboni, kuchinjwa kisha pikipiki yake kuchukuliwa na watu
wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Inasemekana John, alipigiwa simu na mtu
asiyemfahamu akimtaka akamchuke na kumpeleka Kisarawe II, baada ya
maongezi, John alionekana kumfahamu mteja huyo na kumuahidi kumfuata.
Inasemekana John alikuwa amembeba mama yake mdogo wakitokea hospitali, ambapo alimshusha mama na kumfuata mteja huyo.
Akisimulia bodaboda mwenziye alisema
“John huwa na taratibu za kufika kijiweni asubuhi (mtaa wa Tungi kwa
Matenga ambapo anapaki) lakini siku ya tukio haikuwa hivyo, jambo
lililowashangaza wenzake na mmoja wao akaamua kumpigia simu lakini
iliita pasipo kupokelewa.
“Baada ya kumtafuta kwa muda bila
mafanikio ndipo tukapata taarifa za kuwapo kijana mmoja aliyekutwa
amekufa nje ya mji, ndipo tukaamua kwenda eneo la tukio na kumkuta ni
John’’ alisema kijana huyo.
Aidha Katekista Millinga, akizungumza katika misa ya kuaga mwili wa marehemu huyo alisema, “Pengine wauaji wako hapahapa tulipo, sidhani kama wauaji wanatoka mbali, lakini maandiko yanasema, anayeuwa kwa upanga naye atauwawa kwa upanga."
Aidha Katekista Millinga, akizungumza katika misa ya kuaga mwili wa marehemu huyo alisema, “Pengine wauaji wako hapahapa tulipo, sidhani kama wauaji wanatoka mbali, lakini maandiko yanasema, anayeuwa kwa upanga naye atauwawa kwa upanga."
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa
Temeke, Engelbert Kiondo amekiri kutokea kwa tukio hilo na kutaka
familia na wanabodaboda wote kuwa wavumilivu wakati uchunguzi
ukiendelea.
Aidha, amewataka vijana wa bodaboda kuwa makini na abiria wanaowakodi,wasivutike na pesa nyingi wanazoahidiwa.
Aidha, amewataka vijana wa bodaboda kuwa makini na abiria wanaowakodi,wasivutike na pesa nyingi wanazoahidiwa.
John, ambaye alikuwa ni kijana mdogo
sana kiumri na hata umbo, alikutwa na mauti siku ya Alhamisi tarehe
8/05/2014 majira ya saa 8 mchana eneo la Kisarawe II, nje kidogo na
Kigamboni.
Marehemu alizikwa tarehe 10/05/2014 katika makaburi ya Magogoni-Kigamboni, Dar.
0 comments:
Post a Comment