Mzee Majuto, Ray, JB na Irene Uwoya wakiwa nchini Uturuki
Akizungumza na Mtandao wetu, Mzee Majuto amesema kuwa baada ya kuushangaa mji wa Instabul na jinsi wanavyozitumia tamaduni zao kwenye maisha ameona aandae filamu itakayoonyesha maisha hayo.
“Nimefanya kazi, sio tu na wasanii wa Uturuki pia kuna Watanzania ambao wanaishi kule, nimejifunza vitu vingi sana, wenzetu wanathamini vya kwao,” amesema. “Nimeshangaa kuona treni za chini,Uturuki umeme haukatiki hata siku moja, yaani kule hakuna kitu kinashindikana kwao. Kwahiyo kutokana na hali hiyo ikanijia wazo nifanye kitu, Strange of Turkish. Filamu na vipande vya Uturuki nimeshashoot, bado huku Tanzania, ni filamu yangu mwenyewe.”
0 comments:
Post a Comment