Mambo
bado mabaya! Ule ugomvi wa mashosti wawili nyota katika tasnia ya
sinema Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja ‘K’, sasa
umechanja mbuga hadi kufika mjengoni, ambako inadaiwa kuwa baadhi ya
wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wameingilia kati ili
kuumaliza, Risasi Jumatano linakuhabarisha.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, baada ya mvutano wao wa muda mrefu, wabunge
hao walimwita Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’ na kumuuliza kama ni kweli wawili hao hawaelewani.
Inadaiwa kuwa Steve alikiri kutokuwepo kwa maelewano kati ya wawili hao ambao awali walikuwa ni marafiki pete na kidole.
Ilisemekana
kwamba baada ya kuhakikishiwa kuwepo kwa ishu hiyo, baadhi ya wabunge
hao, hasa wapenda michezo na sanaa, walimuagiza Steve kulifanyia kazi
tatizo hilo haraka, akishindwa basi awapelekee ili wawakalishe chini.
“Walimwambia
Steve kwamba ni kitendo cha aibu kwa mastaa wakubwa kama hao kugombana,
hiyo inawapunguzia heshima kwani hiki kilikuwa ni kipindi cha
kushikamana kwa umoja ili kuisogeza mbele tasnia yao badala ya
kulumbana,” kilisema chanzo hicho kikikataa kutaja majina ya wabunge hao
na kutaka aulizwe Steve.
Gazeti
hili liliwasiliana na Steve juu ya ukweli wa madai hayo, ambaye
alikubali kuwa ni kweli baadhi ya wabunge wamemtaka kumaliza bifu kati
ya waigizaji hao maarufu Bongo kwani nyuma yao kuna vijana wengi
wanatamani kuwa kama wao.
Risasi
Jumatano lilizungumza na mbunge wa Kinondoni Idd Azan ambaye alisema
hata yeye atawaunga mkono wabunge watakaojitolea kuwasuluhisha
0 comments:
Post a Comment