Thursday, 29 May 2014

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AWASILI WILAYANI BABATI LEO, AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI MANYARA

...

Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukivuka katika mto Magara mapema leo asubuhi kuelekea wilayani Babati mkoani Manyara.Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,siasa na Uenezi Nape Nnauye,wakiwa kwenye ziara ya siku saba ya kukagua kuhimiza na kusukuma miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Chama,kukagua maandalizi ya uchaguzi ya serikali za mitaa,kusikiliza kero za wananchi na kuzitafututia ufumbuzi.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Magara wakivuka mto Magara wakielekea shuleni mapema leo asubuhi,Mto huo umekuwa na changamoto kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo,wakati wa Masika kwa kukosa daraja la kuvukia kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine,daraja hilo ndilo linalotenganisha Wilaya ya Mbulu na Babati mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Magara baada ya kumsimamisha katika mto Magara wakitaka kujengwa daraja katika mto huo litakalounganisha Wilaya ya Mbulu na Babati mkoani Manyara. Daraja hilo liliahidiwa kujengwa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa kampeni zake mwaka 2010. Kinana aliuagiza uongozi wa Mkoa wa Manyara kuangalia uwezekano wa kujenga daraja la muda kwa kutumia vyuma wakati ukisubiriwa ujenzi wa daraja la kudumu ili wananchi wa pande zote mbili hizo waweze kuwasiliana bila shida.
Wakazi wa kata ya Magara wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kwa vifijo na Nderemo mapema leo asubuhi alipokuwa akiwasili wilayani Babati mkoani Manyara.
Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini,Mh.Jitu Son akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana jimboni kwake mapema leo asubuhi,akitokea wilayani Mbulu mkoani Manyara.
Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Babati vijijini katika kata ya Magara mkoani Manyara mapema leo asubuhi
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini,Mh.Jitu Son,mara baada ya kuwasili katika kata ya Magara,wilayani Babati.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa Babati vijijini katika kata ya Magara mkoani Manyara mapema leo asubuhi,ambapo pia alipanda mti na kukagua mradi wa ujenzi wa wodi ya Kituo cha afya Magara,wilayani Babati.
Kinana akipanda mti nje ya jengo la wodi ya kituo cha Afya Magara wilayani Babati leo.
Nape Nnauye akishiriki kupanda Mti nje ya jengo la wodi ya kituo cha Afya Magara wilayani Babati leo,kulia ni .Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini,Mh.Jitu Son
Katibu wa CCM,Ndugu Kinana akipandisha bendera baada ya kuzindua shina la Wakereketwa katika kijiji cha Magugu,Wilayani Babati sambamba na kugawa kadi kwa Wanachama wapya.
Wakazi wa Kijiji cha Magugu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia mapema leo kwenye viwanja vya Magugu Mashine,Wilayani Babati mkoani Manyara mapema leo.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger