BIBI wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole
(65), leo ameangua kilio katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar ers Salaam wakati akipelekwa kizimbani kwa ajili ya kusomewa kesi
yake ya kunaswa na madawa ya kulevya yenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni 37.
Hakimu aliyepelekewa kesi hiyo, Frank
Mushi, aliiahirisha kesi hiyo mpaka kesho ili bibi huyo ambaye hajui
Kiswahili wala Kiingereza atafute mkalimani.
Cole alisema lugha anayoweza kuitumia
kiufasaha ni Kiyoruba ambacho hutumiwa nchini Nigeria. Katika hali
iliyoonesha kukata tamaa, bibi huyo alianza kuangua kilio akiomba Mungu
amsaidie.
0 comments:
Post a Comment