KHAA! Katika hali ya kushangaza, dada wa
kazi za nyumbani (hausigeli) mkazi wa Tabata jijini Dar aliyetambulika
kwa jina moja la Aneth, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudai
kuwa bosi wake ambaye ni Mzungu amemlazimisha kufanya mapenzi na mbwa
wake.
Mzungu huyo ambaye jina tunalihifadhi,
alidaiwa kufanya tukio hilo la kinyama Mei 26, mwaka huu na inadaiwa
Aneth alipomkatalia, alimtimua nyumbani hapo kwa kumtupia virago.
Chanzo makini kilidai kuwa, baada ya
kutupiwa virago bila kupewa mshahara wake sambamba na kipigo, Aneth
aliripoti tukio hilo katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Tabata, Dar na
muda mfupi polisi walifika nyumbani hapo lakini Mzungu huyo hakutoka
ndani, akakataa kuzungumza chochote.
Taarifa zilidai kuwa, baada ya polisi
kukutana na kizingiti hicho, walimpigia simu kiongozi wao ambaye
aliwaamuru warudi kituoni wajipange upya.
Akisimulia zaidi ishu hiyo, Aneth
alisema polisi walipoondoka eneo hilo, umati uliochukizwa na kitendo
hicho ulikusanyika nje ya nyumba ili kumdhibiti ‘mtasha’ huyo kwa
lolote.
“Kuna jirani mmoja alipiga simu tena
kituo cha polisi alipoona hali ya hewa imechafuka ndipo polisi wakafika
kwa mara nyingine na difenda na kufanikiwa kuingia ndani kwa kutumia
geti kubwa, walipofika walikuta milango imefungwa lakini ilisemekana
aliruka ukuta na kutimkia kusikojulikana.
“Polisi waliniambia nimpigie simu
ajisalimishe lakini nilipompigia alisema hayupo na kama tunamhitaji
tukutane sehemu huku na yeye akiwa na polisi wake,” kilisema chanzo.
Mmiliki wa nyumba hiyo anayeishi
Kigamboni, Mr. Cris alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo, alikiri kupokea
malalamiko na manyanyaso kutoka kwa Aneth.
Akisimulia zaidi maisha anayoishi na
Mzungu huyo, Aneth alisema: “Alikuwa akinitafutia sababu za kunitimua
kwani hivi karibuni kwa bahati mbaya nilipoteza ufunguo wa ndani,
akanipiga mateke na kunisababishia maumivu makali mwilini kiasi cha
kushindwa kutembea.
“Lakini lililoniuma zaidi ni hili la
kunilazimisha eti nifanye mapenzi na mbwa wake, amekuwa akifanya hivyo
mara kwa mara mimi nikaona siyo sawa na nilipokataa ndipo yakanikuta
hayo.”
Aneth aliripoti matukio hayo katika
Kituo Kidogo cha Polisi Tabata na kupewa fomu ya matibabu (PF-3)
sambamba na kufunguliwa jalada la kesi namba TBT/RB/3132/2014/ SHAMBULIO
na jalada la uchunguzi lenye namba TBT/IR/1829/2014/UCHUNGUZI.
-GPL
0 comments:
Post a Comment