Mwili wa Marehemu Munuo ukitolewa katika Gesti hiyo
Mtumishi
wa idara ya Afya katika halmashauri ya mji wa Kahama, Mkoani Shinyanga,
Jeremiah Munuo (50) amekutwa amefariki dunia katika nyumba moja ya
kulala wageni mjini Kahama.
Taarifa kutoka jeshi la polisi wilayani humo zimesema kwamba Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika nyumba hiyo iitwayo KK Lodge iliyopo jirani na ofisi za Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Taarifa zimesema watumishi wenzake walikwenda kumuona leo majira ya saa 6 mchana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa kwa muda mrefu.
Jesh la polisi wilayani Kahama limefika katika eneo la tukio na kumkuta marehemu Munuo ambaye alikuwa na miezi 3 tu tangu ahamishiwe katika halmashauri hiyo akiwa na Fedha taslimu shilingi 596,000 na simu nne za mkononi.
Mwili wa marehemu Munuo umepelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya wilaya hiyo na uchunguzi juu ya tukio hilo bado unaendelea.

Marehemu Munuo akiwa katika gesti hiyo alikokuwa amelala |
mwili wa Marehemu Munuo baada ya kugeuzwa na kukaguliwa |
Mwili wa Marehemu Munuoukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama |
0 comments:
Post a Comment