Sunday 4 February 2018

Tetesi za soka Jumapili 4.02.18


Riyad Mahrez

Arsenal inatarajiwa kujiunga katika kuwania kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Leicester Riyad Mahrez, mwenye umri wa miaka 26. (Daily Star Sunday)

Meneja wa Leicester Claude Puel anasaema "hamfikrii" Mahrez, ambaye hajaonekana katika kalbu hiyo tangu pendekezo la uhamisho wake kwenda Manchester City litibuke kufuatia kuwadia kwa muda wa mwisho wa uhamisho. (Mail on Sunday)

Muungano wa wachezaji soka kitaaluma umejitolea kusaidia kutatua hali baina ya mchezaji raia wa Algeria Mahrez na timu ya Leicester City. (Sun on Sunday)

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anafikiria kumlipia Maurizio Sarri Euro milioni 8 katika mkataba wake ili aweze kumsajili kocha huyo wa Napoli kuwa meneja mpya wa timu yake.(La Gazzetta dello Sport - in Italian)Conte aliteuliwa kuifunza Chelsea baada ya kuisimamia timu ya Italia katika michuano ya Euro mnamo 2016

Huenda bosi wa Chelsea Antonio Conte akafutwa kazi iwapo upande wake utashindwa na Watford Jumatatu. (Sunday Express)

Conte ameiambia Chelsea kuwa wanaihitaji kuwasajili wachezaji wawili au watatu wa kiwango cha kimataifa kuweze kulinyanyua taji la ligi msimu ujao, na ametaja kuwasili kwa wachezaji wengi kama mojawapo ya kushindwa kwao kulilinda taji lao msimu huu. (Sunday Telegraph)

Kipa wa Manchester City mwenye umri wa miaka 30, Joe Hart, aliyechukuliwa kwa mkopo huko West Ham, atalengwa na Chelsea iwapo Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 25 ataondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Sun on Sunday)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea Ross Barkley, huedna amepata jereha la msuli wa paja ambalo iwapo litathibitishwa , litamfanya mchezaji huyo raia wa England kuwa mchezaji wa nane katika klabu hiyo kukabiliwna tatizo hilo msimu huu. (Sunday Telegraph)

Manchester United wapo katika hatua kubwa ya mazungumzo ya kumchukua winga wa Ajax mwenye umri wa miaka 18 Justin Kluivert msimu huu wa joto - ambaye ni mwanawe mchezaji wa zamani wa Barcelona Patrick. (Sunday Mirror)Mesut Ozil na Rihanna

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Mesut Ozil ametangaza kuwa Rihanna ndio "bahati yake" baada ya muimbaji huyo kutazama ushindi wa Arsenal dhidi ya Everton. Rihanna pia alisherehekea na Ozil na wachezaji wenziwe ushindi wa Ujerumani katika kombe la dunia mnamo 2014 nchini Brazil. (London Evening Standard)

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, yupo tayari kuingia Real Madrid lakini mchezaji mwenzake wa timu ya kimataifa Dele Alli, mwenye umri wa miaka 21, hayuko tayari kwa mujibu wa mchezaji wa zamani wa Liverpool kiungo cha kati, Graeme Souness. (Sunday Times )

Real Madrid ipo tayari kuongeza mshahara wa Cristiano Ronaldo hadi Euro milioni 30 kwa mwaka kuanzia msimu huu wa joto, na kumfanya mchezaji huyo mwenye umri wamiaka 32 raia wa Ureno kuwa juu pamoja na mwenzake Neymar ki malipo ya mwaka. (ABC, via Marca)

Edin Dzeko aliipuza Chelsea ili asalie Roma kwasababu ya maisha yake 'yasio halisi' Italia, licha ya kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 raia wa Bosnia na Herzegovina anasema ni 'heshima kubwa' kwamba The Blues' inamtaka. (Klix, via Mail on Sunday)

Everton imempa ruhusa aliyekuwa kaimu mkuu wa zamani David Unsworth, ruhusa kuzungumza na Oxford United kuhusu pengo lao la kazi ya usimamizi. (Sky Sports)
Jose Mourinho

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameshutumu kwa mara nyingine hisia iliopo Old Trafford, and claims the noise made at Portsmouth's Fratton Park is better. (London Evening Standard)

Mourinho amelenga kumsajili mchezajiwa kiungo cha kati wa Bayern Munich raia wa Chile Arturo Vidal, mwenye umri wa miaka 30, katika msimu ujao wa joto huku kukiwepo wasiwasi kuhusu ukosefu wa nafasi zaidi katika kiungo hicho. (Manchester Evening News)

Mkuu wa West Brom Alan Pardew anawataka maafisa wa Baggies wamshawishi Jonny Evans akubali makubaliano mapya ya kumhifadhi mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 30 kutoka Ireland ya kaskazini dhidi ya timu nyingine za Ligi ya England. (Birmingham Mail)Bakary Sako

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Crystal Palace raia wa Mali Bakary Sako, mwenye umri wamiaka 29, ameondolewa kwa siku zilizosalia msimu huu kutokanana kuumiza mishipa na jicho la mguu. Ametuma ujumbe wa matumaini katika mtandao wa kijamii.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anasisitiza kuwa mshambuliaji Sadio Mane hana wivu na mshambuliaji mwenza Mohamed Salah na kwamba wachezaji hao raia wa Senegal na Misri ni 'marafiki wa dhati'. (Sunday Mirror)

Klopp anasema hana shinikizo kutoka kwa wamiliki wa Liverpool kwasbabau hawasemi, "mwaka ujao muwe mabingwa la sivyo unaweza kuondoka" na badala yake " ni watu wanje wanaosema , asipoleta taji, yupo kwenye shinikizo'." (Mail on Sunday)

Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Didi Hamann anaamini klabu hiyo badu ina mapungufu katika upande wa ulinzi , licha ya kumsajili bekiwa kati raia wa Uholanzi Virgil van Dijk, kwa thamani ya pauni milioni 75 mapema mwezi Januari. (Omnisport, via Liverpool Echo)
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger