Sunday 30 April 2023

AUAWA KWA KUCHINJWA BAADA YA KUPEWA TALAKA NA MUMEWE TINDE



Picha haihusiani na habari hapa chini

Na Mwandishi wetu - Tinde

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Mwanandakuna anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 58-60 mkazi wa kitongoji cha Ngaka kijiji cha Nyambui kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye kali shingoni na tumboni na watu wasiofahamika akiwa nyumbani kwake.


Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa mapema jana jioni  Aprili 29, 2023 kuna vijana walifika eneo jirani na alipopanga mama huyo wakawa wanavuta sigara lakini wakazi wa eneo hilo hawakuchukulia maanani kwa sababu mtaa ule una mwingiliano wa watu wengi.


“Kuna watu wawili walikuwa jirani chumba cha mama huyu, wakakaa kwa muda mrefu wakivuta sigara  na kuchat na simu huyo mama alikuwa anapika chakula cha usiku, wakati mama anatoka kumwaga maji ya kuoshea nyanya/uchafu majira ya saa mbili kasoro usiku ndipo watu hao wakamkaba na kumchoma kwa visu shingoni na tumboni”,wameeleza wananchi kutoka Tinde.


“Huyo mama alikuwa anaishi katika kitongoji hiki hiki na baada ya mgogoro wa ndoa aliondoka kwa mmewe akapanga chumba chake katika kitongoji hiki. Ametoka kwa mme wake miezi kadhaa iliyopita.Tukio hili limetokea wakati kesi ya kugawana mali baina yake na mme wake ipo mahakamani kwani baada ya kuachana na mmewe ambaye yupo Arusha ilifikia hatua ya kugawana mali wiki hii”, taarifa kutoka Tinde zinaeleza.


Inaelezwa kuwa Kesi ya ndoa baina ya mwanamke huyo na mmewe ilikuwa imefikia tamati Alhamis wiki hii Aprili 27,2023 ambapo alipewa talaka kwenye mahakama ya Mwanzo Tinde.


Akizungumza na Mwandishi wetu,i Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ngaka bw. Mabula Kuzenza amesema watu waliohusika na mauaji hayo bado hawajafahamika.

“Jana Jumamosi Aprili 29,2023 majira ya saa mbili usiku nilipigiwa simu na majirani wa marehemu kwamba kuna tukio kuwa Mwanandakuna ameuawa kwa kuchomwa na visu shingoni na tumboni, baada ya hapo nikapiga simu polisi kwa hatua zaidi”,amesema Kuzenza.


“Waliomchoma hawajahamika na chanzo cha mauaji bado hakijafahamika, inaelezwa kuwa kuna watu wasiofahamika walionekana eneo hilo lakini kutokana na kwamba eneo hili limechangamka kuna mwingiliano wa watu hakuna aliyedhani kuna tukio lingetokea… Inasadikika huenda hao ndiyo wamefanya mauaji haya.

Tukio la mauaji limetokea kimya kimya baada ya mama huyo kutoka nje kwenda kumwaga uchafu na ndani ya mtu mfupi majirani wakaona mtu kaanguka chini na kubaini kuwa ameuawa, hata haijulikani imetokeaje tokeaje”,ameeleza Mwenyekiti wa Kitongoji.


Akizungumza na Mwandishi wetu, Diwani wa kata ya Tinde Japhar Kanolo amesema mama huyo ameuawa akiwa nyumbani kwake alipopanga kitongoji cha Ngaka kijiji cha Nyambui kata ya Tinde kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na tumboni.


“Nilipewa taarifa kuhusu tukio hili la kikatili majira ya saa mbili usiku ambapo wananchi waliokuwa eneo hilo wanasema mapema jana jioni watu waliona vijana wawili wakichat na simu karibu na nyumbani alipopanga mama huyo. Mama huyo alifarakana na mme wake na juzi ndiyo alipata talaka yake mahakamani 40 ya mali walizopata”,ameeleza Kanolo.


Diwani wa viti maalumu tarafa ya Itwangi Mhe. Hellena Daudi Ng’wana mbuli amelaani tukio hilo huku akiomba vyombo vya sheria kuwachukulia hatua kali watu watakaobainika kufanya mauaji hayo ya kikatili.


“Ukatili huu aliofanyiwa mama huyu ni mbaya, wanakosea sana kuua wanawake. Naomba wananchi waache ukatili na vyombo vya vichukue hatua kali kwa watakaobainika kuhusika na tukio hili”,ameeleza Diwani huyo.

Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ili azungumzie tukio hilo zinaendelea.


Share:

KIWANJA CHA NDEGE CHA SUMBAWANGA KUBORESHWA

Mkoa wa Rukwa waingia katika historia mpya mara baada ya Serikali kupitia Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) kuingia mkataba na Kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group Co. Ltd ya nchini China kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga kwa gharama ya Shilingi Bilioni 55.908 kwa muda wa miezi 18.

Uboreshaji huo ni utekelezaji wa mkakati wa Serikali wa kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii Mkoani humo na ukanda wa Magharibi mwa nchi ya Tanzania ili kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji.

Zoezi la utiaji saini wa mkataba huo uliofanyika katika Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga, mkoani humo umefanyika kati ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Matavila pamoja na Mwanasheria wa TANROADS, Wakili Gurisha Mwanga na kushuhudiwa na wananchi, viongozi mbalimbali wa Serikali na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa.

Akizungumza baada ya Zoezi hilo, Prof. Mbarawa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kuboresha miundombinu pamoja na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) kwa kutoa fedha za utekelezaji wa mradi huo.

Waziri Prof. Mbarawa ameeleza kuwa uboreshaji wa kiwanja hicho utakapokamilika utaruhusu kiwanja hicho kufanya kazi saa 24 yaani usiku na mchana na kitakuwa na uwezo wa kupokea ndege aina ya Boeing Q 400 pamoja na ATR 72.

Amesema utekelezaji wa mradi huo umeletwa mahsusi ili kuchochea shughuli za kiuchumi kama vile kilimo, utalii, uwekezaji, uvuvi, usafirishaji wa mizigo na abiria na shughuli za kijamii kwa ujumla.

"Mapema mwakani wana Sumbawanga mtegemee ndege ya kwanza kutua hapa", amesisitiza Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amefafanua kuwa uboreshaji wa kiwanja hicho pia utahusisha ujenzi wa jengo jipya la abiria, ununuzi na usimikaji wa taa za kuongozea ndege (AGL) na mitambo ya Usalama (DVOR/DME), barabara ya kuingia na kutoka kiwanjani, maegesho ya magari na uzio wa usalama.

Aidha, amesema kiwanja hicho kwa sasa kina barabara ya kuruka na kutua ndege ya kiwango cha changarawe yenye urefu wa kilometa 1,516 na upana wa meta 30 ambapo kupitia mradi huu barabara hiyo itaboreshwa kufikia urefu wa kilometa 1,750 na upana wa meta 30 kwa kiwango cha lami.

Waziri Prof. Mbarawa, ametoa rai kwa Uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuusimamia mradi na vifaa vitakavyotumika katika ujenzi huo pamoja na kuwasisitiza wananchi wetu wanaozunguka eneo la mradi kuepukana na uhalifu wa namna yoyote katika mradi badala yake waulinde mradi huu ili wafaidike na fursa mbalimbali zitakazojitokeza wakati utekelezaji wa mradi ukiwa unaendelea.

"Mkiulinda mradi huu utasaidia kulinda thamani halisi ya mradi lakini pia kukamilika kwa wakati na ubora unaokubalika", amesisitiza Prof. Mbarawa.

Amewaagiza Wataalam wa Wizara, TANROADS, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga (TCAA) na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) na wadau wote kufanya kazi kwa weledi na kusimamia utekelezaji wa mradi huu ili kuhakikisha kuwa mradi unakamilika kwa wakati.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Queen Sendinga, ameishukuru Serikali kwa baraka ya miradi inayoendelea mkoani kwake ambapo ukiondoa kiwanja cha ndege hicho pia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Ntendo - Kizungu (km 25) na barabara ya Matai - Tatanda (km 25) inaendelea vyema.

Mkuu wa Mkoa huyo pia ameahidi kuusimamia uboreshaji wa kiwanja hicho ili uweze kukamilika kwa wakati kwani mkoa huo hauna viporo vya miradi kucheleweshwa.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, ameeleza kuwa uboreshaji wa kiwanja hicho utahusisha ujenzi wa jengo jipya la abiria lenye uwezo wa kuhudumia abiria 150,000 kwa mwaka ambapo Jengo hilo litakuwa na sehemu ya kuongozea ndege.

Matavila ameeleza kwamba upembuzi yakinifu wa kiwanja hicho ulifanywa na kampuni ya Sir Fredrick Snow & Partners Ltd ya Uingereza ikishirikiana na Kampuni ya Belva Consult ya Tanzania kati ya mwaka 2007 mpaka mwaka 2009.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila akisaini mkataba wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbwanga na Mwakilishi kutoka kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group ya nchini China kwa gharama ya Bilioni 55.908 kwa muda wa miezi 18, mkoani Rukwa.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila pamoja na Mwakilishi kutoka kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group ya nchini China wakionesha mkataba wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbwanga mara baada ya kusainiwa, mkoani Rukwa. Uboreshaji huo utatekelezwa kwa muda wa miezi 18 na utagharimu Bilioni 55.908.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza na wananchi wa mkoa wa Rukwa mara baada ya kusiani mkataba wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbwanga utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 55.908, mkoani humo.



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila, akitoa taarifa ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbwanga utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 55.908, wakati wa utiaji saini mkataba wa uboreshaji wa kiwanja hicho na mkandarasi kutoka kampuni ya M/s Beijing Construction Engineering Group ya nchini China, mkoani Rukwa.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendinga, katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbwanga utakaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 55.908, mkoani humo.



Muonekano wa sehemu ya barabara ya kuruka na kutua ndege kwa kiwango cha changarawe katika Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga ambapo Serikali imesaini mkataba wa ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho kwa gharama ya shilingi Bilioni 55.908, mkoani Rukwa. Ukarabati wa barabara hiyo utafanyika kutoka kilometa 1,516 hadi kufikia kilometa 1,750 kwa kiwango cha lami.
Share:

WAZIRI DKT MABULA AFAFANUA UPOTOSHAJI VIWANJA VINAVYOMILIKIWA NA KAMPUNI YA SLIPWAY TOWERS LTD

Na Munir Shemweta, WANMM

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametoa ufafanuzi wa viwanja vinavyomilikiwa kampuni ya Slipway Towers Ltd vilivyopo Msasani Peninsula jijini Dar es Salaam ambapo amemuagiza katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Anthony Sanga kuchunguza kubaini kama kuna wataalam waliohusika katika upotoshaji huo ili waweze kuchukuliwa hatua za haraka za kinidhamu.

Aidha, Dkt Mabula ameelekeza kuwa, kuanzia sasa Manispaa ya Kinondoni inapotaka kupangisha maeneo au eneo ambalo ni kwa matumizi ya umma inatakiwa kijiridhisha kwanza kwa lengo la kujua eneo husika kama mipaka yake haijaingiliana na wapangishaji wengine ili kuepuka migogoro.

Kumbukumbu za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi zinaonesha kuwa viwanja namba 1497, 1498 na 1856 vinamilikiwa kampuni ya Slipway Towers Limited kwa hati namba 29035 ya muda wa miaka 99 iliyotolewa Januari 1, 1980 kwa ukubwa wa hekta 1.383 kama ilivyo kwenye ramani ya usajili namba 18460 ya mwaka 1980.

Hata hivyo, upimaji wa viwanja ulirejewa na kufanyiwa maboresho yaliyoongeza kiwanja namna 1967 ambapo kampuni ya Slipway Towers Ltd iliomba kiwanja husika kuunganishwa kwenye hati moja na maombi kukubaliwa na kusajiliwa Agosti 13, 1998 ambapo ukubwa uliongezeka kutoka hekta 1.383 hadi 1.8759.

Waziri Mabula alitoa ufafanuzi huo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam tarehe 29 April 2023 kufuatia malalamiko yaliyotolewa na mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Somgoro Mnyonge kuhusu umiliki na uendelezaji wa eneo katika viwanja hivyo.

"Ieleweke wazi kuwa mhe. Dkt Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akivutia wawekezaji wengi nchini katika sekta mbalimbali kwa maslahi mapana ya nchi yetu hivyo serikali haitavumilia vitendo vinavyoenda kinyume na azma ya rais kuvutia wawekezaji na tanzania ni sehemu salama kuwekeza" alisema Dkt Mabula.

Amemuelekeza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala kusimamia taratibu zote katika kipindi cha mpito wakati mgogoro katika eneo hilo ukishughulikiwa sambamba na kusimamia pale inapotokea changamoto yoyote kwa kuangalia namna bora ya kufanya mawasiliano kabla ya kutolewa matamko yenye kuleta upinzani.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, uhakiki uliofanywa na wataalam wa wizara yake umebaini kuwa, siyo kweli kwamba mwekezaji kampuni ya Slipway Towers Limited imeingia baharini kwa mita 850 bali zilizotajwa ni mita za mraba ambazo Manispaa ya Kinondoni imempangisha kampuni ya Dorishers ndani ya kiwanja cha hati milki namba 29035 kinachomilikiwa na kampuni ya Slipway Towers Limited.

"Tangu mwaka 1998 hadi sasa wizara haijapata maombi ya Slipway kufanya mabadiliko yoyote kwenye ramani au hati miki na hakuna jambo lolote wizarani linalohusiana na upimaji au umilikishaji unaohusina na kampuni ya Slipway towers ltd, kilichosemwa na meya wa manispaa ya kinondoni kuwa kuna mchakato unaoendelea ndani ya wizara hakipo na hakuna mchakato wala maombi". Alisema Waziri Mabula.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mpango wa uendelezaji upya eneo la Masaki yaani Masaki-Oyesterbay Development Plan ya 2011-2031 ulijadiliwa na kupitishwa na Baraza la Mawaziti hivyo marekebisho yoyote ya mpango wa eneo hilo lazima yapitishwe na Baraza la Mawaziri.

"Kwa hiyo wizara kama wizara hakuna inachoweza kufanya mabadiliko hayo kwa sababu tayari yapo katika mpango wa uendellezaji ulioasisiwa na Baraza la Mawaziri na marekebisho yoyote lazima yapitishwe na baraza hilo". Alifafanua Dkt Mabula.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akifafanua jambo wakati wa kikao chake na waandishi wa habari kufafanua upotoshaji wa viwanja vinavyomilikiwa na kampuni ya Slipway Towers Ltd tarehe 29 April 2023.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Slaam wakati wa kutoa ufafanua wa upotoshaji wa viwanja vinavyomilikiwa na kampuni ya Slipway Towers Ltd tarehe 29 April 2023.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga (Kulia) pamoja na Mpima wa Wizara ya Ardhi Romanus Sanga wakati wa kikao cha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam tarehe 29 April 2023. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)
Share:

CHUO CHA MZUMBE KUZITAFUTIA MASOKO BUNIFU ZINAZOIBULIWA NA WANAFUNZI WAKE



Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la chuo hicho katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha,akizungumza na watumishi wa chuo hicho katika banda la chuo hicho katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.


Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa chuo hicho wakati wa kilele cha Maadhimisho ya maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

CHUO Kikuu cha Mzumbe kimesema kitaendelea kuibua,kuendeleza na kuzitafutia masoko bunifu mbalimbali zinazoibuliwa na wanafunzi wa chuo hicho huku kikidai tayari ina kitengo maalum kwa kusimamia bunifu hizo.

Hayo yameelezwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof.William Mwegoha wakati akizungumza katika banda la chuo hicho katika maonesho ya wiki ya ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Prof Mwegoha amesema wanayafurahia maonesho hayo kwani yanahamasisha bunifu mbalimbali pamoja na masuala ya Sayansi na Teknolojia.

Amesema Mzumbe wanachokifanya ni kuhakikisha wanapromoti bunifu mbalimbali za wanafunzi wao ambapo amedai kwa sasa wana Kitivo cha Sayansi na Teknolojia.

Amesema katika mambo wanayofanya katika kitivo hicho ni pamoja na wanafunzi kuja na bunifu mbalimbali ambazo zinaenda kutatua changamoto za wananchi.

Amesema bunifu ambazo wamekuja nazo ni kwa ajili ya kupambana na changamoto za afya,mazingira,usafirishaji na uchukuzi.

“Sasa hivi tuna kitengo maalum kabisa kwa ajili ya kusimamia bunifu,baada ya hapa hawa vijana ili zile waweze kuzitangaza zifike mahali ambako wataweza kutengeneza biashara ambazo zitawainua kiuchumi.

“Hii inaendana na sera ya kitaifa ya kuhakikisha kwamba vijana wanajiajiri vijana wanaokuja hapa wanakuja na mawazo yao na tunawapa ushuri na baadae kuzigeuza kuwa biashara ikiwa ni pamoja na kuwatafutia wafanadhili ambao watazikuza,”amesema Prof Mwegoha

Amesema kupitia kituo hicho cha ubunifu wameanza kwenye kituo atamizi ambacho kinawataalamu kwa ajili ya kukuza idea zao.

Amesema chuo kinakiwezesha kitengo hicho ili kuendeleza miradi na waendelee kuwepo na kuwafikisha katika ndoto zao.

“Tutaendelea kuzisapoti mpaka pale ambapo wanaweza kuziendeleza na kuwa fursa.Hata wakiamua kwenda kufanya hizo kazi wana mahali pa kuanzia,”amesema Prof Mwegoha

Amesema katika bunifu walizokuja nazo ni pamoja na jiko ambalo linatumia mkaa wa taka kwa ajili ya kulinda mazingira.

“Katika bunifu ambazo tumekuja nazo ni jiko ambalo linatumia mkaa wa taka kwa ajili ya nishati na hii ni moja ya bunifu ambazo zipo nyingi ili serikali ikipiga marufuku mkaa tuweze kusapoti, majiko yanatumia taka lakini yanatoa nishati kubwa,”amesema Prof Mwegoha
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 30,2023














Share:

POLISI WATOA UFAFANUZI AJALI YA NAIBU WAZIRI DUGANGE, WAFUNGUKA MADAI KULIKUWA NA MWANAMKE





Gari ya Serikali Vs Gari binafsi ya Mhe Dugange iliyopata Ajali




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange leo tarehe 29 Aprili 2023 wakati alipofika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa kumjulia hali baada ya kupata ajali ya gari.




Dkt. Dugange alipata ajali usiku wa tarehe 26 Aprili 2023 wakati akiendesha gari yake binafsi Jijini Dodoma ambapo kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa.
Share:

Saturday 29 April 2023

MTOTO WA MIAKA 7 ACHOMWA MOTO NA MAMA YAKE KISA KALA KIPORO CHA WALI



Mikono ya mtoto aliyochomwa moto na mama yake mzazi

Na Suzy Luhende, Shinyanga 

Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga linamshikilia Grace Godwin(23) Mkazi wa Mtaa wa Sido Kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga kwa tuhuma za kumchoma moto mikono yote miwili mtoto wake kwa tuhuma za kula wali.

Tukio hilo lilitokea  April 27, 2023 katika Mtaa huo wa Sido baada ya mama huyo kumchoma moto mtoto wake mwenye umri wa miaka saba anayesoma darasa la kwanza kwa madai ya kula wali uliobaki (kiporo) bila kuruhusiwa.


Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari wanamshikilia mwanamke huyo kwa hatua zaidi za kisheria na upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.


“Tunamshikilia mtuhumiwa ambaye anaitwa Grace ni mama mzazi wa mtoto anayedaiwa kuchomwa moto mikono yake yote miwili,tukio hili ni baya na vitendo hivyo vya ukatili tunalaani vikali visijirudie”amesema Kamanda Magomi.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Sido Kata ya Ibinzamata Emmanuel Kayange amesema alipata taarifa za tukio hilo na kuamua kufuatilia na kubaini kweli mtoto kachomwa moto na mama yake mzazi kama inavyodaiwa.

Mwenyekiti amesema kutokana na tukio hilo walimuita mama mzazi wa mtoto pamoja na bibi yake Agnes Mgaya na kuwahoji ambapo walibaini mtoto huyo ana siku mbili amechomwa moto wakiendelea kumpa matibabu nyumbani.


Aidha mtoto aliyechomwa moto mikono yote miwili amesema mama yake alimchoma moto kwa kutumia mfuko ambao aliuwasha na kuniwekea mikononi kwa sababu nilikula wali uliokuwa umebaki.

Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Sido wamesema kitendo kilichofanywa na Grace Godwin kumchoma moto mtoto wake kwa madai ya kula chakula ni ukatili mkubwa ambao unapaswa kukemewa vikali ili kukomesha matukio hayo.


Fatuma Ramadhan mkazi wa mtaa huo amesema mtoto aliyefanyiwa ukatili na mama yake mzazi amekuwa akipigwa mara kwa mara na kuiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukubwa wa tatizo kwa kuwahoji mama na bibi wa mtoto huyo.


“Kwa kweli nashindwa kuelewa kwanini watu hawataki kusema ukweli, huyu mtoto anaishi kwa shida anapigwa mno hata ukimuangalia mgongoni na kwenye mikono ana alama za fimbo hili tukio la kuchomwa moto ndilo ambalo limeonekana”, amesema Fatuma.


Shaaban Juma mkazi wa eneo hilo amesema tukio hilo linasikitisha kwani mtoto alikuwa na haki ya kula chakula kwa kuwa hapo ndiyo nyumbani badala ya kuanza kuzunguka mitaani akiomba omba chakula.


Juma amewataka wazazi na walezi kuwa na moyo wa upendo na hofu ya Mungu kwani watu wanaogopa moto, lakini wengine wanachukuwa moto huo na kumchoma binadamu mwenzio ambaye ni mtoto wako jambo ambalo linasikitisha.


Kwa upande wao wadau wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto akiwemo Anascholastika Ndagiwe,amesema mtoto huyo amefanyiwa unyama na mama yake na kuziomba mamlaka husika kuchukuwa hatua kali.


Amesema matukio ni mengi ya ukatili kwa watoto yanafanyika hivyo na serikali inatakiwa kuchukuwa hatua kali kwa watu wanaofanya matukio hayo ili kuyakomesha na kuwawezesha watoto kuishi katika mazingira salama.
Mtoto aliyechomwa moto na mama yake mzazi
Anascholastika Ndagiwe mdau wa kupinga vitendo vyaukatili mkoani Shinyanga





Share:

TCRA YAWATAKA WASFIRISHAJI WA VIPETO KUJISAJILI NA WENGINE KUHUISHA LESENI

*Matapeli kutuma ujumbe mfupi waibukia Viwanja vya ndege


Na Chalila Kibuda,

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imetoa wito kwa wadau wa posta wenye leseni kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu, kanuni na sheria pamoja na kuhuisha leseni zao ili wafanye kazi zao kwa ufanisi na kutambulika zaidi.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Meneja TCRA Kanda ya Mashariki Ikuja Jumanne katika utoaji mafunzo kwa wadau wa posta kupitia kampeni walioanzisha ya kutambua umuhimu wa kukata leseni na ambao bado wakate kwani itawasaidia kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi.

Aidha amesema kuwa elimu hiyo imekuja kutokana na uwepo wa malakamiko ya wateja kupotelewa na vipeto na vifurushi vyao kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha hivyo kutapeli watu na kushindwa kujua wamdai nani.

Hata hivyo amesema kupitia kampeni walioanzisha ya “Tumachapuchapu kwa Usalama “ itawezesha elimu kuwafikia wananchi wengi kupitia vipeperushi, vyombo vya habari, vituo vya usafiri na elimu zinazoendelea kutolewa na TCRA ili kupunguza wimbi la upotevu wa vipeto na vifurushi.

Ameongeza kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) haihusiki tu na usimamizi wa Mawasiliano bali pia wana kitengo cha posta ambacho hushughulikia utumwaji wa vipeto vyenye kilogramu 2 na vifurushi vyenye kilogramu 30 ndani na nje ya nchi kupitia kampuni zilizosajiliwa na mamlaka hiyo.

Amesema kuwa kuanzishwa kwa kitengo hich cha posta kumewezesha ongezeko la pato la taifa kkutokana na kusajiliwa kwa nakampuni hayo ya utumaji vifurushi na vipeto pamoja na kuongeza ajira kwa watanzania.

Kwa upande wao wada wa posta walioshiriki katika mafunzo hayo wamemshukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kwa kuwapatia elimu hiyo ambayo itasaidia kutatua changamoto mbalimbali walizokuwa wanakumbana nazo wakati wa utumaji wa vipeto na vifurushi.

Hatahivyo wameiomba Mamlaka hiyo kuendelea kushirikiana na wadau hao wa posta katika kukabiliana na wimbi la watu wasiofuata taratibu za usajili ambao huwasababishia usumbufu pindi mteja anapopoteza kipeto au kifurushi na kushindwa kujua amdai nani kwani aliowapa watume hawajasajiliwa.

Meneja wa Basi la Gallaxy Magreth Kibiki amesema kuwa wapo watu hawana mabasi lakini wanafanyabiashara ya kusafirisha vipeto na kuleta usumbufu kwao wakati mzigo umepotea na kudai walipwe wakati hawana stakabadhi ya malipo ya basi husika.

Kibiki amesema wananchi wanatakiwa kuwa na uangalifu wa kutuma mizigo kwenda katika kampuni ambazo zinafanya biashara kwa ya kusafirisha vipeto kwa njia ya halali.

Afisa Mauzo na Masoko wa ATCL Hellon anasema kuwa wanapata changamoto na matepeli wanawatumia ujumbe mfupi kuwatumia watu kuwa na mzigo ATCL wakiomba watume fedha ambapo waliotumiwa ujumbe wanatuma na kuanza kufatilia ATCL kupatiwa mzigo na kuleta usumbufu kwao.

Amesema kuna baadhi wanasafirisha mizigo kwenda nje wanatumia mwanya wa abiria wasio na mizigo hali amabayo ni changamoto kwa wenye leseni kukosa kufanya biashara na hao baadhi ya watu wanaotumia fursa isiyo halali kwao.


Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Kanda ya Mashariki Mhandisi Jumanne Ikuja akizungumza na waandishi habari kuhusiana na wasafirishaji wa vipeto kufuata sheria jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya watoa huduma za vipeto wakiwa katika mkutano wa elimu ya utoaji wa huduma hiyo iliyoandaliwa na TCRA Kanda ya Mashariki.

Afisa Masoko na Mauzo wa ATCL Hellon akizungumza kuhusiana na matapeli wanaowatumia watu ujumbe wa mizigo wakati wao wakiwa hawajafanya huduma kwa mhusika ambaye alitumiwa ujumbe, jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Basi la Gallaxy Magreth Kibiki akizungumza kuhusiana na TCRA kuwasaidia kwa watu wanaofanya biasharara ya kusafirisha vipeto bila kusajiliwa, jijini Dar es Salaam.
Share:

GGML YAIBUKA MUONESHAJI BORA KATIKA MAONESHO YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI 2023

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo Afisa Uhusiano wa GGML, Doreen Denis baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi ya kundi la muoneshaji bora katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayoendelea mkoani Morogoro.
Baadhi ya wafanyakazi wa GGML, wakiwa katika picha ya pamoja kufurahia ushindi wa muonesha bora na mbunifu bora katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayofanyika mkoani Morogoro.
Afisa Uhusiano wa GGML, Doreen Denis (kushoto) akimfafanulia jambo mwananchi aliyetembelea banda la maonesho la kampuni hiyo katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayoendelea katika Viwanja vya Tumbaku mkoani Morogoro. Wapili kushoto ni Afisa Mawasiliano Afisa Mawasiliano mwandamizi wa GGML, Laurian Theophil Pima.
Daktari wa Kituo cha Afya cha GGML kutoka Idara ya Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo ya GGML, Dk. Subira Joseph akitoa huduma za matibabu kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la huduma za afya la kampuni hiyo kwenye maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi yanayofanyika mkoani Morogoro.
KATIKA maadhimisho ya siku ya afya na usalama mahali pa kazi yanayoratibiwa na Wakala wa afya na usalama mahali pa kazi (OSHA), Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetangazwa muoneshaji bora (Overall best exhibitor) miongoni mwa kampuni zote zilizoshiriki maonesho hayo mjini Morogoro.

Pia imetangazwa kuwa mbunifu bora wa maonesho hayo yaliyoanza Aprili 26 na kutarajiwa kuhitimishwa Aprili 30 mwaka huu katika viwanja vya Tumbaku mkoani humo.

Kilele cha maonesho hayo yenye kauli mbiu Mazingira Salama na Afya ni Kanuni na Haki ya Msingi Mahali pa Kazi.” kimefanyika Aprili 28,2023 mkoani Morogoro.

Share:

WANANCHI WATEMBELEA BANDA LA CHUO CHA TAKWIMU MASHARIKI MWA AFRIKA WIKI YA UBUNIFU 2023 DODOMA




MKUU wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika, Eusebius Mwisongo,akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la Chuo hicho wakati wa Kilele cha Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


Mhadhiri Msaidizi na Mratibu wa maswala ya Udahili Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika,Samuel Marandu,akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea banda la Chuo hicho wakati wa Kilele cha Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


WANANCHI mbalimbali wakiendelea kupata elimu katika banda la Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika,walipotembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika Dr.Tumaini Katunzi akisaini kitabu Cha wageni katika Banda la Chuo hicho wakati wa Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


WANAFUNZI wakisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembela banda la Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika,wakati wa Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


WASHIRIKI kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda la Chuo hicho mara baada ya kumalizika kwa Kilele cha Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yaliyomalizaka leo Aprili 28,2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma

Na.Alex Sonna-DODOMA Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika, Eusebius Mwisongo amesema wamebuni mifumo itakayomsaidia mwananchi kufanya shughuli zake kiurahisi ili kuwa na mafanikio kwa haraka.

Hayo ameyasema leo Aprili 28,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la Chuo hicho katika Maonesho ya wiki ya ubunifu 2023 yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yanayofanyika uwanja wa Jamhuri Dodoma

Bw.Mwisongo amesema kuwa lengo ni kuujulisha umma umuhimu na faida za mifumo ya TEHAMA inayotengenezwa chuoni hapo.

“Tumekuja na mifumo sita ambayo inahusu ufatiliaji wa magari, mkulima, kufatilia mahudhulio ya wanafunzi na pamoja na mfumo wa vikoba”, amesema Mwisongo.

Ameitaja mifumo hiyo ni pamoja na E- Task Management,Vehicle Management System, e-mkulima,Class Tracking Attendance System, e-management

Ameeleza kuwa Mifumo hiyo inafanya kazi tofauti kulingana na mahitaji ya mteja mfano kwa taasisi za elimu kuna mfumo wa class tracking attendance ambao huonyesha idadi ya wanafunzi walio hudhulia kipindi husika pamoja na mwalimu.

Lakini ameongeza kuwa wana mfumo wa e- task manengment ambao unawezesha mkuu wa kitengo kupanga majukumu kwa watu wake na wahusika hupata ujumbe wa majukumu waliopangiwa na kutekeleza majukumu yao na kuleta taarfa kupitia mfumo huo.

Hivyo ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda lao hili kujua ni mafunzo gani wanatoa na huduma zinazopatikana katika banda lao hususani mifumo katika kuendesha shughuli za kijamii.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 29,2023

























Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger