Thursday, 27 April 2023

POLISI SHINYANGA WAKAMATA KONDOMU, BUNDUKI ZA MAKAMPUNI YA ULINZI ZIKIAZIMWA NA WAHALIFU

...
Na Halima Khoya  & Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanya ukaguzi wa kushitukiza kwenye malindo ya kampuni mbalimbali za ulinzi na kufanikiwa kukamata Bunduki 5 ambazo hazikufuata utaratibu wa kisheria zikitumika kuazimishwa kwa wahalifu huku likikamata vipodozi vyenye viambata vya sumu ambavyo haviruhusiwi kwa matumizi ya binadamu pamoja na bidhaa mbalimbali yakiwemo maboksi 9 ya kondomu zinazopaswa kutumika kwenye vituo vya afya na mashirika yanayosika na masuala ya kudhibiti UKIMWI.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamisi Aprili 27,2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amezitaja zilizokamatwa kufuatia ukaguzi wa kushitukiza wa malindo ya kampuni mbalimbali kuwa ni Bunduki aina ya MARK IV yenye namba TZ car 89936 na risasi 04 na Bunduki aina ya MARK IV yenye namba K 9239 na risasi 03.


Silaha zingine ni Bunduki aina ya MARK IV yenye namba D 6000 na risasi 01, Bunduki aina ya MARK IV yenye namba MG 564884 na risasi 02 na Short gun Birmingham England na risasi.


“Tumekamata bunduki hizi tano ambazo zilikuwa zikimilikiwa kinyume cha utaratibu chini ya kifungu 10(7) na 60 Cap 38 cha Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi ya Mwaka 2015 pamoja na kanuni zake GN 334 ya tarehe 30/12/2016 kanuni namba 14(2) na (3).
“Pia kupitia misako na Operesheni mbalimbali katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia tarehe 22/03/2023 hadi tarehe 26/04/2023 tumefanikiwa kukamata vitu na vielelezo mbalimbali ambavyo ni magodoro mawili, TV 05, Remote 01 ya Star X, Pard 05, PlayStation PS-3 01, Pikipiki 06 (MC 248 CYP- SANLG, MC 700 AQL-SANYA, MC 815 DQC, MC 494 DCM- KINGLION, MC 909 CEV-HAOJUE na MC 134 DDL-KINGLION), Redio Subwoofer 03, Redio ndogo 02, Sigara aina ya CLUB box 3 na pakiti 15 aina mbali mbali, Computer 02, Vitenge doti 05, Simu smart aina ya Honor, Saa 02 aina ya Titarium, Mtungi wa Gesi, Draya 01, Pombe ya moshi lita 120, Meza ya kuchezea kamari na karata zake tatu, Vifaa vya kupiga ramli chonganishi maarufu MBIGI, Panga 02 kubwa, Viuatilifu vya Serikali vya kuua wadudu wa Pamba”,ameeleza Kamanda Magomi.

Amevitaja vitu vingine vilivyokamatwa ni pamoja na Flash Disk ya 16GB aina ya Toshiba 02, Bhangi Kilogram 327 na kete 85, Mirungi bunda 05, Madumu tupu 14 yenye ujazo wa lita 20, Madumu 16 yenye ujazo tofauti tofauti yakiwa na mafuta ya Petrol Lita 269 yote yakidhaniwa kuibiwa kwenye mradi wa ujenzi wa reli ya SGR.
“Vitu vingine ni Vipodozi vyenye viambata vya sumu ambavyo haviruhusiwi kwa matumizi ya binadamu (Epiderm crème box 01, Betasol crème box 03, CaroLight box 01), Pombe kali aina ya Hakiri box 12, Kondom box 09 zikiwa kwenye maduka ya watu binafsi ambazo zinazopaswa kutumika kwenye vituo vya afya na mashirika yanayosika na masuala ya kudhibiti UKIMWI.
 Mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku pakiti 100, Kiberiti bunda 02, Extention 02, Lita 67 ya mafuta ya kula na bidhaa mbali mbali za madukani”,amesema.


Katika hatua nyingine amesema Jeshi la Polisi kupitia kitengo chake cha Upelelezi kwa kipindi hicho cha mwezi mmoja limewafikisha watuhumiwa 132 mahakamani katika kesi 129 zilizoripotiwa katika kipindi hicho ambapo mpaka sasa kesi zilizopata mafanikio ni kesi 62 ikiwa ni pamoja na watuhumiwa kufungwa jela/kifungo cha nje pamoja na kulipa faini.


Miongoni mwa kesi hizo 62 zipo kesi ambazo zimehusisha makosa ya ukatili wa kijinsia ambazo ni kumpa mimba Mwanafunzi kesi 04, kubaka kesi 02 na kulawiti kesi 01.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea kuwaasa wananchi kufuata sheria za nchi wakati wote na kutojihusisha na vitendo vya kiuhalifu kwa namna yoyote ile.


Aidha Jeshi la polisi linatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa dhidi ya uhalifu na wahalifu ili kutokomeza vitendo hivyo miongoni mwa jamii inayotuzunguka na halitokuwa na muhali kwa yeyote yule ambaye atajihusisha na vitendo vya kiuhalifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 27,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 27,2023
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 27,2023
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 27,2023

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Aprili 27,2023
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akionesha vitu mbalimbali vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger