Tuesday 31 March 2020

IGP Sirro Awaonya Watalii Kutojihusisha Na Biashara Ya Dawa Za Kulevya

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa Jeshi la Polisi kamwe halitamvumilia mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo kujihusisha na uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya pamoja na uhalifu mwingine.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akifungua kituo cha utalii Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja kisiwani Zanzibar, huku akiwataka watendaji wa Jeshi la Polisi nchini kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa weledi na kwa kufuata misingi ya kisheria na kufuata maelekezo ya Jeshi hilo.

Kuhusu Corona IGP SIRRO ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kufuata maelekezo mbalimbali yanayoendelea kutolewa na viongozi wa kiserikali pamoja na wataalamu wa masuala ya afya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini  Unguja Mhe.Vuai Mwinyi Khamis, amesema kuwa, mkoa huo unaidadi kubwa za hoteli za kitalii na kwamba ujenzi wa kituo hicho cha Polisi utasaidia zaidi katika kukabiliana na kuzuia uhalifu.

Ujenzi wa kituo hicho ambacho kimegharimu zaidi ya shilingi milioni 64 zilizotolewa na wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa utalii visiwani humo.


Share:

Waziri Mpina Ashtukia Upigaji Wa Bilioni 2.6 Ujenzi Maabara Ya Uvuvi

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesimamisha malipo yote kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Petra Construction co. Limited inayojenga maabara ya kisasa ya Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kituo cha Dar es Salaam hadi uhakiki wa gharama halisi za mradi huo utakapokamilika baada ya kubaini kuwepo matumizi mabaya ya fedha za umma kiasi cha shilingi bilioni 2.6

Hivyo Waziri Mpina ameunda tume ya kiuchunguzi itakayofanya kazi kwa siku saba na kuwahusisha wataalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kubaini ukweli wa gharama halisi za mradi huo.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) jijini Dar es Salaam, Waziri Mpina alisema amebaini mradi unaojengwa miundombinu yake ni midogo ikilinganishwa na mkataba ulioridhiwa wa sh. bilioni 2.6 na kwamba taarifa ya uhakiki ya mradi huo itawasilishwa wizarani ikiwa na mapendekezo ya hatua za kuchukua dhidi ya wizi huo wa fedha za umma.

WaziriMpina alisema thamani halisi ya mradi huo hailingani na fedha zilizotolewa na Serikali huku akitolea mfano baadhi ya miradi ya ujenzi wa majengo mbalimbali ikiwemo vituo vya afya na hospitali za wilaya zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini.

Hata hivyo wakati wa mjadala ukiendelea wa kuhoji matumizi ya fedha hizo kwenye mradi huo, mmoja wa wakandarasi wanaojenga majengo hayo alimweleza Waziri Mpina kuwa hadi mradi utakapomika kutabaki ‘chenji’ kiasi cha shilingi milioni 500 jambo lililotilia mashaka na kuibua maswali mengi juu ya gharama halisi za mradi huo.

Kufuatia mkanganyiko huo wa maelezo ya mkandarasi na hali halisi iliyoonekana kwenye mradi huo ndipo Waziri Mpina akalazimika kutangaza uamuzi huo wa kuundwa tume hiyo ili iweze kufanya tathmini ya gharama ya mradi iliyofanywa na Mshauri mwelezi wa mradi, namna zabuni ya kumpata mkandarasi ilivyotangazwa na namna mshauri mwelekezi alivyopatikana na hali ya ujenzi unavyoendelea kwa sasa ili kujua dosari ilisababishwa na nani.

Hivyo Waziri Mpina akabainisha kuwa baada ya kazi hiyo ya uhakiki kukamilika ndani ya siku saba ukweli utajulikana na hatua zote zilizopitiwa katika mradi huo ili kubaini kama Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2004 ilikiukwa ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa wote watakaohusika na ubadhirifu huo wa fedha za umma.

“Sikubaliani na hizi gharama za mradi majengo na miundombinu ni midogo ikilinganishwa na mkataba wa bilioni 2.6, BOQ ilihakikiwa na wahandisi wa wizara, washauri waelekezi walijiridhisha kwamba iko sawa na ujenzi ukaenda hadi bilioni 2.6 mtu yeyote akija anakataa” alihoji Waziri Mpina.

Hivyo Waziri Mpina ameagiza ujenzi wa mradi huo uendelee bila kusimama na ukamilike ifikapo Aprili 20 mwaka huu kama mkataba unavyoeleeza na baada ya jengo litazinduliwa ikiwa ni sehemu ya kuleta mageuzi makubwa ya sekta ya uvuvi kupitia eneo hilo muhimu la utafiti.

“Nitaleta timu ya ukaguzi itakayofanya uhakiki wa thamani ya fedha katika ujenzi wa jengo hili, kuanzia kwenye kutangaza tenda yenyewe, thamani ya mradi, kumpata mkandarasi mwenyewe, cost estimates zilizofanywa na wizara na baadae watafanya uhakiki wa kinachoendelea kujengwa hapa na kujua thamani halisi inayotakiwa na kwanini mradi huu upitishwe hadi kusainiwa”alihoji Waziri Mpina.

Menejawa Mradi wa Swiofish, Flora Luhanga alisema mradi huo wa ujenzi wa Jengo la Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi ulianza Juni 10, 2019 kwa gharama ya shilingi bilioni 2, 609,491,754 unajengwa na Mkandarasi Kampuni ya Petra Construction Limited na kusimamiwa na Kampuni ya YP Architect.

Luhangaalisema mradi huo unajumuisha pia ujenzi wa uzio, ofisi ya walinzi, kuchimba kisima cha maji, ujenzi wa tenki la maji ya mvua na kujenga mnara wa maji.

Mkandarasiwa Mradi huo, Nicholaus Mlayi alisema hadi sasa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 70 na tayari ameshalipwa shilingi milioni 963 na unatarajia kukamilika mwezi Aprili.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Uvuvi, Magese Bulayi alimhakikishia Waziri Mpina kuwa maagizo yote aliyoyatoa atayasimamia kikamilifu hasa katika kuangalia thamani ya fedha ‘value for money’ katika mradi huo na kwamba hatua stahiki zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuhusika katika mchakato huo.


Share:

Afariki kwa kupigwa na radi akiendesha pikipiki Toka Shambani

Mkazi wa kata ya Kabungu mkoani Katavi, Paulo Chundu (27) amefariki dunia kwa ya kupigwa na radi wakati akitoka shambani.

Tukio hilo lilitokea machi 29 mwaka huu majira ya saa 12: 45 jioni katika mbuga za kalilankulukulu kata ya kabungu wilayani Tanganyika mkoani katavi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoni katavi Benjamin Kuzaga amesema kijana huyo alikutwa na umauti akiwa katika mbuga hiyo akiendesha pikipiki kutokea katika Kijiji cha ikaka akielekea nyumbani kwake.

Kamanda alisema majira ya saa 12:45 alipatiwa taarifa za kijana huyo kufariki kwa kupigwa radi akiwa anatokea shambani kuelekea nyumbani

Baba mdogo wa kijana huyo, John Laurent alisema alimuagiza shambani kumpeka mtu wa kufanya kazi za shambani ikiwemo kutoa majani, hivyo wakati anarudi akafariki kwa kupigwa na radi.

Alisema tukio hilo limemuumiza na kwamba mtoto huyo aliachiwa na kaka yake baada ya kufariki na kupewa jukumu la kumlea.


Share:

Nafasi Mpya Za Kazi 100 Zilizotangazwa Wiki Hii na Makampuni Mbalimbali

Share:

Meya wa Manispaa ya Iringa Aliyeng'olewa kukabidhi ofisi leo

Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe amesema atakabidhi ofisi na gari la meya leo Jumanne asubuhi baada ya kukamilisha taratibu za kiofisi.

Kimbe ametoa ufafanuzi huo kwa waandishi wa habari waliofika ofisini kwake kutaka kujua kwanini anaendelea na kazi licha ya kuondolewa madarakani siku chache zilizopita.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Hamid Njovu amesema kanuni zinamtaka meya huyo kuondoka ofisini ndani ya siku 30 na hivyo anatakiwa kukabidhi ofisi na gari mara moja.

Akizungumzia malalamiko ya meya kuwa hakutendewa haki katika mchakato upigaji kura, Njovu amesema uamuzi wa madiwani wa CHADEMA kutoandika chochote kwenye karatasi ya kura ndicho kilichomuangusha.

Aidha, amewaondoa hofu wananchi kuwa kazi za meya zitafanywa na Naibu Meya, Joseph Lyata, na watendaji wake wataendelea kutoa huduma kama kawaida.


Share:

Atiwa Mbaroni Kwa Kumfundisha Mbwa Kuendesha Gari

Mwanaume mmoja kutoka Lakewood Washington nchini Marekani, amekamatwa kwa kosa la kumfundisha Mbwa wake mwenye jinsia ya kike kuendesha gari kwa spidi, hali iliyopelekea kusababisha ajali.

Jamaa huyo alimuweka Mbwa wake katika siti ya dereva, ambapo amesababisha ajali ya gari mbili zilizokuwa mbele yake bahati nzuri hakukuwa na mtu aliyepata majeraha kwenye ajali hiyo.

Ripoti ya msemaji wa Jeshi la Polisi la Washington State Patrol amesema  "Gari la mtuhumiwa lilikuwa linaendeshwa kwa spidi sana tena isiyo ya kawaida, ameendesha maili 109 kwa muda wa saa moja,na alikuwa anajaribu kutukwepa lakini imeshindikana, tunashukuru baada ya ajali hiyo hakukuwa na mtu yeyote aliyepata majeruhi imekuwa kama miujiza".

Pia  ameendelea kusema tayari wanamshikilia mtuhumiwa huyo kama atataka kuachiwa kwa dhamana itabidi alipe fedha za Kitanzania Shilingi milioni 19, na mbwa wake amehifadhiwa kwenye mazingira ya wanyama wengine baada ya mmiliki wake kukamatwa.

Kwa upande wa mtuhumiwa anayemmiliki mbwa huyo amejitetea kwa kusema, alikuwa anamfundisha  mbwa wake jinsi ya  kuendesha gari.


Share:

Spika Ndugai Ataka Tusiwaige Wazungu Katika Kupambana Na Virusi Vya Corona

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa kama nchi haiwezi kuchukua tahadhari kama zilivyochukuliwa na Mataifa mengine duniani ya kupambana na Virusi vya Corona kwa kuwa watu wengi nchini maisha yao ni ya kubangaiza siku kwa siku.

Hayo ameyabainisha leo Machi 31, 2020, Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 Mkutano wa 19.

"Hatuwezi kuchukua measure za wazungu na kuzi copy na ku- paste hapa kwetu kama zilivyo, tutaua watu wetu, lazima tuangalie maisha yetu ya Kitanzania na kujaribu kuchukua hatua kufuatana na mazingira yetu" amesema Spika Ndugai.

Amesema katika maeneo yenye masoko wanatakiwa kuchukua hatua kadhaa kama kuweka maji ya kunawa na sabuni, kutokaa karibu ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

“Kuna nchi polisi wanapiga watu viboko ikilazimika huko Serikali itafanya lakini hatuishauri kwa sasa, tunajaribu kuelimisha zaidi, kutoa wito na kumuomba Mungu atuepushe na janga hili ambalo limezitikisa nchi zenye uchumi mkubwa,” amesema Ndugai 


Share:

Halima Mdee Ashauri Wabunge Wote Wapimwe Virusi Vya Corona

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma
Mbunge wa jimbo la Kawe jijini  Dar Es  Salaam Mhe.Halima  Mdee ameishauri  Serikali kufanya mchakato wa kupima Corona wabunge wote na watakaobainika wawekwe karantini.

Mhe.Mdee amesema hayo leo Machi 31,2020 bungeni jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa inatakiwa kila mbunge apimwe homa ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya corona[COVID -19]na akibainika  na maambukizi ya  virusi hivyo atengwe eneo maalum[karantini] na wale watakaobainika kutokuwa na maambukizi waendelee na mkutano ili kujadili bajeti kuu ya serikali ikiwa ni mkutano wa Mwisho kuelekea uchaguzi mkuu.

“Leo wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi wote,kwa nini tusipime wote atakayebainika ana virusi apelekwe karantini na akiwa salama abaki hapa kujadili mambo ya msingi kwa mstakabali wa taifa letu  maana ni mkutano wa mwisho”amesema.

Naye,Mbunge wa   Iringa Mjini  Mch.Peter  Msigwa ameiomba serikali kuja na mpango wa pamoja katika kujadili katika mapambano ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu inayosababishwa na virusi vya corona[COVID-19].

Spika wa bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai amesema katika mkutano wa bunge  la bajeti  ni vyema majadiliano ya pande zote mbili yakazingatiwa huku akitoa wito kwa wabunge kusikilizana na kuelekeza zaidi kwenye bajeti kwani ni mkutano wa Mwisho ambapo bunge litavunjwa kuelekea uchaguzi mkuu  2020.

“Kikao ni chetu kisiwe cha upande mmoja au watu wachache hata kidogo kwa hiyo natoa wito kusikilizana kwa pande zote mbili na ni vyema zaidi mbunge ukajielekeza kwenye bajeti kuliko ukasimama na yako tu ni muhimu sana kuzingatia muda”amesma.

Katika hatua nyingine Mhe.Ndugai ametoa maelekezo kwa serikali kuandaa majibu haraka iwezekanavyo juu ya Hoja Za Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali[CAG] zilizowasilishwa hivi karibuni kwa  Mhe.Rais .


Share:

WAZIRI MPINA ASHTUKIA UPIGAJI WA BILIONI 2.6 UJENZI MAABARA YA UVUVI, AAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA NDANI YA SIKU 7


 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akipata maelezo ya namna ya shughuli ya ujenzi wa mradi wa jengo la Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kituo cha Dar es Salaam  kutoka kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Petra Constuction co. Limited, Nicholaus Mlayi alipotembelea mradi huo Kunduchi Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akipata ufafanuzi kutoka kwa Mshauri Mwelekezi wa Kampuni ya Y&P Architect inayosimamia Mradi wa Ujenzi wa Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kituo cha Dar es Salaam, Anna Shayo alipotembelea mradi huo Kunduchi Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Wetu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akiangalia ramani ya mradi wa jengo la Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI) Kituo cha Dar es Salaam baada ya kutembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo hayo na kuunda tume kuchunguza mradi huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TAFIRI, Dk. Ismael Kimerei . Picha na Mpiga Picha Wetu.

 Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesimamisha malipo yote kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Petra Construction co. Limited inayojenga maabara ya kisasa ya Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kituo cha Dar es Salaam hadi uhakiki wa gharama halisi za mradi huo utakapokamilika baada ya kubaini kuwepo matumizi mabaya ya fedha za umma kiasi cha shilingi bilioni 2.6

Hivyo Waziri Mpina ameunda tume ya kiuchunguzi itakayofanya kazi kwa siku saba na kuwahusisha wataalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kubaini ukweli wa gharama halisi za mradi huo.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya  Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI)  jijini Dar es Salaam, Waziri Mpina alisema amebaini mradi unaojengwa miundombinu yake ni midogo ikilinganishwa na mkataba ulioridhiwa  wa sh. bilioni 2.6 na kwamba taarifa ya uhakiki ya mradi huo itawasilishwa wizarani ikiwa na mapendekezo ya hatua za kuchukua dhidi ya wizi huo wa fedha za umma.

Waziri Mpina alisema thamani halisi ya mradi huo hailingani na fedha zilizotolewa na Serikali huku akitolea mfano baadhi ya miradi ya ujenzi wa majengo mbalimbali ikiwemo vituo vya afya na hospitali za wilaya zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini.

Hata hivyo wakati wa mjadala ukiendelea wa kuhoji matumizi ya fedha hizo kwenye mradi huo, mmoja wa wakandarasi wanaojenga majengo hayo alimweleza Waziri Mpina kuwa hadi mradi utakapomika kutabaki ‘chenji’ kiasi cha shilingi milioni 500 jambo lililotilia mashaka na kuibua maswali mengi juu ya gharama halisi za mradi huo.

Kufuatia mkanganyiko huo wa maelezo ya mkandarasi na hali halisi iliyoonekana kwenye mradi huo ndipo Waziri Mpina akalazimika kutangaza uamuzi huo wa kuundwa tume hiyo ili iweze kufanya tathmini ya gharama ya mradi iliyofanywa na Mshauri mwelezi wa mradi, namna zabuni ya kumpata mkandarasi ilivyotangazwa na namna mshauri mwelekezi alivyopatikana na hali ya ujenzi unavyoendelea kwa sasa ili kujua dosari ilisababishwa na nani.


Hivyo Waziri Mpina akabainisha kuwa baada ya kazi hiyo ya uhakiki kukamilika ndani ya siku saba ukweli utajulikana na hatua zote zilizopitiwa katika mradi huo ili kubaini kama Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2004 ilikiukwa ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa wote watakaohusika na ubadhirifu huo wa fedha za umma.
 “Sikubaliani na hizi gharama za mradi majengo na miundombinu ni midogo ikilinganishwa na mkataba wa bilioni 2.6, BOQ ilihakikiwa na wahandisi wa wizara, washauri waelekezi walijiridhisha kwamba iko sawa na ujenzi ukaenda hadi bilioni 2.6 mtu yeyote akija anakataa” alihoji Waziri Mpina

Hivyo Waziri Mpina ameagiza ujenzi wa mradi huo uendelee bila kusimama na ukamilike ifikapo Aprili 20 mwaka huu kama mkataba unavyoeleeza na baada ya jengo litazinduliwa ikiwa ni sehemu ya kuleta mageuzi makubwa ya sekta ya uvuvi kupitia eneo hilo muhimu la utafiti.

“Nitaleta timu ya ukaguzi itakayofanya uhakiki wa thamani ya fedha katika ujenzi wa jengo hili, kuanzia kwenye kutangaza tenda yenyewe, thamani ya mradi, kumpata mkandarasi mwenyewe, cost estimates zilizofanywa na wizara na baadae watafanya uhakiki wa kinachoendelea kujengwa hapa na kujua thamani halisi inayotakiwa na kwanini mradi huu upitishwe hadi kusainiwa”alihoji Waziri Mpina.

Meneja wa Mradi wa Swiofish, Flora Luhanga alisema mradi huo wa ujenzi wa Jengo la Maabara ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi ulianza Juni 10, 2019 kwa gharama ya shilingi bilioni 2, 609,491,754 unajengwa na Mkandarasi Kampuni ya Petra Construction Limited na kusimamiwa na Kampuni ya YP Architect.

Luhanga alisema mradi huo unajumuisha  pia ujenzi wa uzio, ofisi ya walinzi, kuchimba kisima cha maji, ujenzi wa tenki la maji ya mvua na kujenga mnara wa maji.

Mkandarasi wa Mradi huo, Nicholaus Mlayi alisema hadi sasa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 70 na tayari ameshalipwa shilingi milioni 963 na unatarajia kukamilika mwezi Aprili.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Uvuvi, Magese Bulayi alimhakikishia Waziri Mpina kuwa maagizo yote aliyoyatoa atayasimamia kikamilifu hasa katika kuangalia thamani ya fedha ‘value for money’ katika mradi huo na kwamba hatua stahiki zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuhusika katika mchakato huo.
Share:

Viongozi wa Dini Rukwa waazimia kupunguza muda wa ibada kujihadhari na Corona

Viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Rukwa wamekubaliana kuwa kila dhehebu kulingana na imani zao kuona namna ya kupunguza muda wa kufanya ibada katika misikiti na makanisa mbalimbali ili kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19).

Wamekubaliana hayo wakati wa kikao kifupi kilichoitishwa na Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura katika kikao hicho kilicholenga kuwaelimisha viongozi hao juu ya Chanzo, usambaaji na namna ya kujikinga na ugonjwa huo ambao unaendelea kuisumbua dunia huku jukumu la kutoa elimu likifanywa na Mganga mkuu wa mkoa wa Rukwa.

Wakati akielezea namna ya kutekeleza azma hiyo Shekhe wa mkoa wa Rukwa Rashid Akilimali alisema kuwa atazungumza na mashekhe wa wilaya na Maimamu wa miskiti ya mkoa huo kupunguza muda wa ibada ili kukwepa kuwaweka watu wengi katika eneo moja kwa muda mrefu lakini pia kuwafanya waumini hao wasikose ibada hizo.

“Niungane na Askofu wa Monravian, tupunguze nyakati za ibada zetu, na kubwa iwe ni kuongoza dua na maombi kwaajili ya nchi yetu, sisi tumelipunguza hili baada ya kutokea hili, ibada ya nusu saa tumekwenda dakika kumi na tano, dakika kumi inakuwa ni mahubiri na dakika tano ni kuiombea nchi ili Mungu atuepushe na jambo hili,” alisema

Naye Mwakilishi wa Kanisa la Anglikan Mkoani Rukwa Mchungaji Mathias Gwakila alisema kuwa atajitahidi kufikisha ujumbe na elimu aliyoipata kutokana na namna alivyojifunza na kuwasisitiza waumini hao kuendelea kufanya maombi ili kuepukana na ugonjwa huo na kusisitiza kuwa ugonjwa huo ni pepo na hivyo hatunabudi kulikemea na kisha kushauri juu ya kufupisha ibada.

“Hicho ni kitu muhimu mno, ibada ziwe fupi zisiwe ndefu, kwahiyo kwa ushauri wangu kupitia madhehebu mengine yote, viongozi wote wa madhehebu wajitahidi kufupiza, kwa mfano kanisa la Anglican ibada zetu ni masaa mawili, sasa tufupishe, ibada ichukue saa moja katika vipengele vyovyote vile ambavyo wewe utaviona upunguze kipi na kipi ilimradi ibada iwe fupi watu watoke mapema,” Alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Ziwa Tanganyika Mchungaji Haruni Kikiwa alisema kuwa kupitia kikao hicho wamepata elimu ya kutosha ya namna ya kuwaelekeza wananchi ambao ni waumini wao juu ya namna ya kupambana na janga la kirusi cha Corona na kusisitiza kuwa atayafikisha kwa askofu ili kusambazwa kwa makanisa.

“Tunachukua hatua za kunawa kabla ya ibada na baada ya ibada, lakini pia hatua za kupunguza muda wa ibada ili kupunguza muda wa waumini kukaa pamoja katika msongamano lakini pia hatua za kupunguza misongamano kwa makanisa makubwa kwa maana wanaweza wakafanyia hata nje ili kupunguza msongamano watu wakae mbalimbali, haya yote nitayafikisha,” alisema.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu wakati akieleza namna ya kujikinga na ugonjwa huo alitoa msisitizo kwa viongozi hao kutumia maji tiririka pamoja na sabuni ya maji wakati wa kunawa huku akieleza madhara ya kutumia sabuni ya unga na ya kipande kuwa na tabia ya kushikwa na kila mtumiaji.

“Sabuni ya unga ambayo imechanganywa na maji ikawekwa kwenye chombo maalum kama chupa, kwahiyo mtu anaweza kuitumia hii, tunaepuka kuweka sabuni ya unga kama ilivyo kwamba mtu mmoja achukue na mwingine aje achukue na mwingine achukue, tunaepuka kuweka sabuni ya kipande kwasababu lazima mtu aje aishike akishajipaka arudishe mwengine aje aishike, kwahiyo tunasema ni sabuni ya maji na kama ni sabuni ya unga basi ichanganywe na maji,” Alisisitiza.

Wakati akifunga kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura aliwaomba viongozi hao kuzingatia makubaliano ya kikao hicho na kuongeza kuwa anaamini viongozi wa dini wasingependa waumini wao wateketee na kisha kusisitiza juu ya kupunguza muda wa ibada pamoja na mikusanyiko hasa kwa madhehebu ambayo yana waumini wengi.

“Kuna makanisa ambayo ni madogo sana au misikiti midogo watu wanajua lakini kama mikiti naona wameshajipanga wao wanasali muda mfupi lakini kuna makanisa mengine tunatumia masaa mengi, mkishaingia saa 4 mpaka saa 9 kwahiyo huo ni muda mrefu sana mnaweza mkajichanganya sana, hivyo ninaona kwamba hii kumbunguza mud ani muhimu zaidi, vile vipindi vyetu tuvipunguze zaidi tutoe elimu hasa ya kuwa na imani,” Alisistiza
Aidha, alibainisha kuwa kama serikali hawataweza kuwapangia muda wa kufanya inbada hizo huku akiweka msisitizo kuwa imani zinatofautiana na kufafanua kuwa waumini hao wanaweza hata kulala ndani ya makanisa yao kwa kuomba lakini msisitizo ni kuwa wachache ili kuepusha msongamano.


Share:

Elimu juu ya Ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona itolewe katika Maeneo ya Vijijini.

SALVATORY NTANDU
Wakazi wa mkoa wa Shinyanga wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya wananchi wanaokaidi maagizo ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Wazee na Watoto juu ya kujikinga na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya  Corona kwa kutonawa mikono kwa maji yaliyowekewa dawa za kuzuia maabukizi ya ugonjwa huo.

Hayo yalibainishwa Machi 28 na  Kisena Mihambo Mkazi wa Igwamanoni katika Halmashauri ya Ushetu mkoani humo baada ya kutembelewa na shirika lisilo la kiserikali la (REDCROSS) lililokuwa linatoa elimu kwa njia ya vipeperurishi na mabango kuhusina na kuchukua tahadhari juu ugonjwa unaosababishwa na virusi vya  Corona.

Alisema baadhi yao wamekuwa wakikaidi kutii maagizo ya serikali kwa kutonawa mikono hali ambayo inaweza kusababisha wakapatwa na maambukizi ya ugonjwa huo pindi utakapojitokesha na kuiomba serikali kupitia maafisa afya wa ngazi ya kata kuwachukulia hatua kali ili waweze kutii maagizo hayo.

“Katika Maeneo yote ya kutolea huduma za kijamii Serikali imeweka ndoo zenye Maji yaliyokwisha wekewa dawa za kuzuia maambukizi ya Ugonjwa wa Corona lakini baadhi yetu tumekuwa wagumu kunawa mikono na badala yake tunaendelea kushikana mikono pindi tunaposalimiana”,alisema Mihambo.

Zubeda Ramadhani ni Mkazi wa Ntobo katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama alisema endapo wananchi wakihimizwa kwa kupewa elimu sahihi juu ya ugonjwa wa Corona na serikali hususani maeneo ya vijijini itawezakuzuia mlipuko wa virusi vya homa ya Mapafu (Corona).

“Tunaiomba serikali iwashirikishe viongozi wetu wa ngazi za mitaa,vijiji na kata ili kusaidia kuwafikia wakazi wengi hususani wakulima ambao kwa sasa wanaendelea na shughuli za uvunaji wa mazao mashambani ili kuwakinga na maambukizi ya Ugonjwa huo”alisema Ramadhani.

Kwa upande wake Mratibu wa RED CROSS Mkoa wa Shinyanga Samwel Katamba alisema Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la kuwahudumia  watoto Duniani (UNCEF) limewapa jukumu la kusambaza vipeperushi na Mabango nchi nzima kuhusiana na kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Corona.

“Tumeweza kuzifikia Halmashauri Sita  za mkoa wa Shinyanga kwa kuweka Mabango sambamba na kugawa vipeperushi vya ujumbe kuhusiana na ugonjwa huu wa Corona ikiwa ni pamoja na kutumia magari ya Matangazo lengo ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu hii”alisema Katamba.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Ushetu Dk Nichodemas Senguo alisema mpaka sasa wameweza kutembelea kata 20 kwa kuwapatia elimu sahihi ya kujikinga na ugonjwa wa Corona huku mwitikio wa wananchi ukiwa ni mkubwa.

“Niwatake wananchi wa Ushetu waendelee kuzingatia maelekezo ya Wizara ya afya ya kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kutumia vitakasa mikono (Sanitaizer) sambamba na kuepuka kupeana mikono,pamoja na kujizuia kukaa kwenye mikusanyiko isiyokuwa na ulazima”alisema Dk Senguo.

Mwisho


Share:

Tanzia: Katibu mkuu wa CUF Khalifa Suleiman Khalifa afariki dunia

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Khalifa Suleiman Khalifa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Machi 31 2020 akipatiwa matibabu katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam. .

Mwanaye  Said Khalifa  amesema tangu Januari 2020 kwa nyakati tofauti baba yake aliugua na kulazwa katika hospitali hiyo.

Machi 16, 2019 Khalifa akichaguliwa na baraza kuu la uongozi la CUF kuwa katibu mkuu wa pili wa chama hicho akichukua nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alivuliwa uanachama.

Mwili wa Khalifa utazikwa leo katika makaburi ya Kisutu wilayani Ilala, Dar es Salaam.


Share:

Ofisi Ya Ardhi Mara Kuwezeshwa Vifaa Vya Upimaji

Na Munir Shemweta, WANMM MUSOMA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amesema wizara yake itaipatia ofisi ya ardhi mkoa wa Mara vifaa vya upimaji ili viweze kutumiwa na halmashauri za mkoa huo  kwa lengo la kuongeza kasi ya upimaji.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana wilayani Musoma mkoa wa Mara alipokwenda kukagua ofisi mpya ya ardhi ya mkoa Mara ikiwa ni jitihada za wizara ya ardhi kusogeza huduma za ardhi kwa wananchi.

Awali huduma za ardhi zilikuwa zikitolewa na ofisi za Mkamishna Wasaidizi wa Kanda ambapo kanda moja ilikuwa ikihudumia zaidi ya mikoa miwili jambo lililokuwa likiwapa usumbufu wamiliki wa ardhi kwenda umbali mrefu kuifuata huduma hiyo.

Alisema, baada ya wizara yake kuanzisha ofisi za mikao sasa wananchi watapata huduma za ardhi katika mikoa husika na migogoro ya ardhi sasa itapatiwa ufumbuzi kupitia wataalamu watakaokuwa katika mikoa hiyo.

Alibainisha kuwa, katika jitihada za kuongeza kasi ya upimaji maeneo mbalimbali ofisi za mikoa zitapatiwa vifaa vya upimaji ili visaidie halmashauri kupanga, kupima na kumilikisha ardhi na kusisitiza vifaa hivyo vitatolewa bure na aliwataka wakurugenzi wa halmashauri kushirikiana na ofisi za ardhi za mikoa.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri Mabula, Wizara yake imeamua kubeba jukumu la kutoa vifaa vya upimaji ili kuongeza kasi ya upimaji ingawa jukumu hilio linapaswa kufanywa na halmashauri kwa kuwa ndizo zenye mamlaka za upangaji miji katika maeneo.

Dkt Mabula amesikitishwa na kiasi kidogo kinachotengwa na halmashauri kwa ajili ya kazi za kupanga, kupima na kumilikisha ardhi ambapo alitolea mfano wa halmasahauri ya Musoma kutenga milioni 30 kwa kazi mbalimbali za sekta ya kiasi alichokieleza kuwa  kidogo.

‘’Milioni 10 au 15 utapima viwanja vingapi? Halmashauri hazijaipa kipaumbele sekta ya ardhi ndiyo maana malalamiko yanakuwa mengi, muongeze bajeti za upimaji’’ alisema Dkt Mabula

Hata hivyo, ameishauri halmashauri ya wilaya ya Musoma kuwatumia wataalamu wake kwa kuandika andiko ili kupatiwa mkopo usio na riba unaotokewa na wizara kwa ajili ya shughuli za umilikishaji ardhi ambapo alisema katika kipindi caha bajeti ijayo wizara inatarajia kupata bilioni saba kwa ajili ya kuzikopesha almashauri.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt Vincent Naano Anney aliipongeza wizara ya ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa uamuzi wake wa kuanzisha ofisi za mikoa na kueleza kuwa uamuzi huo utaleta  nafuu kwa wananchi wa mara katika kupata huduma za ardjhi ambapo awali iliwalazimu kusagiri hadi Simuiyu kupata huduma  hiyo.


Share:

Rais wa Uganda Yoweri Museveni atangaza amri ya kutotoka nje kwa siku 14 ili Kukabiliana na Corona

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametagaza masharti zaidi ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona wiki mbili baada ya kupiga marufuku usafiri wa Umma.

Katika hotuba yake kwa taifa iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni usiku wa Jumatatu ,Museveni amepiga marufuku usafiri wa kutumia magari binafsi na boda boda kuanzia saa nne usiku.

Mtu yeyote anayehitaji huduma za dharura za kiafya kama vile kujifungua au kufanyiwa upasuaji anatakiwa kupata idhini kutoka kwa maafisa wa serikali katika ngazi ya Wilaya kabla ya kutoka nyumbani

Wauzaji bidhaa za chakula sokoni watahitajika kuondoka maeneo yao ya biashara hadi pale serikali itakapokamilisha kushughulikia maeneo mapya ya wao kuuzia bidhaa zao .

Rais Museveni pia ameahidi msaada wa chakula kwa watu ambao hawafanyi kazi kutokana na vikwazo vya kukabiliana na covid-19 na hawana uwezo wa kujipatia bidhaa hiyo muhimu.

Museveni pia ametoa agizo kwa polisi kuwakamata wanasiasa watakaotoa misaada ya chakula kwa jamii na kushtakiwa kwa ''jaribio la mauaji ''

Uganda kufikia sasa imethibitisha kuwa na wagonjwa 33 wa corona na maafisa wanatarajia idadi hiyo kuongezeka.

Magari binafsi yatazuiwa kuingia barabarani baada ya maelekezo ya awali kutaka magari kubeba abiria watatu pekee kukiukwa, na baadhi ya watu kutumia magari binafsi kuwasafirisha wengine na kuongeza hatari ya kusambaa kwa virusi hivyo. 

-BBC


Share:

Naibu Waziri Mabula Aridhishwa Na Kasi Ya Ujenzi Hospitali Ya Rufaa Mkoa Wa Mara

Na Munir Shemweta, WANMM, MUSOMA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara iliyoko Kwangwa Musoma unaogharimu takriban Bilioni 15.082.

Dkt Mabula aliridhishwa na kasi ya mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo alipokwenda kukagua maendeleo ya ujezi wake jana wakati akiwa katika ziara ya siku moja mkoani Mara.

Alisema, ujenzi wa mradi huo ni ukombozi kwa wananchi wa Mara sambamba na mikoa na nchi jirani kwa kuwa itakuwa ikitoa huduma za kitabibu kwa wananchi wa maeneo hayo.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alibainisha kuwa, hana mashaka na Shirika la Nyumba la Taifa katika kutekeleza mradi huo kutokana na Shirika hilo kufanya vizuri kwenye miradi mbalimbali inayosimamia.

‘’Kwa sasa sina mashaka na Shirika la Nyumba la Taifa katika masuala ya ujenzi kutokana na kufanya vizuri kwenye miradi mingi ya ujenzi inayosimamia lakini kinachotakiwa hapa ni kukamilisha ujenzi kwa wakati’’ alisema Dkt Mabula

Ameitaja baadhi ya miradi ya ujenzi inayofanywa na NHC na kufanya vizuri kwenye maeneo mablimbali kuwa ni ujenzi wa ofisi kumi na saba za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),  Hospitali ya Rufaa ya Kusini iliyopo Mtwara, Ofisi ya wilaya ya Wang’ingombe na nyumba za wakuu wa wilaya za Hai na Ulanga.

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Mara Goodluck Thomas alisema Shirika lake katika kutekeleza mradi huo tayari baadhi ya kazi zimekamilishwa ikiwemo jengo la Huduma ya Mama na Mtoto, nyongeza ya ghorofa moja na kupaua, kupiga plaster nje na ndani, maandalizi ya rangi, fremu za milango pamoja na kuweka marumaru.

Kwa mujibu wa Goodluck, kazi zinazoendelea sasa ni uwekaji mifumo ya maji safi na maji taka, kazi ya umeme, uwekaji mifumo ya gesi, ufungaji madirisha ya alminiuam na ukamilishaji kazi nyingine ukiendelea na mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo umefikia asilimia 65.

Mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt Vincent Naano Anney alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi kuwa wakati ujenzi wa hospitali hiyo ukiendelea kukamilishwa kuna haja kwa mamlaka husika  kuanza kuangalia mahitaji ya Wataalamu na Vifaa vinavyohitajika kwenye vitengo mbalimbali vya hospitali hiyo na kubainisha kuwa kazi hiyo isipofanyika mapema kuna hatari ujenzi utakapokamilika hospitali hiyo ikakosa wataalamu wa kutosha kutokana na ukubwa wake.


Share:

BREAKING: Mgonjwa Mmoja wa Corona Tanzania Afariki Dunia




Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne March 31



















Share:

Monday 30 March 2020

WANANCHI WAOMBA ELIMU JUU YA UGONJWA WA CORONA ITOLEWE KATIKA MAENEO YA VIJIJINI



Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali la REDCOSS Samwel Katamba akibandika Bango lenye Ujumbe wa kuhamasisha wananchi kujikinga Ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona katika kijiji cha Ulowa Halmashauri ya Ushetu.
Baadhi ya Watumishi wa RED CROSS mkoa wa Shinyanga wakibadilishana Mawazo baada ya kumaliza kazi ya Kubandika Mabango katika Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga.
Christina Joakimu kutoka RED CROSS akitoa elimu kwa baadhi ya wakazi wa kata ya Nyamilangano katika Halmashauri ya Ushetu baada ya kuwapatia vipeperushi vyenye ujumbe wa kujikinga na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.
.Endnoela Ngeleja kutoka Shirika la RED CROSS akizungumza na wakazi wa kata ya Igwamanoni Halmashauri ya Ushetu baada ya kuwapatia Mabango yenye ujumbe wa kujikinga na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.
Afisa Ustawa wa jamii wa Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga Esta akitoa elimu kwa wakazi wa Kata ya Ushetu kuhusiana na kujikinga na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.
*
**

Na Salvatory Ntandu - Kahama
Baadhi ya Wakazi wa mkoa wa Shinyanga wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya wananchi wanaokaidi maagizo ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto juu kujikinga na ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona kwa kutonawa mikono kwa maji yaliyowekewa dawa za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.


Hayo yalibainishwa Machi 28,2020 na Kisena Mihambo Mkazi wa Igwamanoni katika Halmashauri ya Ushetu mkoani humo baada ya kutembelewa na shirika lisilo la kiserikali la (REDCROSS) lililokuwa linatoa elimu kwa njia ya vipeperurishi na mabango kuhusina na kuchukua tahadhari juu ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona.

Alisema baadhi yao wamekuwa wakikaidi kutii maagizo ya serikali kwa kutonawa mikono hali ambayo inaweza kusababisha wakapatwa na maambukizi ya ugonjwa huo pindi utakapojitokeza na kuiomba serikali kupitia maafisa afya wa ngazi ya kata kuwachukulia hatua kali ili waweze kutii maagizo hayo.

“Katika Maeneo yote ya kutolea huduma za kijamii Serikali imeweka ndoo zenye Maji yaliyokwisha wekewa dawa za kuzuia maambukizi ya Ugonjwa wa Corona lakini baadhi yetu tumekuwa wagumu kunawa mikono na badala yake tunaendelea kushikana mikono pindi tunaposalimiana”,alisema Mihambo.

Zubeda Ramadhani ni Mkazi wa Ntobo katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama alisema endapo wananchi wakihimizwa kwa kupewa elimu sahihi juu ya ugonjwa wa Corona na serikali hususani maeneo ya vijijini itaweza kuzuia mlipuko wa virusi vya homa ya Mapafu (Corona).

“Tunaiomba serikali iwashirikishe viongozi wetu wa ngazi za mitaa,vijiji na kata ili kusaidia kuwafikia wakazi wengi hususani wakulima ambao kwa sasa wanaendelea na shughuli za uvunaji wa mazao mashambani ili kuwakinga na maambukizi ya Ugonjwa huo”,alisema Ramadhani.

Kwa upande wake Mratibu wa RED CROSS Mkoa wa Shinyanga Samwel Katamba alisema Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la kuwahudumia watoto Duniani (UNCEF) limewaja jukumu la kusambaza vipeperushi na Mabango nchi nzima kuhusiana na kuchukua juu ya ugonjwa wa Corona.

“Tumeweza kuzifikia Halmashauri Sita za mkoa wa Shinyanga kwa kuweka Mabango sambamba na kugawa vipeperushi vya ujumbe kuhusiana na ugonjwa huu wa Corona ikiwa ni pamoja na kutumia magari ya Matangazo lengo ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu hii”,alisema Katamba.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Ushetu Dk Nichodemas Senguo alisema mpaka sasa wameweza kutembelea kata 20 kwa kuwapatia elimu sahihi ya kujikinga na ugonjwa wa Corona huku mwitikio wa wananchi ukiwa ni mkubwa.

“Niwatake wananchi wa Ushetu waendelee kuzingatia maelekezo ya Wizara ya afya ya kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kutumia vitakasa mikono (Sanitaizer) sambamba na kuepuka kupeana mikono,pamoja na kujizuia kukaa kwenye mikusanyiko isiyokuwa na ulazima”,alisema Dk Senguo.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger