Friday 31 December 2021

YANGA YAINYESHEA MVUA YA MAGOLI DODOMA JIJI, YAICHAPA 4-0



*************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Klabu ya Yanga imeichapa mvua ya magoli timu ya Dodoma Jiji mabao 4-0 katika mchezo wa NBC Premier league uliochezwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Yanga imecheza kandanda safi ambapo mshambuliaji wao mahiri Fiston Mayele alipachika bao la kuongoza dakika ya 42 kipindi cha kwanza .

Kipindi cha pili Yanga iliendelea kutawala mchezo kwani mpaka dakika ya 54 ya mchezo Yanga ilikuwa inatawala mchezo kwa asilimia 80% kwa 20%.

Yanga ilifanikiwakupata bao la pili kupitia kwa winga wao Jesus Muloko na baadae Dodoma Jiji kujifunga.

Aucho alifunga ubao wa magoli kwa kupachika bao tamu akipokea pasi kutoka kwa Jesus Muloko.
Share:

NAMUNGO YATAMBULISHA MAKOCHA WAPYA



Klabu ya Namungo imetangaza benchi jipya la ufundi la klabu hiyo. Imemtambulisha Hanour Janza ambaye ni raia wa Zambia kuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo akisaidiwa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye atakuwa kocha msaidizi.
Share:

RAIS SAMIA ATEUA VIONGOZI MBALIMBALI... YUMO JAKAYA KIKWETE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Miongoni wa walioteuliwa ni Rais mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor) kwa kipindi kingine cha miaka sita kuanzia Januari 12, 2022.
Share:

MREMBO AIBA MTOTO ILI KUNUSURU NDOA YAKE 'KAKOSA MTOTO MUDA MREFU'



JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia mkazi wa Buhongwa jijini humo, Rose Joshua (27) kwa tuhuma ya wizi wa mtoto wa kiume.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng’anzi amesema kuwa, tukio hilo lilitokea Desemba 19, mwaka huu, saa 4:00 usiku katika eneo la Dampo Soko la Machinga, Kata ya Buhongwa, wilayani Nyamagana.

Amesema kabla ya mtuhumiwa huyo kufanya wizi huo, alijenga ukaribu na mama wa mtoto aliyeibiwa, Stella Damas (22) ambaye ni mfanyabiashara wa eneo hilo la Dampo Soko la Machinga.

“Baada ya mazoea hayo, baadaye mtuhumiwa alimuomba mama huyo amsaidie kumbeba mtoto wakati akiendelea na shughuli zake za biashara kisha akatoweka nae kwenda kusikojulikana,” amesema.

Kamanda Ng’anzi amesema baada ya kitendo hicho, mama wa mtoto alitoa taarifa polisi ndipo ufuatiliaji wa haraka ulifanyika kwa kushirikiana na polisi Mkoa wa Kigoma na mtuhumiwa alikamatwa mkoani Kigoma na kumuokoa mtoto akiwa hai na mwenye afya njema.

“Uchunguzi wa awali umebaini mtuhumiwa alifanya uhalifu huo ili kunusuru ndoa yake baada ya kukosa mtoto kwa muda mrefu,” amesema
Share:

MWANAMKE AJIFANYA KAHABA, AWALEWESHA WANAUME KISHA KUWAIBIA



JESHI la Polisi nchini Kenya wanamshikilia mwanamama Joyce Aluta wa Mombasa kwa kosa la kuwawekea wanaume dawa za kulevya kwenye pombe na kisha kuwaibia vitu mbalimbali kama simu, saa, viatu, wallet na pesa.

Joyce mwenyeji wa eneo la Kisimani, Nyali anadaiwa wakati mwingine kujifanya kahaba na kisha akiondoka na mteja mpaka nyumbani kwake huondoka na TV, Radio, Computer na vitu vingine.

Polisi wanamshikilia Joyce na wamefanikiwa kupata baadhi ya vitu alivyowaibia wanaume hao simu, viatu na fedha taslimu na sasa anasubiri uchunguzi ukamilike ili apandishwe kizimbani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Share:

MHUDUMU WA BAA AMUUA MWENZAKE KWA CHUPA WAKIGOMBANIA CHENJI 2500 ILIYOACHWA NA MTEJA




Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia mhudumu wa baa Pendo Mwakifamba (21) kwa tuhuma za mauaji ya Hilda Mwambona (25) kwa kumkata na chupa sehemu mbalimbali eneo la tumboni.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Urlich Matei amesema tukio hilo limetokea jana wakati mtuhumiwa na marehemu wakigombea Shilingi 2,500 ambayo ni chenji iliyoachwa na mteja aliyekuwa akipata kinywaji.
Share:

MKE AMUUA MUMEWE KWA KUMCHOMA MOTO SINGIDA




Mwalimu wa Sekondari ya New Kiomboi mkoani Singida, Simon Roman (33) amefariki dunia baada ya kuchomwa moto na mkewe sababu ikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo lilitokea Desemba 27, 2021 jioni baada ya mume kurudi kutoka matembezi huku mkewe akitaka kujua kuhusu uhusiano wa mumewe na mmoja wa wanawake katika eneo hilo.


Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa Singida, Stella Mutabihirwa amemtaja mtuhumiwa wa mauaji ambaye ni fundi cherehani naye amelazwa hospitali ya mkoa wa Singida akipatiwa matibabu kutokana na majeraha ya moto aliyoyapata.

Mbali na mtuhumiwa, watoto wao Clara Anthony na Wisley Anthony wamelazwa hospitalini kwa majeraha ya moto huku Apolinary Simon (18) ambaye ni mdogo wa marehemu inadaiwa hali mbaya baada ya kuungua zaidi usoni.

Katika taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari, Kamanda Mutabihirwa amesema chanzo cha ugomvi ni mwanamke huyo kumtuhumu mumewe (marehemu) kwamba alikuwa na uhusiano na mwanamke mwingine jambo lililozua ugomvi kwa wawili hao.

“Majibizano yalipoendelea, mwanamke alikwenda kuchukua maji ya moto yaliyochemshwa kwa ajili ya kuoga akamwagia mumewe wakiwa sebuleni na kabla hajajua la kufanya alimwagia tena mafuta ya petroli kisha akawasha moto wa kiberiti,” anasema Kamanda Mutabihirwa.


Amesema moto huo ulisambaa ndani na kuunguza vitu vingi na kujeruhi wanafamilia waliokuwa ndani ya nyumba hiyo hivyo kusababisha hasara kubwa ambayo haijaweza kufahamika mara moja lakini Mwalimu huyo anajatwa kuwa aliungua vibaya mwili mzima.
Share:

WADAU WAJADILI MIKAKATI YA KAMPENI SHIRIKISHI YA KINGA DHIDI YA UVIKO 19…HALMASHAURI KUCHANJA WATU 500 KILA SIKU SHINYANGA

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkoa wa Shinyanga unatarajia kuchanja watu wapatao 1,196,153 (60%) ifikapo mwezi Juni, 2022 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Shirikishi na Harakishi wa utoaji wa chanjo awamu ya pili ambapo kila halmashauri inatakiwa ichanje watu kuanzia 500 na kuendelea kwa siku ili kuweza kufikia lengo hilo.


Hayo yamesemwa leo Desemba 31,2021 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary wakati akifungua kikao cha wadau juu ya Utekelezaji wa mpango shirikishi na harakishi kuhusu utoaji wa chanjo dhidi ya uviko-19 awamu ya pili mkoa wa Shinyanga kilichoandaliwa na Shirika la Tanzanian Men as Equal Partner in Development (TMEPiD) kwa kushirikiana na UNFPA.

Omary ameeleza kuwa moja ya mikakati ya kufanikisha mpango huo ni kushirikisha wadau wote pamoja rasilimali zilizopo kuhakikisha jamii inapata uelewa na kuongeza uhitaji wa chanjo hivyo amewaomba wadau waongeze nguvu katika maeneo ya uhamasishaji kwa kuishirikisha jamii ili kufikia lengo katika Mkoa wa Shinyanga.


Katibu Tawala huyo wa mkoa amesema kwa kuzingatia ufanisi mkubwa wa utekelezaji wa Mpango Shirikishi na Harakishi wa utoaji wa chanjo awamu ya kwanza, Serikali imeweka Mpango Shirikishi awamu ya pili wenye lengo la kuchanja asilimia 60 ya watu wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea ifikapo Juni, 2022.

“Katika utekelezaji wa Mpango Shirikishi na Harakishi wa utoaji wa chanjo awamu ya pili Mkoa wa Shinyanga unatakiwa kuchanja watu wapatao 1,196,153 (60%) ifikapo Juni, 2022. Tumelekezwa kila halmashauri ichanje watu kuanzia 500 na kuendelea kwa siku ili kuweza kufikia lengo hilo”,amesema Omary.


“Kupitia kikao hiki, naelekeza chanjo iwe kipaumbele kwa kila mmoja wetu hivyo Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi mshiriki na kusimamia zoezi hili na kuhakikisha kila mwananchi mwenye umri kuanzia miaka 18 anahamasika na kupatiwa chanjo ,wanasiasa wote katika ngazi tofauti mnaombwa kushirikiana na watoa huduma za Afya kufanya uhamasishaji na kuwashawishi wananchi kupata chanjo”,amesema.

"Ninaishukuru serikali kwa kuhakikisha chanjo hizi zinakuwepo muda wote ili wananchi wapate chanjo.  Serikali inatumia rasilimali nyingi katika masuala ya chanjo ya Uviko – 19 hivyo hatutamvumilia mtu yeyote atakayehamasisha watu wasichanje.Tutawachukulia hatua kali wale watakaokwamisha zoezi la utoaji chanjo”,amesema Omary.

“Naelekeza pia mtu yeyote atakayepotosha kuhusu chanjo ya UVIKO-19 ndani ya Wilaya za Mkoa wa Shinyanga Wakuu wa Wilaya shughulikie suala hilo na kila mwananchi kuwa sehemu ya uhamasishaji wa chanjo dhidi ya Uviko – 19”,ameongeza.

Amesisitiza kuwa tatizo la ugonjwa wa UVIKO – 19 bado lipo, na serikali inaendelea kuhakikisha wananchi wake wanapata kinga kupitia chanjo, hivyo inaendelea kuhakikisha chanjo zinapatikana na kutolewa.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Shinyanga umeendelea kupokea chanjo kwa ajili ya kujikinga na UVIKO – 19 kwa awamu tofauti tofauti na kwamba hadi kufikia tarehe 25/12/2021 Mkoa umepokea jumla ya Dozi 88491 baada ya kumaliza dozi za awamu ya kwanza.


Hata hivyo amesema katika awamu iliyopita miongoni mwa changamoto walizozibaini ni kuwepo kwa uelewa mdogo wa jamii juu umuhimu wa chanjo ya UVIKO – 19, imani potofu na uvumi usio sahihi juu ya chanjo miongoni mwa jamii na baadhi ya viongozi wa dini, siasa na serikali kutotoa ushirikiano na kupotosha jamii kuhusu chanjo ya Uviko 19.

“Kutokana na muitikio mdogo wa jamii, serikali ilikuja na mpango mkakati unaoitwa Mpango Shirikishi na Harakishi wa utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 kwa jamii “Accelerated Community Based Covid-19 Vaccination Strategy” kwa lengo la kufikia kiwango cha asilimia 100 cha utoaji wa chanjo zote zilizopokelewa ndani ya siku 20 kuanzia tarehe 01/10/2021 hadi tarehe 20/10/2021”,amefafanua.

“Kupitia mpango huo ambao ulioanza kutekelezwa rasmi tarehe 27/09/2021 Mkoa wa Shinyanga uliongeza vituo vya kutoa huduma ya chanjo hiyo kutoka vituo 18 hadi vituo 208 na ukaweka mkakati wa kumaliza chanjo tarehe 10/10/2021 ambapo ulifanikiwa kumaliza tarehe 14/10/2021.

Nipende kuwashukuru wote kwa umoja wetu kuweza kufanikisha kumaliza chanjo zote ndani ya muda uliokuwa umepangwa na Serikali, kwa pamoja tunaweza, na sasa tumeanza kutekeleza awamu ya pili”,amesema

“Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau inaendelea na utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kupambana na ugonjwa wa UVIKO – 19. Serikali iliongeza mkakati wa kutoa chanjo kwa wananchi ikiwa ni moja ya njia ya kupambana na ugonjwa huo. Naomba wananchi mjitokeze kupata chanjo kwani Kinga ni bora kuliko tiba, chanjo dhidi ya Uviko-19 ina ubora, usalama na ufanisi wa kutosha”,amesema Omary.

Mratibu Miradi wa Shirika la TMEPiD, John Maliyapamba Komba amesema wao ni wadau wa maendeleo hivyo wataendelea kushirikiana na serikali pamoja wadau mbalimbali ili kuwa na jamii yenye afya na iliyo huru dhidi ya maambukizi ya UVIKO 19.

Naye Mratibu wa Chanjo ya UVIKO 19 Mkoa wa Shinyanga Timoth Sosoma amesema lengo la mpango shirikishi na harakishi awamu ya kwanza ilikuwa ni kuongeza uelewa,kuikubali na kuongeza matumizi ya chanjo na kufikia asilimia 100 ya chanjo zilizokuwepo na sasa awamu ya pili ni kufikia asilimia 60 ya wananchi katika mkoa.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee amesema lengo la kikao hicho ni kufanya uhamasishaji kuhusu utoaji chanjo,kukumbushana wajibu wa kukabiliana na UVIKO – 19 na chanjo ya UVIKO 19 wa wajumbe kufahamu mpango mkakati wa shirikishi na harakishi wa utoaji wa chanjo kwa jamii awamu ya pili.


Nao washiriki wa kikao wameshauri Wenyeviti wa serikali za mitaa na maafisa maendeleo ya jamii, viongozi wa dini,mila,siasa na waandishi wa habari wasiachwe nyuma katika uhamasishaji  elimu ya utoaji  chanjo ya Uviko 19 na kupuuza upotoshaji wa radio za mbao na mitandao ya kijamii kuhusu chanjo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi akizungumza katika kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Kaimu Mganga Mkuu wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee akizungumza katika kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Kaimu Mganga Mkuu wa Shinyanga Dkt. Daniel Mzee akizungumza katika kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Mratibu Miradi wa Shirika la TMEPiD, John Maliyapamba Komba akizungumza katika kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Mratibu Miradi wa Shirika la TMEPiD, John Maliyapamba Komba akizungumza katika kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Mratibu wa Chanjo ya UVIKO 19 Mkoa wa Shinyanga Timoth Sosoma akizungumza katika kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Mratibu wa Chanjo ya UVIKO 19 Mkoa wa Shinyanga Timoth Sosoma akizungumza katika kikao cha wadau kwa ajili ya kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni Shirikishi ya Kinga dhidi ya UVIKO -19 na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO - 19 Mkoani Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

Thursday 30 December 2021

NAIBU WAZIRI ATOA SIKU 14 KWA KIWANDA KUREKEBISHA MFUMO WA MAJI TAKA


Kiwanda cha Hengji Investment Ltd cha Jijiji Dar es Salaam hii leo Desemba 30, 2021 kimepewa siku 14 kuhakikisha kinaweka mfumo wa kutibu maji taka kabla ya kuyatiririsha kwenye mazingira kufuatia agizo lililotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Chande (hayupo pichani)

Bomba la maji taka kutoka Kiwanda cha Hengji Investment Ltd cha Jijini Dar es Salaam, likitiririsha maji taka kwenye mto Ng’ombe kabla ya kuyatibu. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Chande (hayupo pichani) ametoa siku 14 kwa kiwanda hicho kurekebisha dosari hiyo.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Chande akizungumza na Askofu Allen Sisso wa Kanisa la Methodist Tanzania katika eneo la Boko, Dar es Salaam. Naibu Waziri Chande leo Desemba 30, 2021 amefanya ziara ya kukagua mwendelezo wa usafishaji mto huo kwa kuondoa mchanga, tope na taka ngumu katika eneo la Boko na kuagiza kasi iongezwe na kuandaa mpango wa muda mrefu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kingo za mto ili kukabiliana na mafuriko katika eneo hilo.

******************************

Na Lulu Mussa -Dar es Salaam

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Chande leo Desemba 30, 2021 amefanya ziara ya kushtukiza katika Kiwanda cha kurejeleza mifuko cha Hengji Investment Co. Ltd kilichopo eneo la Ubungo, Dar es Salaam na kushuhudia ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 kwa wamiliki wa kiwanda hicho kutiririsha maji taka ambayo hayatibiwa na bila kibali cha Mamlaka ya Bonde la Wami Ruvu kwenye Mto ng'ombe

Kufuatia ukiukwaji huo wa Sheria Naibu Waziri Chande ametoa siku 14 kwa Kiwanda hicho kuhakikisha kinaweka mfumo sahihi wa kutibu maji taka kabla ya kuyatiririsha kwenye mazingira kama Sheria inavyoelekeza na kupata kibali kutoka Mamlaka ya Bonde la Wami Ruvu.

"Wataalamu wa NEMC simamieni hili kikamilifu, nitarudi tena kukagua. Hatuwezi kuweka maisha ya wananchi rehani kwa kuruhusu ukiukwaji wa Sheria" Alisisitiza Naibu Waziri Chande.

Pia, amemuagiza Meneja wa Kiwanda cha Hengji Investment Bw. Calvin Payovela kuhakikisha wafanyakazi wa kiwanda hicho wanapatiwa vifaa vya usalama mahala pa kazi na kusisitiza kuwa hilo ni takwa la kisheria na si maamuzi ya mtu binafsi.

“Wafanyakazi hawa wapewe vifaa vya kujikinga na vumbi na afya zao kwa ujumla maana afya zao ni jambo muhimu sana, ili tuwe na kizazi endelevu yatupasa kuwa vijana wenye nguvu kazi ya kutosha” Alisisitiza Naibu Waziri Chande.

Meneja wa Kiwanda hicho Bw. Calvin Payovela amesema kuwa watahakikisha wanatekeleza maelekezo ya Serikali ndani ya muda uliotolewa.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Mhe. Hamad Chande ameuagiza uongozi wa Bonde la Wami Ruvu na Manispaa ya Kinondoni kuandaa mpango wa muda mrefu wa kunyosha Mto Nyakasanga ili kupunguza athari za mafuriko kwa wakazi wa eneo hilo. Naibu Waziri Chande ametoa rai hiyo baada ya kufanya ziara ya kukagua mwendelezo wa usafishaji mto huo kwa kuondoa mchanga, tope na taka ngumu katika eneo la Boko. Amesema Mamlaka ya Bonde la Wami Ruvu wana wajibu wa kuendelea kusimamia Sheria na kuhakikisha wananchi hawaweki makazi ya kudumu pembezoni mwa mto huo na kutoa elimu kwa umma juu ya namna bora ya kujikinga na athari zinazoweza kutokea kutokana na mto kupanuka.

"Lengo la Serikali ni kuhakiksha watu wako salama na mto unabaki salama" Chande alisisitiza. Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki Kaskazini Bi. Lilian Kapakala amesema jamii inapaswa kupanda miti rafiki kwa mazingira pembezoni mwa mito ili kupunguza kasi ya mmomonyoko wa udongo.

Nae Mhaidrolojia kutoka Mamlaka ya Bonde la Wami Ruvu Bw. Jeremia Nestory amesema Mamlaka ya Bonde kwa kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni wanaendelea na utekelezaji wa kusafisha Mto Nyakasanga kwa kuondoa tope na mchanga ili kurejesha mto katika mkondo wake.

Kufuatia uchimbaji holela wa mchanga kwenye mito na mabonde katika Mkoa wa Dar es Salaam umeandaliwa mwongozo wa usafishaji mchanga, tope na taka ngumu kwenye mito na mabonde kwa jiji la Dar es Salaam ambao utekelezaji wake umeanza.

Share:

Video : ZEE CUTE – PARTY AFTER PARTY


 VIDEO | Zee Cute – Party after Party


Share:

MWANAMKE MWINGINE AUAWA JIJINI ARUSHA


Happy Lazaro, Arusha
Mwanamke mwingine mkazi wa Njiro, jijini Arusha,Janerose Dewasi(66) ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali na anayetuhumiwa ni mfanyakazi wake wa ndani.


Tukio hili  limetokea siku chache baada ya mwanamke mwingine,Ruth  Mmasi kubainika kuuawa eneo la Njiro pia na anayetuhumiwa ni mtoto wake wa kiume Patrick Mmasi(19)


Kamanda wa  polisi mkoani Arusha,Justine Masejo amethibitisha kutokea mauwaji hayo kubainika leo saa 2:30 asubuhi na kueleza kuwa polisi  wanamsaka  mfanyakazi wa ndani ambaye anatuhumiwa baada ya kufanya mauaji hayo alitoweka.


Kamanda Masejo amesema imebainika mwanamke huyo ambaye alikuwa anaishi na mfanyakazi huyo kwenye nyumba yake eneo la block D mwili wake umepigwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso kushoto.


"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa anaishi na mfanyakazi huyo wao pekee na alimuajiri wiki moja iliyopita”amesema


Hata hivyo amesema mara baada ya mauwaji hayo mfanyakazi huyo ametoweka na anaendelea kusakwa.
Kamanda amesema jeshi la polisi linatoa wito kwa wenye nyumba kuwa makini na wafanyakazi wa ndani wanaowapa kazi kwa kujua historia zao.


Mmoja wa majirani wa nyumba hiyo,Mary Muchi alisema mfanyakazi huyo alikuwa hajulikani sana mtaani kwani ameanza kazi muda si mrefu.


“Hatujui lolote huyo kijana anatajwa Boniface alikuwa akiimsaidia huyu mama kazi zao na leo tumeshangaa kupata taarifa za kifo cha mama huyu”,amesema.


Share:

AZAM FC YAMSAINISHA IBRAHIMU AJIBU


***********

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kuinasa saini ya Ibrahimu Ajibu akitokea klabu ya Simba Sc mara baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa.

Ajibu amekuwa miongoni mwa wachezaji wakipekee waliochezea timu kubwa mbili ambazo ni mahasimu yaani Simba Sc pamoja na Yanga.

Sasa Ajibu amejiunga na Azam Fc ili kuweza kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho ambacho kimekuwa kikisuasua msimu huu.

Kupitia kwenye ukurasa wa klabu ya Simba Sc kwenye mitandao ya kijamii wamemtakia kila la heri mchezaji huyo kwa kuandika "Kwa maslahi ya pande zote mbili, uongozi wa klabu umefikia makubaliano na mchezaji Ibrahim Ajibu kusitisha mkataba wake kuanzia leo Alhamisi Desemba 30, 2021".

Share:

NHC KUANDAA KAMPENI KABAMBE YA UKUSANYAJI MADENI KWA WADAIWA SUGU

Meneja wa Huduma na Uhusiano wa NHC, Bw.Muungano Saguye akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam. Meneja wa Huduma na Uhusiano wa NHC, Bw.Muungano Saguye akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi za Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki na Masoko NHC, Bw.Elias Msese akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ofisi za Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeanza kuyafanyia mapitio madeni ya kodi na kuyahakiki ili kubainisha kila mdaiwa na mahali alipo ili mwezi Januari Shirika lianze kampeni kabambe ya ukusanyaji madeni hayo.

Ameyasema hayo leo Meneja wa Huduma na Uhusiano wa NHC, Bw.Muungano Saguye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.

Amesema hadi sasa NHC inadai malimbikizo ya kodi ya jumla ya shilingi Bilioni 26 kutoka kwa wapangaji wake, hivyo Shirika limeanza kufanyia mapitio madeni hayo na kuyahakiki.

Aidha Bw.Saguye amesema malimbikizo hayo ya Shilingi Bilioni 26, yana uwezo wa kujenga nyumba nyingine 450 ambazo zitawasaidia watanzania wengine kupata makazi kupitia Shirika hilo.

“Mpaka sasa tumeshaanza mazungumzo na baadhi ya wadaiwa zikiwemo taasisi za serikali, kufikia Januari shirika litaanza mpango wa kukusanya madeni yake yote, hayo ni maelekezo ya serikali na bodi kwa wapangaji wasio waaminifu,” amesema.

Amesema kuwa shirika limebaini wapangaji wasio halali wanaoishi kwenye nyumba kinyume na utaratibu wapatao 30 na tayari wamewachukulia hatua za kisheria kwa kuwanyang'anya upangaji na kuwapatia wanaostahili.

Pamoja hayo amesema kuwa Shirika limetenga Shilingi bilioni 8.5 kwa mwaka huu wa fedha kukarabati majengo yake 350 ambapo mpaka sasa limeshaanza ukarabati wa baadhi ya majengo katika mkoa wa Kilimanjaro na Dar es Salaam.
Share:

Wananchi Muhimbili ‘wafunguka’ Mbele Ya Waziri Gwajima


Na Atley Kuni, WAMJW, DSM.
Wananchi na wazazi wanaopata huduma kwenye kliniki ya watoto katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamemuomba Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuongezewa wataalam wa huduma ya mishipa ya ubongo.

Wakizungumza mbele ya Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima  mara baada kufanya ziara ya kutembelea  kliniki ya watoto kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, na kuzungumza na wananchi na watoa huduma kisha kupokea maoni ya wazazi aliwaokuta wakipata huduma ndani ya kitengo hicho, wazazi hao wamemuomba yafanyike maboresho kwenye eneo la huduma za vyoo kwa ajili ya kuwasitiri watoto wadogo, kuwekewa feni ili upunguza joto kwa watoto wadogo, kuongezewa mabenchi ya kukalia.

“Mhe. tunaomba kuongezwa kwa wataalam wa huduma ya mishipa ya ubongo kwani uhitaji mkubwa” alisema mmoja ya wananchi hao.

Kitengo hicho cha Mishipa ya fahamu pamoja na Ubongo, takwimu zinaonesha kinahudumia hadi Watoto 80 kwa siku, Idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na Idadi ya Mabingwa waliopo kwa sasa.

Akijibu maswali ya wananchi na wazazi hao Dkt. Gwajima alisema ameyapokea maoni na mapendekezo yaliyotolewa na kuahidi kuyafanyia kazi.

“Ndugu zangu nimewasikia, uzuri hapa tupo na Mkurugezi anawasikia pia, lakini kama haitoshi, naomba niwape namba yangu ya kunitumia ujumbe mfupi, hii sio kwa ajili ya kupiga, niandikie ujumbe, tushauri nini tuweze kuboresha, kwa kutumia wataalam wetu tutachukua maoni yenu na tutayafanyia kazi” amesema Dkt. Gwajima.

Katika hatua nyingine, Waziri amemuelekeza Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufanyie kazi maboresho ambayo wananchi waliomba kuboreshewa, sambamba nakuendelea kuchukua maoni zaidi kwenye maeneo mbalimbali ambayo yatawasilishwa na wananchi ili huduma ziweze kuboreshwa.

Akizungumza wakati wa ziara, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Prof Laurence Museru aliahidi kuyafanyia kazi maboresho hayo, ambayo wananchi waliwasilisha ili kuweza kutatuliwa sambamba na kuongeza wataalam Bingwa wa masuala ya matatizo ya watoto ya Ubongo Pamoja na mishipa ya fahamu.

“Mhe. Waziri tumeyachukua haya ambayo wananchi wamewasilisha mbele yako, lakini mkakati mwingine tulionao ni kuongeza wataalam wabobezi kwa kuwapeleka shule ili wakihitimu waweze kusaidiana na hawa waliopo na kuondoa kabisa mapungufu haya ama kuyapunguza kwa asilimia kubwa. Prof. Mseru

Awali kabla ya kuwatembelea na kuzungumza wananchi hao waliofika kwa ajili ya huduma za kitabibu, Waziri Dkt. Gwajima, alifanya kikao cha Pamoja na Uongozi wa Hospitali hiyo kwa lengo la kukumbusha wajibu na kuweka mikakati ya uboreshaji wa huduma zinazo tolewa na Hospitali hiyo ya Taifa nchini.


Share:

Wednesday 29 December 2021

TUME YA UTUMISHI WA WALIMU YATAJA MAKOSA VINARA KWA UTOVU WA NIDHAMU KWA WALIMU..YAMO MAPENZI


 Mwenyekiti wa TSC Profesa Willy Komba akiongea na waandishi wa habari Jijini Dodoma (hawapo pichani) kuhusu mwenendo wa maadili ya utumishi wa walimu nchini 

***

Na Dotto Kwilasa Malunde 1 blog, DODOMA.

TUME ya Utumishi wa Walimu Nchini (TSC) imetaja makosa  ambayo ni  vinara kwa utovu wa nidhamu yanayofanywa na walimu na kupelekea  kuchukuliwa hatua za kinidhamu katika kipindi cha mwaka 2020/21 ambapo jumla ya walimu 1795 walichukuliwa hatua kutokana na makosa hayo.


Mwenyekiti wa TSC Profesa Willy Komba amesema hayo leo Disemba 29,2021 katika Mkutano wake na waandishi wa  habari ambapo ametaja makosa hayo kuwa ni pamoja na utoro huku akibainisha kuwa jumla ya walimu 931 walishtakiwa, kugushi vyeti walimu 461, uhusiano wa mapenzi na wanafunzi walimu 211, ukaidi asilimia 6.3 na ulevi makosa 184 sawa na asilimia 4.5 ya makosa yote.


Amesema licha ya changamoto hizo bado kuna walimu waadilifu ambao wanaendelea kutekeleza majukumu yao kikamilifu na kupandisha viwango vya ufaulu katika shule za msingi na sekondari .

Kuhusu vitendo vya utovu wa nidhamu mwenyekiti huyo ametaja vitendo vya utovu wa nidhamu ambavyo vimekuwa vinara kwa sekta hiyo katika kipindi Cha mwaka Januari 2020/21 na Julai/ Desemba 2021.


"Walimu wengi bado watoro , hivyo sisi kama  TSC katika kipindi hicho tumewachukulia hatua za kinidhamu,lakini pia tunawakumbusha walimu kurudi kwenye misingi ya maadili ya utumishi wa umma, jumla ya walimu 1795 walichukuliwa hatua ikiwemo utoro ambapo walimu 931 walistakiwa, kugushi vyeti walimu 461, uhusiano wa mapenzi walimu 211, ukaidi Asilimia 6.3 na ulevi Asilimia 4.5 ya makosa yote", amesema.


Amesema katika vitendo hivyo suala la utoro wa walimu ndilo lililoongoza ambapo walimu 931 walistakiwa na kuchukuliwa hatua mbalimbali katika kipindi cha Januari/Juni sawa na asilimia 51.9 ya makosa yote huku kipindi cha Julai/Septemba mwaka huu makosa hayo yalikuwa 105 na kuchukuliwa hatua mbalimbali.


KUGUSHI VYETI

Profesa. Komba ametaja kosa ambalo linashika nafasi ya pili kuwa ni vitendo vya kugushi vyeti vinavyofanywa na baadhi ya walimu ambapo walimu 461 walistakiwa sawa na asilimia 25.7 katika kipindi cha Januari/Juni 2021 na kesi 41 katika kipindi cha Julai/Septemba 2021.


UHUSIANO WA MAPENZI  WA WALIMU NA WANAFUNZI

Amesema kosa hilo linashika nafasi ya tatu kwa utovu wa nidhamu ambapo katika kipindi cha januari/Juni jumla ya walimu 211 walistakiwa sawa na asilimia 21.8 huku katika kipindi cha Julai/Septemba kikiwa na kesi 31 sawa na asilimia 16.8 ziliripotiwa.

Pamoja na hayo ametumia nafasi hiyo kuwaasa walimu nchini kuwapa uhuru wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwaheshimu ili wasome vizuri.


Amesema ni wajibu wa Mwalimu kumlea mtoto kimwili na kiroho ikiwemo kumkinga na madhara ya ubakaji,madawa ya kulevya na mengineyo.


"Tunaposikia Mwalimu amejihusisha na mapenzi na wanafunzi anakuwa amekiuka yote hayo,wajibu mwingine wa Mwalimu ni kumlea kiroho mtoto anawajibika kumlea kwa kuwa anatumia muda mwingi shuleni kuliko nyumbani,"amesema.


VITENDO VYA UKAIDI 

Kuhusu vitendo vya ukaidi ametaja kosa hilo kushika nafasi ya nne ambapo makosa yaliyoripotiwa yalikuwa asilimia 6.3 katika kipindi cha Januari/Juni na katika kipindi cha Julai/Septemba  mwaka huu ni asilimia 1.6.


"Mwalimu anapaswa kumuelimisha mwanafunzi aheshimu watu wa rika zote kwa kuzingatia kuomba msamaha anapokosea,awe na hofu ya Mungu ndiyo maana tuna vipindi vya dini,ukaidi unayofanywa na baadhi ya walimu unawaharibu watoto wanabaki na viburi ,lazima walimu muwasimamie watoto  kupendana na kuwa na utayari wa kusaidiana,"ameeleza.


Mbali na hayo ameeleza kuwa masuala ya nidhamu wasiachiwe viongozi wa dini   peke yao bali walimu pia wana jukumu la kutunza fikra na mahusiano ya mwanafunzi ili kuwalea vizuri ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila somo lazima walimu wahakikishe linamjenga mwanafunzi kiakili, kiutendaji , kiroho na kijamii.


WALIOPEWA ADHABU

Alisema kutokana na makosa hayo zipo hatua mbalimbali ambazo zilichukuliwa dhidi ya wahusika kulingana na makosa yao asilimia 57.1  walifukuzwa kazi katika kipindi hicho cha mwaka Januari/Juni 2020/21, Julai/Septemba 46.7 huku waliopewa kalipio ni asilimia 8.5 kipindi cha Januari/Juni ilikuwa asilimia 8.5 huku Julai/Septemba ikiwa ni asilimia 7.1.


Profesa. Komba amefafanua kuwa asilimia 8.5 walishushwa daraja katika kipindi cha Januari/Juni na Julai/Septemba walioshushwa vyeo 7.6,walioshushwa mshahara walikuwa asilimia 7.7 katika kipindi cha Januari/Juni na kipindi cha Julai/Septemba 9.8, walipewa onyo katika kipindi cha Januari/Juni 7.2 na Julai/Septemba walikuwa asilimia 16.8.


"Katika kipindi hicho wapo watumishi walioshtakiwa na baada ya kutathimini mashauri yao kwa kuzingatia kanuni, Sheria na taratibu waligundua kuwa hawakuwa na hatua ambapo walikuwa asilimia 5.5 Januari/Juni na asilimia 10.5 kipindi Julai/Septemba",ameeleza.


"Adhabu zinazotolewa zinalingana na kanuni na taratibu za tume ya Utumishi  ila kwa wale ambao hawaafiki na maamuzi ya viongozi wanakata rufaa kwa mamalaka ya nidhamu  ngazi ya Wilaya, baadaye kwa TSC na mwisho kabisa wanakata rufaa kwa Rais,"amesema.


Kutokana na hayo, mwenyekiti huyo ametoa wito kwa walimu kuhakikisha wanaijua TSC ,wajibu wao ,kanuni na taratibu zinazosimamia utumishi wao ikiwa ni pamoja na  kuzingatia maadili na kuwatendea haki wanafunzi na kuzingatia maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Ummy Mwalimu ya kuwataka kuwaacha watoto wapumzike kipindi cha likizo.

Katika hatua nyingine amemshukuru na kuipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kuufanya mwaka 2021 kuwa mwaka wa baraka kwa sekta ya elimu nchini kwa kufanikisha kupandisha madaraja na kulipa mishahara mipya baada ya kupandishwa ambapo takribani walimu 146000 walipandishwa vyeo.


Amesema,tangu Rais Samia aingie  madarakani umekuwa mwaka wa neema kwa sekta ya elimu nchini tofauti na vipindi vingine vilivyopita.


"Katika kipindi cha mwaka mwaka huu wameweza kupandisha madaraja na kuanza kulipa viwango vipya vya mishahara jambo ambalo huko nyuma halikuweza kufanikiwa ,tume  inampongeza Rais Samia na Serikali yake kwa kuendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya elimu hapa nchini hususani kupitia fedha ya UVIKO-19 iliyotolewa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya ujenzi wa madarasa,"amesema.

Share:

Tuesday 28 December 2021

RAIS MWINYI ATEUA VIONGOZI WANNE


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
***
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameteua wafuatao kuwa makamishina wa Tume ya Kurekebisha Sheria.

Mosi kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said leo Desemba 28,2021 Mheshimiwa Rais amemteua Yahaya Khamis Hamad.

Pili amemteua Dkt.Sikujua Omar Hamdan, tatu amemteua Juma Msafiri Karibona.

Nne ni Salim Mohammed Abdalla na uteuzi huo umeanza leo Desemba 28,2021.
Share:

RAIS SAMIA : TUTAENDELEA KUKOPA ILI KUMALIZA MIRADI YA MAENDELEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
**
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba serikali yake itaendelea kukopa kwa lengo la kumaliza na kuikamilisha miradi yote ya maendeleo.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 28, 2021, jijini Dar es Salaam, mara baada ya kushuhudia hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) awamu ya tatu kipande cha Makutupora hadi Tabora.

Rais Samia amesema serikali itaendelea kuchukua mikopo nafuu kutoka kwa nchi wahisani, ili kukamilisha mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambao mpaka sasa gharama za ujenzi wake zimefikia shilingi trilioni 14.

Amesema tayari ameiagiza wizara ya ujenzi na uchukuzi kukamilisha utaratibu wa manunuzi ili kumpata mkandarasi wa reli ya Tabora- Isaka na Tabora- Kigoma na baadaye Kaliua-Mpanda mpaka Kalema.

“Leo hii tumekusanyika hapa kushuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha kutoka Makutupora hadi Tabora, KM 368 na mkataba huu una thamani ya Tsh trilioni 4.41 ukijumuisha na kodi ya ongezeko la thamani.

“Uwekezaji mpaka sasa hivi ni Tsh tril 14.7 tusipoendelea na ujenzi wa reli tukakamilisha fedha hizi tulizozilaza chini zitakuwa hazina maana kwa njia yoyote tutakopa sababu fedha hizi hatutazitoa kwenye tozo, wala kodi tunazokusanya ndani",amesema

Kazi ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ni kazi kubwa yenye kuhitaji uthubutu mkubwa wa Serikali na wananchi, nitumie fursa hii kuwapongeza Watanzania wote kwa mafanikio haya.
Share:

Tanzia : MWANAMUZIKI MAARUFU GENERAL DEFAO AFARIKI DUNIA



Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema  mwanamuziki mahiri wa Rhumba Le General Defao Matumona amefariki dunia akiwa nchini Cameroon Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde


Defao alizaliwa Desemba 03, 1958 katika jiji la Kinshasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Baada ya kuzaliwa akapewa majina ya Mutomona Defao Lulendo.

Ni mwanamuziki mwenye talanta za kutunga na kuimba kwa sauti nyembamba na nyororo. Defao alianza kujishughulisha na muziki mwaka 1976, akiwa katika bendi ya Orchestra Suka Movema. Baadaye akaenda kujiunga katika bendi ya Fogo Stars.

Mwaka 1978 Defao akaenda kupiga muziki katika bendi ya Korotoro huko Somo, Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).

Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki waliounda bendi mpya ya Grand Zaiko Wawa mwaka 1981, ikiongozwa na mpiga gitaa mashuhuri Pepe Felix Manuaku.

Katika kile kilichoitwa mbinu za kujitafutia maisha, Defao aliungana na mwanamuziki Ben Nyamabo kuunda kikosi kipya cha Choc Stars.

Bendi hiyo ya Choc Stars na Orchestra Shakara Gagna Gagna, zilikuwa chini ya uongozi wa Jeanpy Wable Gypson, zilimfanya General Defao kuwa maarufu kwa mara kwanza kitaifa.

Akiwa na wanamuziki akina Ben Nyamabo, Debaba, Carlito, Bozi Boziana na Djuna Djunana, bendi ya Choc Stars ikajizolea umaarufu mkubwa kupitia tungo zao.Uimbaji na uwajibikaji jukwaani wa General Defao aliweza kuonesha kuwa kipaji chake siyo cha kubahatisha.

Defao Mutomona kwa kawaida alicheza sambamba na wanenguaji wake, ambapo huwa kivutio kikubwa cha wapenzi na mashabiki wake akicheza mitindo mbalimbali ukiwemo ule wa ‘Ndombolo’ pasipo kuchoka.

Mutomona ilipofika mwishoni mwa mwaka 1990, aliiacha bendi hiyo ya Choc Stars, akiwa na madhumuni ya kuunda bendi yake.Dhamira yake alitimia baada ya kuunda bendi yake iliyopewa jina la Big Stars.

Katika bendi hiyo alipiga muziki kwa kushirikiana na mwimbaji mwingine Djo Poster, aliyetokea katika bendi ya Grand Zaiko.

Defao aliomuongeza katika safu ya wanamuziki mpiga solo chipukizi Jagger Bokoko, ambaye alitokea kuwa kipenzi chake kikubwa.

Bendi ya Big Stars ilikuwa na wanamuziki wengi wenye uwezo mkubwa wa kutengeneza muziki.

Kulikuwa na waimbaji akina Djo Djo Bayenge, Debleu Kinanga na Adoli Bamweniko.Kwa upande wa wapiga magitaa, kulikuwa na Mogus aliyekuwa akilicharaza gitaa la solo, gita la besi likiungurumishwa na Guy wa Nzambi.

Tumba zilikuwa zikidundwa na Richa Cogna Cogna. Mbofya kinanda alikuwa ni Sedjo Kavanda.

Katika kipindi cha miaka mitano ya bendi ya Big Stars, Defao alionesha ubunifu uliomletea mafanikio makubwa baada ya kufyatua album zisizopungua 17. Kati ya hizo, sita ziliingia katika soko la Ulaya mwaka 1995.

Mifarakano katika sehemu za kazi huwa hazikosi. Big Stars iliteteleka kwa kipindi kifupi mara baada ya kuondoka Djo Djo Bayenge na kumuacha Defao akiwa kiongozi wa bendi hiyo.

Defao akiwa na wanamuziki wake wa Big Stars, walikarabati upya bendi yao na kuweza kutengeneza kikosi kipya chenye wanamuziki mahiri. Walimuongeza Roxy Tshimpaka.

Roxy kabla ya kujiunga na Big Stras alikuwa katika bendi ya Choc Stars.

 Aidha alimpata mwimbaji mpya Azanga.Siku zilivyokuwa zikiiendela, mpigaji gitaa la solo Jagger Bokoko akawa kuwa kipenzi kikubwa cha Defao.

Umaarufu wa General Defao ulizagaa maeneo mengi Afrika Mashariki na Kati kwenye miaka 1990.

Wapenzi na mashabiki wake waliulinganisha umaarufu wake na ule wa wanamuziki akina Papa Wemba, Koffi Olomide, Bozi Boziana na Kester Emeneya.

Hapana ubishi kwamba Defao Mutomona ni mwanamuziki aliye na umaarufu mkubwa miongoni mwa wanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mpenzi msomaji utakubaliana nami iwapo utasikiliza nyimbo za Georgina, Fammilie Kikuta, Nadine, Bana Kongo, Oniva na Filie.

Nyimbo hizo ziko katika kiwango cha juu na zimepigwa katika mitindo miwili ya rumba na sebene mold.

Kufuatia uangalizi wa uzalishaji wa kazi toka kwa meneja wake kuwa mbovu, Defao alilazimika kubadili maprodyuza na kampuni za kurekodia.

Wakati mwingine alikuwa akitoka na matoleo ya kazi zake zilezile kwa lebo tofauti.

Defao alilivunja kundi zima la Big Stars mwaka 2000 wakiwa katika jiji la Kinshasa.

Yeye akaamua kwenda ‘kutanua’ katika jiji la Paris nchini Ufaransa wakati wa kipindi cha joto.

Lakini akiwa katika jiji hilo, alirekodi album ya Nessy de London, akiwashirikisha wanamuziki nyota waishio katika jiji hilo la Paris.

Wanamuziki hao walikuwa akina Nyboma Mwandido, Luciana de Mingongo, Wuta Mayi, Ballou Canta na Deesse Mukangi, walioshirikiana na Defao kufanya onesho kubwa lililo wavutia watu wengi.

Defao kwa kuwatumia waimbaji hao waalikwa, walipelekea album yake ya De London kupanda chati zaidi.

Aliachia album nyingine nyingi zikiwa na nyimbo za Mandova, Ya Gege, Copinnage, Sam Samita, Salanoki Guerre De1, Animation na Nessy of London.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Defao baadae akawa kimya katika anga ya muziki.

Hali hiyo yasemekana kuwa ilitokana na sintofahamu ya kisiasa nchini mwake iliyopelekea kufungiwa kupiga muziki huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa uongozi wa Rais Lauler Kabila.

Defao alifika nchi za Afrika ya Mashariki ikiwemo Tanzania.

Katika ziara yake ya  nchini Tanzania iligubikwa na matatizo lukuki mwaka 2000, uliokuwa mwaka mpya wa Millenium.Baada ya kumaliza kufanya maonyesho kadhaa, Defao alizidiwa akili na ‘Mapromota’ waliomleta, matokeo yake alifikia hadi kukosa pesa ya kujikimu pamoja na kulipia Visa yake kuwa mushkeri.

Nguli huyo ‘alifulia’ hata nauli ya kumrejesha kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hakuwa nayo.

Bahati njema ilikuwa upande wake kwa kuwa alifanikiwa kurejea kwao baada ya kupewa ‘lift’ katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), aliyokuwa ikizindua safari zake kati ya Dar es Salaam na Lubumbashi nchini DRC.

“Kimya kingi kina mshindo mkuu” usemi huu ulijionesha wazi kwa gwiji hilo lililosubiriwa na wapenzi kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2006, ndipo alipotoka na album yake mpya yenye Lebo ya Nzombo le Soi.

Baada ya miaka minne mingine alifyatua CD yake yenye Lebo ya Pur Encore mwaka 2010.Mwaka 2012 Defao kwa bahati nzuri alirudi ulingoni akiwa na album ya The Undertaker.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger