Saturday 19 December 2015

Wanafunzi 97% Wachaguliwa Kujiunga Kidato cha Kwanza 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Asilimia 97 Wachaguliwa Kidato cha Kwanza
Jumla ya wanafunzi 503,914 kati ya wanafunzi 518,034 waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwakani, sawa na asilimia 97.3 wamepata nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za serikali, huku wengine 12,847 wamekosa nafasi za kujiunga na masomo kuanzia mwezi Januari mwakani.Aidha Sh. bilioni 131 zimetengwa na serikali kwa ajili ya shughuli za uendeshaji shule, chakula kwa wanafunzi wa bweni na fidia ya ada ya mitihadi kwa kipindi cha kuanzia mwezi Desemba mwaka huu hadi Juni mwaka 2016.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Selemani Jafo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kati ya wanafunzi hao waliochaguliwa, wasichana ni 255,843 sawa na asilimia 99.2 na wavulana ni 248,076 sawa na asilimia 97.7Alisema idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza imeongezeka kwa asilimia 0.7 ikilinganishwa na asilimia 97.23 ya wanafunzi waliochaguliwa awamu ya kwanza kuingia kidato cha kwanza mwaka 2015.
Aidha wanafunzi 610 sawa na asilimia 61.2 ya wanafunzi 997 wenye ulemavu waliofanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi wamefaulu na wote wamechaguliwa kujiunga na shule za sekondari.Kuhusu mikoa iliyoshindwa kupata nafasi kwa wanafunzi wote waliofaulu, Mhe.Jafo alisema Wanafunzi 12,847 kati ya Wanafunzi 518,031 waliofaulu mtihani wa darasa la saba uliofanyika Septemba 9 mwaka huu, wameshindwa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa madarasa katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Mtwara.
Naibu Waziri alieleza kuwa katika mkoa wa Dar es salaam idadi ya wanafunzi waliokosa fursa ya kuanza masomo mwakani ni wanafunzi 12,225 wa jiji la Dar es Salaam, ambapo wilaya ya Temeke ni wanafunzi 4,707, Ilala wanafunzi 2,365 na Kinondoni wanafunzi 3,183.Kwa upande wa mkoa wa Dodoma; Halmashauri ya Dodoma mjini wanafunzi 131 na Kongwa wanafunzi 52, na kwa mkoa wa Mtwara katika halmashauri ya Masasi ni wanafunzi 200 ambao wamekosa nafasi.
“Pia tunaziagiza Halmashauri, wakuu wa shule na walimu kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi watakao anza masomo mwezi Januari,” alisema Jafo.Kuhusu gharama za kuendesha shule, alisema serikali imetenga Sh. bilioni 18.77 kwa kila mwezi kuanzia Desemba mwaka huu hadi Juni mwaka 2016 kwa ajili ya mahitaji ya shule kiasi ambacho ni Sh. bilioni 131 kwa miezi saba.
Jafo alisisitiza kuwa, fedha hizo zitakuwa zinafuatiliwa kama zinafika kwa wakati na matumizi yake na watakaozifanyia ubadhilifu watawajibishwa.Pia alitilia mkazi agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Magufuli kuhakikisha wanafunzi wanasoma bure kuanzia shule za awali hadi kidato cha nne kwa kuwataka wazazi kujiandaa na sare za shule pekee.
“Nawasisitizia wakuu wa shule na watendaji wengine kuhakikisha elimu ni bure, ole wake Mkuu wa shule au Mtendaji wa Halmashauri atakayepokea mchango wa mzazi,” alisema Jafo.Jumla ya wanafunzi 775,273 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza darasa la saba kuanzia tarehe 9 hadi 10 septemba 2015 ambapo watahiniwa 763,606 sawa na asilimia 98.5 ya waliosajiliwa walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2015.
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 19/12/2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Share:

Friday 18 December 2015

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO AWAMU YA 7 2015/2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
HESLB LOGO
HESLB officially welcomes Local Undergraduate Loan Applicants for Academic Year 2015/2016 to view their Loan Allocation status in (Lots 1, 2, 3, 4, 5,6 & 7 - NEW). To view your status click the link Applicant's Loan Status.
Share:

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DECEMBER 18 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY






Share:

Thursday 17 December 2015

magazeti ya leo alhamisi dec 17 2015

Share:

Sunday 13 December 2015

MAGAZETINI LEO JUMAPILI DEC 13 2015

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger