Monday 31 July 2023

NEMC YAPIGA KAMBI MBEYA KUWAWAPA SOMO WANANCHI


Na Mwandishi Wetu,MBEYA

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira(NEMC) limeanzisha mfumo wa kielektroniki wa usajili wa miradi ili kuwarahisishia wawekezaji kufanyiwa tathmini ya athari ya mazingira(TAM).

Kutokana na hatua hiyo, limewataka wawekezaji wa miradi kutekeleza sheria ya mazingira inayotaka miradi kupata cheti cha TAM kabla ya kuanza utekelezaji wake.

Ofisa Elimu ya Jamii wa NEMC, Suzan Chawe akizungumza kwenye banda la Baraza hilo katika maonesho ya nanenane viwanja vya John Mwakangale jijini hapa, alisema baraza limerahisisha mchakato wa TAM kwa kuanzisha usajili wa miradi

kwa mfumo wa kielektroniki na kusogeza huduma katika ofisi za Kanda zinazopatikana nchini.

"Tunawakaribisha wenye sifa za kuwa washauri elekezi wa Mazingira kujisajili na kupata cheti cha utendaji kwa ajili ya kufanya TAM na ukaguzi wa mazingira,"alisema.

Meneja wa NEMC Kanda ya nyanda za juu kusini, Josia Mlunya, alisema katika banda hilo shughuli zinazofanyika ni kusajili wataalamu elekezi wa mazingira, usajili wa miradi kwa ajili ya cheti cha TAM.


"Pia tunatoa elimu ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira, pamoja na kupokea malalamiko na maoni yanayohusu mazingira na kuyashughulikia,"alisema.
Share:

COSTECH YAAGIZWA KUWEKA MFUMO KURATIBU TAFITI




Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo,akizungumza wakati wa Kikao kazi cha kujadili usimamizi ya utafiti na maendeleo nchini kilichofanyika leo Julai 31,2023 Mjini Morogoro.

Na.Mwandishi Wetu-MOROGORO

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ameitaka Tume ya ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuwa na mfumo mathubuti wa kuratibu tafiti utakaosomana na Taasisi nyingine zinazofanya tafiti.

Agizo hilo Julai 31, 2023 mjini Morogoro katika Kikao kazi cha kujadili usimamizi ya utafiti na maendeleo nchini ambapoa amesema ili kutekeleza hilo kwa ufanisi wizara itaunda kamati ndogo shirikishi ambayo itapitia maoni ya kikao kazi na kuangalia sheria mbalimbali za taasisi zinazohusu masuala ya tafiti ili kutoa mapendekezo.

"Utafiti ni muhimu kwa maendeleo ni vyema ukaratibiwa vizuri ili kupunguza milolongo ya kupatika kwa vibali vya kufanya utafiti na kuwezesha upatikanaji wa matokeo kwa urahisi" amesisitiza Prof. Nombo.

Katibu Mkuu huyo ameongezea kuwa no muhimu kwa taasisi mabimbli kujikita katika kufanya tafiti za pamoja ilinkuleta tija, lakini pia kuhakikisha zinatenga fedha kwa ajili ya tafiti

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Prof. Maulilo Kipanyulu amesema kuwa kikao kazi hicho kinafanyika kwa kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ina jukumu la kutunga na kusimamia utekelezaji wa Sheria na Miongozi ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Utafiti

Naye Mshiriki wa Kikao hicho Makumu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Prof. Lughano Kusiluka ameiponeza wizara kwa kikao hicho na kutaka kifanyike mara kwa mara ili kujadili vipaumbele, utekelezaji na matokeo ya tafiti katika maendeleo
Share:

AUAWA KWA KUKATWA KICHWA AKICHUMA MBOGA



MKAZI wa Kijiji cha Mgongola A Kata ya Kwamgwe wilayani Handeni mkoani Tanga, ameuawa kwa kukatwa kichwa na watu wasiojulikana wakati akichuma mboga shambani.

Akizungumzia tukio hilo lililotokea juzi Julai 29, 2023 kijijini hapo Diwani wa Kwamgwe, Sharifa Abebe amesema mwanamke huyo wa kabila la Kimang’ati alikuwa akichuma mboga ndipo alipouawa kwa kukatwa shingo huku akiwa na mtoto mdogo wa mwezi mmoja na nusu mgongoni.

“Kichwa mpaka sasa hakijajulikana kilipo lakini juhudi za polisi zinaendelea. Ukweli ni kwamba hatujajua nini kilisababisha mauaji haya kwa kweli,” ameeleza Abebe.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya, Albert Msando aliyefika eneo la tukio kwa pikipiki, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kueleza kuwa hadi sasa watu watano wanashikiliwa na Jeshi la Polisi huku juhudi ya kutafuta kichwa cha marehemu zikiendelea.

“Mpaka sasa hivi chanzo cha mauaji hayo hatujajua ni nini na Jeshi la Polisi tangu juzi linaendelea na upelelezi,” amesema.

Alisema kwa ujumla hali ya usalama katika kijiji hicho ni nzuri japokuwa juzi wanakijiji hao walikusanyika wakiwa na silaha za jadi na kufanya vurugu hali ambayo hata hivyo ilitulizwa.

Msando alisema pia watuhumiwa hao watano wanaendelea kuhojiwa na polisi ili kuona kama kuna lolote linaloweza kubainika kuhusu mauaji hayo.

Baba mkwe wa marehemu, Dingo Shauri amesema hata wao hawafahamu chanzo cha tukio hilo.

“Taratibu za mazishi bado tunasubiria askari waseme na tumepanga wakituruhusu tutamzika hapa hapa Kwamgwe hata kama hatujapata kichwa, mwili tunao tutazika tu tutafanyaje sasa,” ameeleza.

Mkazi wa eneo hilo Malick Mohamed aliomba serikali kuingilia kati na kushughulikia mauaji hayo kutokana na wakazi wa eneo hilo kuingiwa na hofu.

“Hali ya amani ni tete. Tumeishi na hawa wafugaji Wamang’ati kwa takribani miaka 10 sasa, pametokea matukio mbalimbali na inapotokea tukio lolote hata kama ni mtu kakwazwa shamba lake limelishiwa akamchapa viboko hawa wenzetu wana tabia ya kulipiza visasi,” amesema Mohamed.
Amesema kutokana na hali hiyo eneo hilo limekuwa na matukio ya mauaji zaidi ya moja.


Share:

13 WAHOFIWA KUFARIKI BAADA YA MITUMBWI MIWILI KUZAMA ZIWA VIKTORIA


Watu 13 wanahofiwa kufariki dunia huku wengine 14 wakiokolewa baada ya mitumbwi miwili kuzama ndani ya Ziwa Victoria wakati wakitoka kusali ibada ya Jumapili Kijiji cha Ichigondo Wilaya ya Bunda mkoani Mara.
Akizungumza kwa simu na Mwananchi leo Jumatatu Julai 31, 2023, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano amesema tukio hilo lilitokea jana saa 12:30 jioni na tayari mwili wa mtoto anayekadiriwa kuwa na mwaka mmoja umeopolewa.

“Hapa Kijiji cha Igundu kuna kama ras sasa watu walikuwa wakitoka kusali katika kanisa la KTMK ndipo mtumbwi mmoja ukapigwa na dhoruba na kuanza kuzama, ukaja mtumbwi wa pili kwaajili ya kuokoa nao ukapigwa na dhoruba mitumbwi yote miwili ikazama,"amesema Dk Naano.

CHANZO-MWANANCHI.

Share:

AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA KWA KUMUUA MWANAFUNZI UDOM




MAHAKAMA kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemhukumu Idris Mwakabola kunyongwa hadi kufa, baada ya kupatikana na hatia ya kumnyonga Happiness Mbonde, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Mwakabola alifikia uamuzi wa kumuua mpenzi wake huyo kwa kuhisi ana uhusiano na mwanamume mwingine. Kabla ya kufanya kitendo hicho, alimwingilia kimwili mpenzi wake huyo bila ridhaa yake kisha kumpa kinywaji chenye kilevi na hatimaye kumnyonga.

Akisoma hukumu hiyo juzi, Jaji Ephery Kisanya, alisema maelezo yanaonyesha kuwa Mwakabola alimuua Happiness baada ya kupata hasira na kwamba kifungu cha 201 cha Kanuni ya Adhabu itatumika, lakini pia maelezo hayo lazima yathibitishe kuwa mauaji yalifanyika wakati mshtakiwa alipokuwa na hasira.

"Lakini lazima mshtakiwa ahojiwe wakati ule ule baada tu ya tukio. Kwa shauri hili, Happiness hakuuawa pale pale baada ya mshtakiwa kuona amepigiwa simu na mpenzi wake wa zamani. hakuna kinachoshawishi kwamba aliuawa kwa hasira, bali inaonyesha Idris (Mwakibola) alidhamiria,” alisema Jaji Kisanya.


Share:

WAZAZI NA WALEZI WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WENYE ULEMAVU



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kushoto) akishiriki chakula cha pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwanga Viziwi Mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro Mhe. Abdallah Mwaipaya (aliyesimama) akifafanua jambo wakati za ziara ya Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga alipowasili katika Wilaya hiyo kuzungumza na  wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwanga Viziwi Mkoani Kilimanjaro.


Na Devotha Songorwa, Kilimanjaro .


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amewataka wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu kutowaficha watoto wao ndani akisema kufanya hivyo ni kuwanyima haki zao za msingi.

Mhe. Ummy ametoa kauli hiyo katika ziara yake alipotembelea wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwanga Viziwi, Wilaya ya Same pamoja na Wilaya ya Mwanga  Mkoani  Kilimanjaro  kwa lengo la kufuatilia  utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Amesema kuwa watu wenye ulemavu wana haki sawa na watu wengine hivyo inapaswa kushirikishwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi pamoja na fursa ili waweze kujikwamua kiuchumi na kutoa mchango wao katika maendeleo ya Taifa.

“Watu wenye ulemavu msivunjike moyo, watoto mlioko hapa  viziwi msikate tamaa mna uwezo wa kusoma mkafika mbali, mna uwezo wa kufanya shughuli yoyote  kwa sababu Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yupo kwa ajili yenu amewezesha elimu bure  kwahiyo tutumie nafasi hiyo,”Amesema Mhe. Ummy

Pia amewahimiza watu wenye ulemavu kutojinyanyapaa na kujiona hawafai akisema wana haki sawa na watu wengine hivyo jamii inatakiwa kuwatambua na kuwapa kipaumbele katika huduma mbalimbali na hata fursa za ajira .

Aidha Mhe. Ummy ametoa mitungi ya gesi ya kupikia 93 kwa watu wenye ulemavu Wilaya ya Mwanga  kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia ikiwa ni hatua ya uhifadhi wa mazingira na kuepuka madhara ya kiafya yatokanayo na matumizi ya kuni.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro Mhe. Abdallah Mwaipaya ameishukuru Serikali kwa kuanzisha shule za watu wenye ulemavu kwani hutoa fursa kwao kupata ujuzi na stadi za maisha ambazo husaidia kundi hilo kujitambua na kujua nafasi yao katika jamii.

“Wilaya yetu ni moja ya Wilaya chache zenye shule hizi ambazo zinawajenga katika stadi za maisha kulingana na hali ya ulemavu wao hatimaye kukabiliana na hali waliyo nayo kwa sababu kuwa mtu mwenye ulemavu haina maana hauwezi hivyo uwepo wa shule hizi ni hatua muhimu sana,”Ameeleza Mhe. Mwaipaya.

Aidha Akitoa taarifa ya Watu Wenye Ulemavu Katibu wa Shirikisho la Vya vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro Bwa. Jeremia Shayo amebainisha kwamba wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa viungo bandia, wakalimani wa lugha ya alama katika baadhi ya Taasisi hali ambayo hukwamisha mawasiliano pindi wanapofika mahali husika kupata huduma.


Share:

MKE WANGU KABADILIKA SANA BAADA YA KUJIFUNGUA


Ndoa yeyote bila ya kuwa na mapenzi ya kweli hukumbwa na misukusuko ya kila aina wakati wowote ule, ni jukumu la kila muhusika katika ndoa kuhakikisha kwamba mapenzi yanazidi kudumu.

Tuliishi na mke wangu kwa amani na upendo, kwa hakika tuliaminiana sana hadi mke wangu alipopata mtoto wa pili katika ndoa yetu na hapo alianza kuwa mkali bila sababu na kushindwa kumuelewa.

Hatukuelewana katika jambo lolote ambalo tulizungumza, jambo dogo tu alikuwa ni mwepesi wa kukasirika, kamwe sikumuelewa kwani pendo ulikuwa umeisha sana.

Kila mara tuligombana kwa ajili ya mambo madogo madogo tu, sio kwamba nilikuwa sitimizi majukumu yangu kama kichwa cha familia, bali kwa sababu ya hasira zake tu.

Ilikuwa ni mwiko kwa jamii yetu mwanaume kuingia jikoni kupika lakini ilinibidi nifanye hivyo maana yeye alisusa, ilifikia hatua nikafikiria nimfukuze halafu nioe mwanamke mwingine!

Nilipokuwa tayari nimekata tamaa ndipo rafiki yangu Odipo aliponiambia kwamba angenisaidia kubadilisha tabia ya mke wangu na hapo akanielekeza kwa mtaalamu wa miti shamba ambaye anaitwa African Doctors.

African Doctors alinihudumia vilivyo na kunipa dawa fulani za miti shamba ambazo alinishauri niziweke chini ya mto ambao tunautumia mimi na mke wangu.

Walinipa hakikisho kwamba mke wangu angebadi tabia yake mara moja na kuwa mtu mzuri, niliporejea nyumbani nilifuata maagizo yote ya African Doctors, huku nikiwa na imani kuwa mambo yangebadilika kwenye ndoa yetu.

Baada ya siku tatu mke wangu alianza kubadilika, chakula kilipokuwa tayari aliniita majina ya kimapenzi na kunikaribisha nile kama mume wake, ama kwa hakika mapenzi yalikuwa yasharudi tena kwenye ndoa yetu.

Kila nilipotoka kazini alinikaribisha kwa moyo wa ukarimu na hata kunijali, kila jambo alilotaka kufanya pale nyumbani aliomba ushauri wangu kinyume na hapo awali ambapo alijichukulia maamuzi mwenyewe. 

Pia African Doctors ana uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali kama vile magonjwa ya kisukari, kisonono na kaswende kwa muda wa siku tatu tu. Anasuluhisha migogoro ya mashamba na pia kukuwezesha kushinda kesi kotini ili kupata haki kwa wakati wowote ule.

Wasiliana na African Doctors kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.

 

Share:

Sunday 30 July 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 31,2023































Share:

GGML YATOA MSAADA WA MADAWATI 8,823 MKOANI GEITA


Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong (kulia) akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Geita, Martin Shigela baadhi ya madawati hayo. Kushoto kwa mkuu huyo wa mkoa ni Mkuu wa wilaya ya Geita, Cornel Maghembe.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong, Mkuu wa mkoa wa Geita, Martin Shigela baadhi ya viongozi wengine wa mkoa huo, wakiwa wamekaa katika madawati hayo pamoja na wanafunzi mkoa huo kama ishara ya furaha ya makabidhiano ya madawati kwa shule mbalimbali za Geita.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano ya madawati kwa shule mbalimbali za Geita.

NA MWANDISHI WETU

KATIKA kutimiza dhamira ya kuimarisha sekta ya elimu na kuwezesha mazingira ya utoaji elimu nchini kuwa ya usawa, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa msaada wa madawati 8,823 kwa shule mbalimbali za Geita ili kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia kwa wanafunzi wa mkoa huo.

 

Katika hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika juzi Mjini Geita kwa ushirikiano na mamlaka za serikali za mitaa kupitia mpango wa GGML wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella, aliishukuru kampuni hiyo kwa kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka.

 

Alisema kadiri shule nyingi zinavyoendelea kujengwa ndivyo hitaji la madawati linavyozidi kuonekana jambo ambalo GGML inajitahidi kutatua changamoto hiyo.

 

Shigella alipongeza GGML kwa kuwa na mipango ya muda mrefu ya kuinua sekta ya elimu mkoani Geita na Tanzania nzima kwa ujumla.

 

"Ni furaha yangu kwamba tangu GGML ianze shughuli za uchimbaji hapa mkoani Geita, imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Serikali kutekeleza miradi kadhaa ya elimu, hasa ujenzi wa madarasa na shule".

 

Mkuu huyo wa mkoa alikiri kuwepo kwa uhaba wa madawati katika shule mbalimbali hivyo kuwaomba wadau wengine mkoani humo kufuata nyayo za GGML katika kuboresha mazingira ya kujisomea kwa wanafunzi.

 

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong, alisema ni muhimu kuboresha mazingira ya utoaji elimu nchini ili kufikia lengo namba 4 la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.

 

"Kutoa elimu bora kwa wote ni msingi wa kujenga dunia yenye amani na ustawi. Elimu huwapa watu maarifa na ujuzi wanaohitaji ili kuwa na afya njema, kupata ajira. GGML inafurahi kuboresha maisha ya Watanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu," alisema.

 

Akielezea malengo ya GGML katika kuboresha maisha ya Watanzania hususani kupitia uboreshaji wa sekta ya elimu, Strong alieleza kuwa tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo mwaka wa 2000, GGML imeendelea kuwekeza katika nyanja mbalimbali zinazoboresha maisha ya jamii nzima ya Geita na Tanzania kwa ujumla.

 

Alisema GGML imewekeza kwa kuzingatia masuala muhimu kama vile afya, elimu, maji, barabara na miradi ya kuzalisha kipato cha kaya na kukuza uchumi wa Taifa.

 

"GGML imewekeza katika utekelezaji wa miradi endelevu ambayo inainufaisha jamii inayouzunguka mgodi. Kwa hiyo mchango huu wa madawati unadhihirisha jukumu la GGML kama mwananchi anayehitaji elimu bora kubadilisha maisha yake," alisema na kuongeza;

 

"Juhudi za GGML kujitolea kutekeleza miradi mbalimbali zinaendelea kuacha alama isiyofutika na kusaidia kuboresha maisha ya jamii kupitia uwepo wa kampuni hii mkoani Geita."


Share:

ORYX GAS YATOA MITUNGI 500, MAJIKO YAKE KWA MAMA LISHE ILEMELA

Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba akitoa elimu ya matumizi salama ya mtungi wa gesi ya Oryx kabla ya mitungi hiyo kukabidhiwa kwa wanawake wajasiriamali wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

***************

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Araman Benoite, amesema kaampuni hiyo imegawa bure mitungi ya gesi 500 pamoja na majiko yake kwa mamalishe wilayani Ilemela, kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Oryx Gas imegawa mitungi na majiko hayo jana kwa wanawake wajasiriamali wa Mama Lishe waliopo katika Kata 19 za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza, kuwaongezea nguvu katika shughuli zao na kuzifanya kisasa.

Akizungumza mbele ya viongozi wa Wilaya ya Ilemela wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angelina Mabulla, Benoite amesema kuwa wameendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kulinda na kutunza mazingira kwa kuhamasisha nishati safi ya kupikia.

“Katika mwendelezo huo wa kuhimiza matumizi ya nishati safi na salama kwa kupikia, Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Limited imekuwa mstari wa mbele kufikia azma hiyo, leo (jana) kampuni yetu imevitupia macho vikundi vya wafanyabiashara wa vyakula (Mama Lishe) wilayani Ilemela kwa kuwakabidhi bure mitungi 500 ikiwa na gesi yake.

“Utoaji huu wa mitungi ya Oryx umefanikiwa kwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa Waziri wa Dk. Mabula. Malengo ya kampuni ni kuona mabadiliko katika matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia kwa jamii zote za Watanzania,” amesema.

Aliongeza kuwa hatua hiyo inaendana na mpango wa serikali wa miaka 10 wa matumizi salama ya nishati safi ya kupikia huku akifafanua wanafahamu kundi la Mama Lishe kila siku linahudumia chakula kwa wananchi lakini wengi wao wameathirika kwa namna mbalimbali kutokana na matumizi ya kuni na mkaa.

“Mwanza na mikoa ya Kanda ya ziwa imeharibiwa kwa kiasi kikubwa na ukataji miti kwa matumizi ya kuqndaa chakula, hivyo juhudi kubwa inahitajika kulinda afya na kuokoa mazingira ya ukanda huu na maeneo mengine nchini,” Amesema.

Aliongeza Oryx Gas inawekeza katika siku zijazo kwa kutekeleza mipango ya kukabiliana na kaboni kupitia elimu ya upishi safi, uchangiaji wa vifaa vya kuanzisha LPG bila malipo kwa baadhi ya mikoa, uhamasishaji wa matumizi ya LPG kupitia uuzaji mkubwa wa mitungi ya gesi kwa bei nafuu.

WAZIRI DK. MABULA APONGEZA

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabulla amesema hatua ya Kampuni ya Oryx Gas kutoa hamasa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia inapaswa kuungwa mkono kwa inaisadia serikali kuhanasisha utunzaji mazingira nchini

Dk. Mabula akizungumza katika hafla ya kukabidhi majiko hayo, Ilemela jijini Mwanza, Waziri Dk. Mabula ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela amesema yatagawanywa katika kata zote 19 za wilaya hiyo kulingana na shughuli zinazofanywa na Mamalishe wilayani humo.

“Tunaona namna ambavyo akinamama wanapata shida katika kutekeleza shughuli zao kwa haraka, katika mazingira mazuri, lakini tunahitaji kutunza mazingira yetu. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuhakikisha huduma zote anazotoa kaanzia kwenye huduma za uchumi, kaja kwenye elimu lakini uwekezaji ameupa kipaumbele.

“Ukija katika huduma za jamii akina mama wengi wamekuwa wakihanagika kutafuta kuni na mkaa, wanakwenda kufyeka misitu.Tumetajiwa hadi kiwango cha uharibifu ambacho kimefanyika. Sasa tunapopata kampuni kama hizi ambazo ziko tayari kuwekeza katika afya na utunzaji bora wa mazingira yetu, lazima tuwashukuru,” ameema.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Araman Benoite.

Mkurugenzi Mtendaji wa Oryx Gas Tanzania Araman Benoite akizungumza wakati wa tukio la ugawaji mitungi ya gesi 500 pamoja na majiko yake kwa Mama Lishe waliopo katika Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 30,2023















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger