Tuesday 28 February 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 1,2023





























Share:

DC JOHARI AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAAFISA UGANI MANISPAA YA SHINYANGA

 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akiwa amepanda Pikipiki wakati wa kukabidhi kwa Maofisa Ugani.

Pikipiki ambazo walizokabidhiwa Maofisa Ugani 

Pikipiki ambazo walizokabidhiwa Maofisa Ugani

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi leo tarehe 28 Februari, 2023 amekabidhi pikipiki 14 kwa Maofisa Ugani katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga huku akiwataka kwenda kuzifanyia kazi iliyokusudiwa na kuleta tija yenye mabadiliko ya haraka kwa wakulima.


Akiongea wakati wa hafla hiyo fupi Mhe. Johari aliwaambia wataalamu hao kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imekusudia kuwawezesha wataalamu katika ngazi zote kwa lengo la kwenda kuongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili waweze kuwahudumia vema zaido wananchi.

"Nitoe angalizo kwenu wataalamu kuwa, Serikali imewawezesha vitendea kazi hivi ili muende kuongeza tija na ufanisi zaidi katika utekelezaji wa majukumu yenu, ikalete mabadiliko na mafanikio yakaonekane kwa wananchi wetu na siyo muende mkazitumie vinginevyo, ikibainika Serikali itamchukulia hatua kali mtumishi huyo," amesema Mhe. Johari.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko alisema kuwa anaishukuru sana Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali watumishi wakiwemo wa Manispaa ya Shinyanga ambapo imepokea pikipiki 14 ikiwa ni gawiwo kwa ajili ya wataalamu wa Ugani.

Akiongea kwa niaba ya maafisa Ugani Bi. Rashida Masawe ambaye ni Afisa Ugani wa Kata ya Kizumbi amesema kuwa wanamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia vyombo vya usafiri, na kwamba, maelekezo ya Mkuu wa Wilaya Mhe. Johari Samizi wataenda kuongeza tija zaidi na wala hawatatumia pikipiki hizo tofauti na lengo kusudiwa.

Hafla ya kukabidhi pikipiki 14 kwa maafisa ugani imefanyika mbele ya Ukumhi wa Lewis Kalinjuna uliopo Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko, Katibu Tawala  Wilaya ya Shinyanga Ndg. Bonipahce Chambi, Wakuu wa Divisheni, Vitengo pamoja na wataalamu mbalimbali wa Manispaa ya Shinyanga.

Share:

WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA TABIA YA KUFANYA MAZOEZI

 


Mbunge wa Jimbo la Malinyi Antipas Mgungusi akiongea na waandishi wa habari katika viwanja vya ushirika ambapo mbio za Kilimanjaro ndipo zilipo fanyika

 Na Woinde Shizza , KILIMANJARO

Watanzania wametakiwa kutenga mda wao kwa ajili ya kufanya mazoezi kwani kwakufanya hivyo kunawasaidia kuendelea kuwa na afya bora na njema pamoja kutenja afya zao na kuwaweka mbali na magonjwa .

Hayo yameelezwa na mbunge wa jimbo la malinyi lililopo mkoani Morogoro Antipas Mgungusi ambaye pia ni muaandaaji wa mbio za zijulikanazo kwa jina la Morogoro marathon alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro wakati alipokuwa akishiriki mashindano ya Kilimanjaro marathon ambapo alisema kuwa ni vyema kila mtanzania akajitaidi kutenga muda wake wa mazoezi kwasababu mazoezi yanafaida kubwa mno ikiwemo na kuweka mwili na afya vizuri.

Alisema watu wengi hawana utaratibu wa kufanya mazoezi jambo ambalo sio zuri kiafya na hivyo kuwataka wananchi kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao.

Aidha aliwapongeza waandaaji wa mashindano ya Kilimanjaro marathon kwa kuanzisha mbio hizo ambapo alisema kuwa mbio hizo zinasaidia sana mkoa huo kwani kwakufanya kipindi zinapofanyika zinasaidia kukuza pato la mkoa na la taifa kwa ujumla huku akibainisha kuwa mashindano hayo pia yanasaidia kuendelea kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi

“Michezo ni muhimu sana kwa afya zetu … tujifunze na sisi tuanze kufanya mazoezi sababu ni muhimu sana kwa afya zetu ,mimi hapa nilipo nimwana michezo mzuri sana na nimekuwa nikishiriki mazoezi mara kwa mara na hii nikwaajili ya kuendelea kuboresha afya yangu niwasihi tu watanzania wenzangu wafanye mazoezi Sana kwani kwakufanya hivyo kunawasaidia hata kuepukana na magonjwa nyemelezi kama magonjwa haya ya pressure unaachana nayo,” alisema .

Aidha aliongeza kuwa mbio kama hizi pamoja na mazoezi ya viungo kwa ujumla vinaimarisha afya ya mwili na akili na kuongeza ufanisi wa kazi, mara ambapo alifafanua kuwa mara nyingi baadhi ya watu wanafanya kazi wakiwa wamekaa na pia hawana muda wa kutosha wa kufanya mazoezi.

Aidha alimpongeza rais Samia Suluhu kwa ajili ya kuzindua filamu ya Royal Tour nakubainisha kuwa filamu hiyo imeendelea kutangaza nchi yetu na hata katika mbio hizo faida yake imeonekana kwani Kuna wageni walikuja kutokana na matangazo ya filamu hiyo lakini walivyofika na kuona mashindano hayo nao wakaamua kushiriki.

Baadhi wa wananchi na wageni wakiwa wanakimbia waliposhiriki katika mashindano ya Kilimanjaro marathon.

Share:

MHANDISI YAHYA SAMAMBA ATEULIWA NA RAIS KUWA KATIBU MTENDAJI TUME YA MADINI

Share:

MANJU MAARUFU JAMES MAKUNGU SOMBI AFARIKI DUNIA... KUZIKWA JUMAMOSI KWA NGOMA


James Makungu Sombi akitoa burudani enzi za uhai wake
James Makungu Sombi enzi za uhai wake akizungumza na Malunde 1 blog nyumbani kwake Kisesa Mwanza
*****

Manju maarufu na Mtaalamu wa Masuala ya Utamaduni wa Kabila la Kisukuma James Sombi (89) amefariki dunia.

James Sombi miongoni mwa waanzilishi wa Makumbusho ya Kabila la Wasukuma Bujora Mwanza ambaye enzi za uhai wake alikuwa mcheza ngoma maarufu ya Bugobogobo na Zeze aliyetangaza utamaduni wa Kabila la Wasukuma ndani na nje ya Tanzania.

Kwa mujibu wa mtoto wake aitwaye Veronica aliyezungumza na Malunde 1 blog, amesema Mzee James Sombi amefariki dunia Jumatatu Februari 27,2023 saa nane mchana baada ya kuanguka.

"Mzee ametutoka baada ya kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake Kisesa Mwanza. Alikuwa anasumbuliwa na tatizo kwenye mishipa ya moyo na alikuwa anasema kifua kinauma na ghafla mchana akaanguka", ameeleza Veronica.

 "Mazishi yatafanyika siku ya Jumamosi Machi 4,2023 katika kijiji cha Mwamanga Magu kama alivyotaka yeye kabla ya kifo chake na kwa kuwa enzi za uhai wake alikuwa mcheza ngoma pia atachezewa ngoma siku ya mazishi yake",amesema Veronica.

James Makungu Sombi alizaliwa mwaka 1934 katika kijiji cha Mwamanga wilayani Magu mkoani Mwanza.
James Makungu Sombi akitoa burudani enzi za uhai wake
\


Soma pia

JAMES SOMBI : KUFANYA SANA MAPENZI KUNAPUNGUZA SIKU ZA KUISHI

MZEE SOMBI : VIJANA WANAOGOPA KUOA KWA SABABU HAWANA KAZI....HAWATAKI USUMBUFU

BABU ATOA DAWA YA KUKOMESHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME...VIBAMIA

Share:

Monday 27 February 2023

PROF.KATUNDU AWAONGOZA WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU MBIO ZA KILI MARATHON 2023


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Prof. Jamal Adam Katundu ( wa sita kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa taasisi zilizochini Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwemo OSHA kabla ya kuanza mbio za kimataifa za Kili Marathon Mkoani Kilimanjaro.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Prof. Jamal Adam Katundu (katikati) akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakikimbia mbio za Kili Marathon Km 21 Mkoani Kilimanjaro.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Prof. Jamal Adam Katundu (katikati) akimaliza mbio za Kili Marathon Km 21


Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa OSHA, Bi Netiwe Mhando (wakwaza kushoto) akikimbia mbio za Kili Marathon Kilomita 21


Baadhi ya watumishi wa OSHA ( katikati) wakikimbia mbio za Kili Marathon Km 5 Mkoani Kilimanjaro wakiambatana na taasisi zingine zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

***********************

Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu na taasisi zake ikiwemo OSHA, wameshiriki katika mbio za Kimataifa za Kili Marathon Mkoani Kilimanjaro wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Jamal Adam Katundu katika mbio za Kilomita 21 na Kilomita 5.

Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali watu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu Bi. Edith Kisanji Simtengu amesema lengo kubwa la kushiriki katika mbio hizo ni kutekeleza sera ya kupambana na magonjwa sugu yasiyoyakuambukiza hivyo kuwafanya wafanyakazi wawe na afya njema na kuhamasika katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

“Tumekuwa tukishiriki mbio hizi za Kili Marathon mara kwa mara lakini awamu hii tumeona nivyema Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na taasisi zake tushiriki kwa pamoja ikiwa lengo ni kutekeleza sera yetu ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kujenga uhusiano mwema mahali pa kazi” Alisema Bi. Edith

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa OSHA, Bi Netiwe Mhando ambaye pia alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa mbio za Km 21 amesema kuwa ushiriki wa mbio hizo unatokana na majukumu ya msingi yanayosimamiwa na taasisi ya OSHA ikiwemo kuimarisha usalama na afya za wafanyakazi.

“Tunaposhiriki katika michezo kama hii maana yake tunahimiza wafanyakazi kujiweka katika hali nzuri ya kiafya hivyo kuilinda nguvu kazi ya taifa nashauri taasisi zingine kuhamasika katika kushiriki michezo na mazoezi mengine ili kuwasaidia wafanyakazi kujiweka imara, kuhamasisha ushirikiano na pia kuleta ari ya kufanya kazi katika maeneo yao ya kazi” alisema Bi Mhando.

Katika mbio hizo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Prof. Jamal Adam Katundu pamoja na watumishi wengine wa Ofisi ya Waziri Mkuu walifanikiwa kumaliza mbio za Km 21 huku watumishi wengine wakikimbia mbio za Km 5. Katika mwaka huu 2023 mbio hizi za Kili Marathon zinatimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002 zikikutanisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi katika mbio za kilometa 42, km21 na Km 5.

Share:

TCDC KUJA NA MKAKATI WA KUKUZA BIASHARA KIDIJITALI


Kamisheni ya Maendeleo ya Ushirika hapa nchini (TCDC) imeanza kutekeleza mpango ya kubadili namna ya kuendesha vyama vya ushirika na kuviwezesha kutumia teknolojia za kisasa katika kufanya shughuli zao.


Mwenyekiti wa Kamisheni ya Maendeleo ya Ushirika hapa nchini Abdulmajid Nsekela ametoa taarifa hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa ushirika kujadili maendeleo ya ushirika na kuweka mkakati wa kuimarisha sekta ya hiyo hapa nchini


Nsekela amesema uwekezaji katika mifumo ya kisasa ya kidijitali itaongeza ufanisi wa kiutendaji katika Vyama vya Ushirika, pamoja na Mamlaka za Usimamizi wa sekta hiyo.
Ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine lakini mapendekezo yatakayotolewa katika mkutano huo yatasaidia kuuboresha mfumo wa ushirika kuwa wa kisasa zaidi na ili kuwawezesha wananchi kushiriki ipasavyo kwa ustawi wao na wa Taifa kwa ujumla.


“Ni matumaini yangu kuwa Maazimio yatakayofikiwa kupitia Mkutano huu yatapaswa kutekelezwa ipasavyo na kila mdau na kwamba taarifa ya utekelezaji itakuwa inatolewa na kujadiliwa mara kwa mara”-amesema Nsekela.
Kwa upande wake Mrajisi wa Ushirika nchini Dkt. Benson Ndiege amesema lengo kubwa la mkutano huo wa wadau wa ushirika ni kujadili maendeleo ya ushirika na kuweka mkakati wa kuimarisha sekta hiyo hapa nchini.


“Mkutano huu ni muhimu kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Ushirika hapa nchini, lakini pia tumekutana wadau wote ili kuja na mapendekezo ya pamoja ya kuendeleza sekta hii kwa maendeleo ya Taifa”- amesema Ndiege.
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa ushirika uliolenga kujadili maendeleo ya ushirika na kuweka mkakati wa kuimarisha sekta hiyo nchini, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam, Februari 27, 2023.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Charles Jishuri akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa ushirika uliolenga kujadili maendeleo ya ushirika na kuweka mkakati wa kuimarisha sekta hiyo nchini, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam, Februari 27, 2023.




Sehemu ya wadau wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), wakifatilia mkutano uliolenga kujadili maendeleo ya ushirika na kuweka mkakati wa kuimarisha sekta hiyo nchini, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Benki ya CRDB, jijini Dar es salaam, Februari 27, 2023.
















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger