Wednesday, 22 February 2023

MAADHIMISHO YA NUSU KARNE YA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO KUFANYIKA MACHI 16....UKAME BADO NI CHANGAMOTO

...


Kamishna msaidizi wa hifadhi ambaye pia ni Mkuu wa hifadhi ya KINAPA ,Angela Nyaki akiongea na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya kwanza ya miaka 50 tangia kuanzishwa kwa hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro


Na Woinde Shizza , ARUSHA


Mabadiliko ya tabia nchi yaliyosababishwa na ukame wa muda mrefu katika mikoa ya ukanda wa pwani mwa Tanzania pamoja na shughuli za kibinadamu yanatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu ya kuyeyuka kwa theluji ya mlima Kilimanjaro.


Wataalam wa uhifadhi wanaeleza kuwa Hali hiyo imekuwa ikisababishwa na upepo kuvuma kuelekea mlima huo mrefu kupita yote barani Afrika.


Hayo yameelezwa na kamishna msaidizi wa hifadhi ambaye pia ni Mkuu wa hifadhi ya KINAPA ,Angela Nyaki wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya kwanza ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro yatakayofanyika, Machi 16 Mwaka huu katika makao makuu ya mlima huo yaliyopo, Marangu Mkoani Kilimanjaro .


Alisema kuwa upepo wa unapotoka katika mikoa ya ukanda wa pwani unapokuja katika mlima Kilimanjaro unakuja ukiwa mkavu pamoja na joto ambapo ndio unasababisha barafu kuendelea kuungua kwa hiyo sio jukumu la hifadhi ya mlima huo bali ni jukumu la Tanzania nzima kuhakikisha tunajihamisha hadi katika katika mikoa hiyo ambapo wanakata mikaa 
kwa wingi ambapo madhara yake yanaonekana kabisa katika katika mlima huo haswa kule kileleni.


"Tumejaribu kufuatilia sana kupitia ikolojia tukagundua kuwa kukiwa na upepo mkali sana baharini basi na mlimani kunakuwa na upepo mkali pia " ,alisema Angela.


Alibainisha kuwa maadhimisho hayo yataanza Machi 1,hadi kilele machi 16 mwaka huu,na mambo mbalimbali yatafanyika ikiwemo usafi wa Mlima utakaofanyika kwa siku kumi kuanzia machi 1,ambapo wadau wa utalii wapatao 500 watashiriki.


Alisema shughuli zingine zitakazofanyika katika sherehe za maadhimisho hayo ni pamoja na ugawaji na upandaji wa miti, zoezi litakalozinduliwa na mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ,Pia watawatembelea waongoza utalii wa miaka ya 70 ili kuzungumza nao na kupata uzoefu wao na ushauri wao


Alisema tangu kuanzishwa kwa shughuli za utalii katika mlima Kilimanjaro, mafanikio kadhaa yamepatikana ikiwemo ongezeko la watalii na kufikia elfu 50 kwa mwaka, kuongezeka kwa njia za kupandisha mlima huo kutoka njia moja hadi kufikia njia sita .

Naibu Kamishna wa Uhifadhi na maendeleo ya biashara,Herman Batiho akiongea na waandishi wa habari


Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Uhifadhi na maendeleo ya biashara,Herman Batiho alisema maadhimisho hayo ya kwanza ya aina yake yalioandaliwa na Shirika la hifadhi za taifa (TANAPA)yanalenga pia kuutambulisha umma na dunia kwa ujumla kuwa mlima huo upo na unapatikana katika nchi ya Tanzania pekee.


Alisema kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Marangu, mkoani Kilimanjaro, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango .


Alisema maadhimisho ya jubilee ya miaka 50 ya mlima Kilimanjaro ni utaratibu wa kawaida wa Tanapa kufanya katika hifadhi zake pindi sinapo timiza miaka 25 au 50 na hii ni baada ya kufanya maadhimisho kama hayo ya miaka 60 ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti


"Kilele cha maadhimisho ya Mlima kilimanjaro kitafanyika Marangu Mkoani Kilimanjaro yalipo makao makuu ya Mlima huo huku makamu wa rais dkt Philip Mpango akitarajiwa kuwa mgeni rasmi " alibainisha


Alisema mlima huo wenye urefu wa kilometa 5,895 ulianzishwa rasmi kama hifadhi ya Taifa Kilimanjaro , Machi 16, Mwaka 1973 kwa ajili ya shughuli za utalii.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger