Friday, 17 February 2023

RUWASA YASAINI MKATABA WA UNUNUZI WA BOMBA ZA CHUMA UJENZI WA MRADI WA MAJI NDUKU - BUSANGI... DC MHITA ATAKA YALETWE HARAKA

...

Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama Mkama Msilanga (kushoto), Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela (katikati) na Mhasibu Miradi wa Kampuni ya Ukandarasi ya Otonde Construction & General Supplies Ltd, Martine Nkomela (kulia) wakitia saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi halmashauri ya Msalala.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga na Kampuni ya Ukandarasi ya Otonde Construction & General Supplies Ltd wametia saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi katika Halmashauri ya Msalala.

Hafla fupi ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi imefanyika leo Ijumaa Februari 17,2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama na kushuhudiwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Mboni Mhita na wadau wa maji.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amemtaka Mkandarasi Otonde Construction & General Supplies Ltd kuzingatia mkataba kwa kuhakikisha anapeleka mabomba ya maji kwa wakati ili wananchi waanze kupata huduma ya maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria.

“Tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuleta fedha ili kutekeleza miradi ya maji lengo likiwa ni kumtua mama ndoo kichwani. Tunataka kuondoa adha ya maji kwa wananchi, Mkandarasi hakikisha unaleta mabomba kwa mujibu wa mkataba uliosaini na uwekaji mabomba ufanyike haraka”,amesema Mhita.

Mkuu huyo  wa wilaya amewataka wananchi kutunza miundombinu ya maji na kuachana na tabia kuvamia vyanzo vya maji na miundombinu ya maji ili miradi ya maji idumu.

Akielezea kuhusu Ujenzi wa Mradi wa Maji Nduku – Busangi, Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama Mkama Msilanga amesema jumla ya mita 18,927 za bomba za chuma zitanunuliwa na Mzabuni na kuletwa eneo la mradi na kiasi hicho cha bomba kitatosheleza kukamilisha mtandao wa bomba kwa awamu ya kwanza.

“Utekelezaji wa mradi huu ulipangwa kutekelezwa kwa awamu mbili ambapo katika awamu ya kwanza wananchi 17,108 wa vijiji vitatu ambavyo ni Busangi, Nyamigege na Ntundu watanufaika na mradi huo. Tayari tumekamilisha ujenzi wa matenki mawili yenye mita za ujazo 175, vituo 16 vya kuchotea maji,ujenzi wa ofisi ya watoa huduma ngazi ya jamii (CBWSO),kuchimba mtaro na kulaza bomba la urefu wa km 20.3, kazi ambazo zimetekelezwa kwa Force Account. Kiasi cha shilingi 1,126,571,596/= kimetumika kutekeleza kazi hizo ikiwemo kulipia bomba za plastiki (HDPE) na bomba za chuma. Ujenzi wa awamu ya kwanza umefikia asilimia 35%”,ameeleza Msilanga.
Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama Mkama Msilanga akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji wilayani Kahama.

“Katika awamu ya pili ya ujenzi wa mradi huu ilipangwa kujenga matenki mawili yenye jumla ya mita za ujazo 755, ujenzi wa mtandao wa maji wenye jumla ya km 29.8 na ujenzi wa vituo 18 vya kuchotea maji katika kijiji cha Ntobo na Gulla. Katika awamu hii vijiji vitatu vya Ntobo, Gulla na Masabi na makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala vitanufaika na mradi huu ambapo jumla ya watu 18,285 watanufaika na mradi kwa awamu ya pili”,amefafanua Msilanga.

Msilanga amesema utekelezaji wa mradi huo ulioanza Julai 2020, umechelewa kukamilika kwa wakati kutokana na changamoto ya fedha za ujenzi wa mradi na sasa utiaji saini wa ununuzi wa bomba za chuma umefanyika ambapo jumla ya mita 18,927 za bomba za chuma zitanunuliwa na Mzabuni na kuletwa eneo la mradi na kiasi hicho cha bomba kitatosheleza kukamilisha mtandao wa bomba kwa awamu ya kwanza.

Hata hivyo amesema kwa kipindi cha Mwaka wa Fedha 2021/2022 RUWASA wilaya ya Kahama imekamilisha ujenzi wa miradi 13 ya maji yenye thamani ya shilingi 16,235,321,604.37/= katika halmashauri zote tatu (Msalala Miradi 6, Ushetu 5 na Manispaa ya Kahama 2).

Katika hatua nyingine amesema RUWASA Kahama inaendelea na shughuli za ujenzi, upanuzi, ukarabati na usanifu wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji.

Naye Mhasibu Miradi wa Kampuni ya Ukandarasi ya Otonde Construction & General Supplies Ltd, Martine Nkomela ameahidi kupeleka mabomba ya chuma ya mradi huo kwa wakati.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela amesema changamoto zilizopo kuwa ni ufinyu wa bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji,ukosefu wa vyanzo vya maji ya uhakika kwenye baadhi ya maeneo, matumizi madogo ya maji wakati wa masika, uvamizi wa maeneo ilipojengwa miundombinu ya maji hususani matanki, uharibifu wa miundombinu iliyokwisha jenga hususani mabomba ya maji na valves na uvamizi wa nyanzo vya maji kwa kufanya shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela.

Mhandisi Payovela amesema wataendelea kufanya tafiti kwa kina kwa ajili ya kupata vyanzo vya maji chini ya ardhi, kutumia kwa ufanisi fedha zinazopatikana kutekeleza miradi yenye tija kwa jamii, kutenga bajeti kwa ajili ya ukarabati wa miradi, kuendelea kuwahamasisha wananchi kutumia maji safi na salama na kutoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na miundombinu ya maji.

Nao Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mibako Mabubu na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji wa halmashauri hiyo, Ibrahim Six wameomba utekelezaji wa mradi huo utakaonufaisha kata tatu za Nduku, Busangi na Ntobo ufanye haraka kwani ni muda mrefu wananchi wanapata adha ya kutafuta maji safi na salama.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa hafla fupi ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi halmashauri ya Msalala leo Ijumaa Februari 17,2023
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akizungumza wakati wa hafla fupi ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi halmashauri ya Msalala 

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akiwa kwenye hafla fupi ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi halmashauri ya Msalala 
Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timoth Ndanya akizungumza wakati wa hafla fupi ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi halmashauri ya Msalala 
 Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela akizungumza wakati wa hafla fupi ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi halmashauri ya Msalala  

Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama Mkama Msilanga akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi wakati wa hafla fupi ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi halmashauri ya Msalala 

Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama Mkama Msilanga (kushoto), Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela (katikati) na Mhasibu Miradi wa Kampuni ya Ukandarasi ya Otonde Construction & General Supplies Ltd, Martine Nkomela (kulia) wakitia saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi halmashauri ya Msalala 

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela akibadilishana nyaraka na Mhasibu Miradi wa Kampuni ya Ukandarasi ya Otonde Construction & General Supplies Ltd, Martine Nkomela (kulia) baada ya kutia saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi halmashauri ya Msalala
 
Mhasibu Miradi wa Kampuni ya Ukandarasi ya Otonde Construction & General Supplies Ltd, Martine Nkomela akizungumza wakati wa hafla fupi ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi halmashauri ya Msalala 
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji wa halmashauri ya Msalala, Ibrahim Six akizungumza wakati wa hafla fupi ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi halmashauri ya Msalala 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mibako Mabubu akizungumza wakati wa hafla fupi ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi halmashauri ya Msalala 

Meya wa Manispaa ya Kahama Yahya Ramadhani akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama wakati wa hafla fupi ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi halmashauri ya Msalala 
Wadau wakiwa kwenye hafla ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi
Wadau wakiwa kwenye hafla ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi
Wadau wa maji wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa hafla ya Utiaji saini Mkataba wa Ununuzi wa Bomba za Chuma za Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Nduku – Busangi.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger