Sunday, 12 February 2023

YANGA SC YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA WAARABU, YACHAPWA 2-0 NA US MONASTIR

...

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Yanga imeshindwa kuibuka na ushiindi mbele ya timu ya US Monastir ya nchini Tunisia baada ya kupokea kichapo cha mbao 2-0 kwenye mchezo huo wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Olympic Rades, Yanga imekuwa ikishindwa kumiliki mpira kwa muda mrefu hivyo kuwapa nafasi US Monastir kucheza mpira kwa uhuru na kuweza kupata mabao mawili ya haraka katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Yanga Sc ilirudi kipindi cha pili kutafuta mabao bila mafanikio licha ya kuwapumzisha baadhi ya wacheaji na kuingiza igizo jipya .

Mabao ya US Monastir yamefungwa na nyota wao Mohamed Saghraoui dakika ya 10 ya mchezo na bao la pili likifungwa na Boubacar Traore dakika ya 16 na kufanya matokeo kuwa 2-0.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger