Monday, 27 February 2023

TMDA YATOA ELIMU YA UTOAJI TAARIFA MADHARA NA MATUKIO YATOKANAYO NA MATUMIZI YA VIFAA TIBA NA VITENDANISHI KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA SHINYANGA

...

 


Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa Magharibi Geita Dkt. Edgar Mahundi akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba - TMDA imetoa elimu ya uhamasishaji juu ya utoaji wa taarifa za madhara na matukio yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba na vitendanishi kwa watoa huduma za afya mkoa wa Shinyanga.

Elimu hiyo imetolewa leo Jumatatu Februari 27,2023 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga yakishirikisha Madaktari, Wafamasia, Wataalamu wa maabara, watunza vifaa tiba na mafundi sanifu wa vifaa tiba na vitendanishi.

Akitoa elimu hiyo, Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa Magharibi Geita Dkt. Edgar Mahundi amesema TMDA inaendelea kutoa elimu ya uhamasishaji kuhusu utoaji taarifa za madhara na matukio ya vifaa tiba na vitendanishi kwa watoa huduma za afya ili wataalamu hao wa afya wanapobaini vifaa tiba vinaleta madhara kwa wagonjwa watoa taarifa TMDA.

“Tunataka watoa huduma za afya wanapobaini vifaa tiba vinaleta madhara kwa wagonjwa watoe taarifa TMDA lakini pia watoa huduma wa afya wanapobaini vifaa tiba havifanyi kazi inayotakiwa watoe taarifa ili TMDA tufanye ufuatiliaji”,ameeleza Dkt. Mahundi.

Amezitaja njia za utoaji wa taarifa za madhara na matukio yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba na vitendanishi ni kupitia Fomu maalumu ya rangi ya machungwa, kutumia simu ya kiganjani/mkononi kwa kubonyeza *152*00# kisha unafuata maelekezo pamoja kutoa taarifa kwa kupiga simu bure namba 0800110084

“TMDA tumetoa elimu hii kwa watoa huduma za afya katika Manispaa ya Shinyanga lakini pia tutatoa elimu katika Manispaa ya Kahama na maeneo mbalimbali nchini kwenye hospitali, zahanati na vituo vya afya vya serikali na watu binafsi ikiwa ni sehemu ya kazi za TMDA kuhakikisha vifaa tiba na vitendanishi vinapozunguka katika Soko la Tanzania vinakuwa na ubora, usalama na ufanisi unaokidhi vigezo”, ameeleza Dkt. Mahundi.

Kwa upande wake, Afisa Usajili Dawa Daraja la kwanza kutoka TMDA, Bw. Haninu Salum Nakuchema amesema TMDA inatoa elimu kuhusu utoaji taarifa za madhara na matukio yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba na vitendanishi ili kuhakikisha jamii inatumia vifaa tiba na vitendanishi vyenye ubora, usalama na ufanisi.


Nakuchema amewataka Madaktari, Wafamasia, Wataalamu wa maabara, watunza vifaa tiba na mafundi sanifu wa vifaa tiba na vitendanishi kushirikiana na TMDA kwa kutoa taarifa za madhara na matukio yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba na vitendanishi ili kuhakikisha jamii inakuwa salama muda wote.

Nao watoa huduma za afya waliopatiwa elimu hiyo wameishukuru TMDA kwa kutoa elimu hiyo na kuahidi kuwa watashirikiana na TMDA kuifanya jamii kuwa salama kwa kutoa taarifa endapo watabaini vifaa tiba vinaleta madhara kwa wagonjwa ama havifanyi kazi kwa ufanisi unaotakiwa.
Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa Magharibi Geita Dkt. Edgar Mahundi akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Afisa Usajili Dawa Daraja la kwanza kutoka TMDA, Bw. Haninu Salum Nakuchema akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Mratibu wa Pharmacovigillance mkoa wa Shinyanga, Clementina Salutari akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga
Maafisa kutoka TMDA wakipiga picha ya kumbukumbu na watoa huduma za afya katika Manispaa ya Shinyanga
Maafisa kutoka TMDA wakipiga picha ya kumbukumbu na watoa huduma za afya katika Manispaa ya Shinyanga
Maafisa kutoka TMDA wakipiga picha ya kumbukumbu na watoa huduma za afya katika Manispaa ya Shinyanga


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger