Tuesday, 28 February 2023

DC JOHARI AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAAFISA UGANI MANISPAA YA SHINYANGA

...

 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akiwa amepanda Pikipiki wakati wa kukabidhi kwa Maofisa Ugani.

Pikipiki ambazo walizokabidhiwa Maofisa Ugani 

Pikipiki ambazo walizokabidhiwa Maofisa Ugani

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi leo tarehe 28 Februari, 2023 amekabidhi pikipiki 14 kwa Maofisa Ugani katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga huku akiwataka kwenda kuzifanyia kazi iliyokusudiwa na kuleta tija yenye mabadiliko ya haraka kwa wakulima.


Akiongea wakati wa hafla hiyo fupi Mhe. Johari aliwaambia wataalamu hao kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imekusudia kuwawezesha wataalamu katika ngazi zote kwa lengo la kwenda kuongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili waweze kuwahudumia vema zaido wananchi.

"Nitoe angalizo kwenu wataalamu kuwa, Serikali imewawezesha vitendea kazi hivi ili muende kuongeza tija na ufanisi zaidi katika utekelezaji wa majukumu yenu, ikalete mabadiliko na mafanikio yakaonekane kwa wananchi wetu na siyo muende mkazitumie vinginevyo, ikibainika Serikali itamchukulia hatua kali mtumishi huyo," amesema Mhe. Johari.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko alisema kuwa anaishukuru sana Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali watumishi wakiwemo wa Manispaa ya Shinyanga ambapo imepokea pikipiki 14 ikiwa ni gawiwo kwa ajili ya wataalamu wa Ugani.

Akiongea kwa niaba ya maafisa Ugani Bi. Rashida Masawe ambaye ni Afisa Ugani wa Kata ya Kizumbi amesema kuwa wanamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia vyombo vya usafiri, na kwamba, maelekezo ya Mkuu wa Wilaya Mhe. Johari Samizi wataenda kuongeza tija zaidi na wala hawatatumia pikipiki hizo tofauti na lengo kusudiwa.

Hafla ya kukabidhi pikipiki 14 kwa maafisa ugani imefanyika mbele ya Ukumhi wa Lewis Kalinjuna uliopo Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko, Katibu Tawala  Wilaya ya Shinyanga Ndg. Bonipahce Chambi, Wakuu wa Divisheni, Vitengo pamoja na wataalamu mbalimbali wa Manispaa ya Shinyanga.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger