Asilimia 97 Wachaguliwa Kidato cha Kwanza
Jumla ya wanafunzi 503,914 kati ya wanafunzi 518,034
waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwakani, sawa na asilimia 97.3
wamepata nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za
serikali, huku wengine 12,847 wamekosa nafasi za kujiunga na masomo
kuanzia mwezi Januari mwakani.Aidha Sh. bilioni 131 zimetengwa na
serikali kwa ajili ya shughuli za uendeshaji shule, chakula kwa
wanafunzi wa bweni na fidia ya ada ya mitihadi kwa kipindi cha kuanzia
mwezi Desemba mwaka huu hadi Juni mwaka 2016.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe.Selemani Jafo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa, kati ya
wanafunzi hao waliochaguliwa, wasichana ni 255,843 sawa na asilimia 99.2
na wavulana ni 248,076 sawa na asilimia 97.7Alisema idadi ya wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza
imeongezeka kwa asilimia 0.7 ikilinganishwa na asilimia 97.23 ya
wanafunzi waliochaguliwa awamu ya kwanza kuingia kidato cha kwanza mwaka
2015.
Aidha wanafunzi 610 sawa na asilimia 61.2
ya wanafunzi 997 wenye ulemavu waliofanya mtihani wa kuhitimu elimu ya
msingi wamefaulu na wote wamechaguliwa kujiunga na shule za
sekondari.Kuhusu mikoa iliyoshindwa kupata nafasi kwa wanafunzi wote
waliofaulu, Mhe.Jafo alisema Wanafunzi 12,847 kati ya Wanafunzi 518,031
waliofaulu mtihani wa darasa la saba uliofanyika Septemba 9 mwaka huu,
wameshindwa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa
madarasa katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Mtwara.
Naibu
Waziri alieleza kuwa katika mkoa wa Dar es salaam idadi ya wanafunzi
waliokosa fursa ya kuanza masomo mwakani ni wanafunzi 12,225 wa jiji la
Dar es Salaam, ambapo wilaya ya Temeke ni wanafunzi 4,707, Ilala
wanafunzi 2,365 na Kinondoni wanafunzi 3,183.Kwa upande wa mkoa wa
Dodoma; Halmashauri ya Dodoma mjini wanafunzi 131 na Kongwa wanafunzi
52, na kwa mkoa wa Mtwara katika halmashauri ya Masasi ni wanafunzi 200
ambao wamekosa nafasi.
“Pia tunaziagiza
Halmashauri, wakuu wa shule na walimu kuandaa mazingira ya kuwapokea
wanafunzi watakao anza masomo mwezi Januari,†alisema Jafo.Kuhusu
gharama za kuendesha shule, alisema serikali imetenga Sh. bilioni 18.77
kwa kila mwezi kuanzia Desemba mwaka huu hadi Juni mwaka 2016 kwa ajili
ya mahitaji ya shule kiasi ambacho ni Sh. bilioni 131 kwa miezi saba.
Jafo
alisisitiza kuwa, fedha hizo zitakuwa zinafuatiliwa kama zinafika kwa
wakati na matumizi yake na watakaozifanyia ubadhilifu watawajibishwa.Pia
alitilia mkazi agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Dkt. John Magufuli kuhakikisha wanafunzi wanasoma bure kuanzia shule za
awali hadi kidato cha nne kwa kuwataka wazazi kujiandaa na sare za shule
pekee.
“Nawasisitizia wakuu wa shule na
watendaji wengine kuhakikisha elimu ni bure, ole wake Mkuu wa shule au
Mtendaji wa Halmashauri atakayepokea mchango wa mzazi,†alisema
Jafo.Jumla ya wanafunzi 775,273 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya
mtihani wa kumaliza darasa la saba kuanzia tarehe 9 hadi 10 septemba
2015 ambapo watahiniwa 763,606 sawa na asilimia 98.5 ya waliosajiliwa
walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment