Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akikagua bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015
ambako alikwenda kupata ukweli kuhusu makontena 2,431yaliyopitia kwenye bandari
hiyo bila kulipiwa kodi ya serikali (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ULE “moto”
aliouwasha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Kassim Majaliwa
kwenye bandari ya Dar es Salaam wiki iliyopita, na kukolezwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli,
wa kumsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw. Rished Bade, umeendelea kusambaa
kwenye eneo lote la bandari na viunga vyake baada ya leo tena Bw. Majaliwa
kufanya ziara ya kushtukiza na kukuta makontena mengine 2431yenye bidhaa hayajulikani
yaliko.
Baada
ya kugundua hilo tena kwa ushahidi wa nyaraka, Waziri
Mkuu ambaye wiki iliyopita aliahidi kuwa "Tunataka ku-deal na wajanja
wajanja wa TRA." ameagiza kabla ya jua kuzama leo hii Desemba 3, 2015,
awe amepata majibu
ya kina na timilifu juu ya “uhuni” huo uliofanywa na watumishi wa umma pale
bandarini. Waziri Mkuu pia alifanya ziara kama hiyo pale stesheni kuu ya reli iliyo chini ya Kampuni ya Reli Tanzania TRL
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfumo wa kukagua makontena bandarini kwa
kutumia scaner huku akipata maelzo kutoka kwa Ofisa wa forodha, January Shauri
wakati alipotembelea bandari ya Dar es salaam Desemba 3, 2015 kutaka
kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431 yaliyopita bandarini hapo bila
kulipiwa kodi ya serikali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu utoaji bili za kulipia kodi za
serikali kwa watumiaji wa bandari ya Dar es salaam kutoka kwa ofisa mwandamizi
wa masuala ya fedha , Bw. Sartho Mbuya wakati alipotembelea bandari hiyo
Desemba 3, 2015 kutaka kujua ukweli wa tuhuma za makontena 2431
yaliyopita bandarini hapo bila kulipiwa kodi za serikali.(Picha na Ofisi ya
Waziri )
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es salaam,
Bw. Abel Mhanga (kulia) orodha ya makontena 2,431 yaliyopitia kwenye banda ya
Dar es salaam bila kulipiwa kodi wakati alipofanya ziara kwenye bandari hiyo
Desemba ,3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimwonyesha Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es salaam,
Bw. Abel Mhanga (kulia) orodha ya makontena 2,431 yaliyopitia kwenye banda ya
Dar es salaam bila kulipiwa kodi wakati alipofanya ziara kwenye bandari hiyo
Desemba ,3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli nchini TRL wakati alipotembelea stesheni ya Dar es salaam
kukagua uendeshaji wa Shirika hilo Desemba 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea steheni ya reli ya Dar es salaam Desemba 3,
2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
|
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea bandarini na shirika la
reli Tanzania(TRL). Akiwa bandarini amekagua mfumo wa utoaji na uingizaji mizigo bandarini. Katika maongezi ya awali meneja wa bandari alimuhakikishia kuwa mfumo hauruhusu kontena kuibiwa lakini waziri mkuu alienda na ripoti ya ukaguzi na kumuonyesha majina ya waliopitisha makontena zaidi 2431 bila kulipiwa kodi.
Amempa muda wa masaa matatu hadi saa kumi na mbili jioni aambiwe hatua zilizochukuliwa kwa wahusika kwa sababu anawafahamu.
Katika hatua nyingine, Waziri mkuu alitembelea shirika la reli na kukuta mabilioni yametumika na miradi iliyokusudiwa haijatekelezwa.
0 comments:
Post a Comment