Spika wa
Bunge, Anne Makinda amesema muda wa Bunge utaongezwa ili kutoa nafasi
kwa serikali kuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kodi ya
Mapato (VAT).
Wiki
iliyopita, Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola aliomba mwongozo na alipopewa
nafasi alimlalamikia Spika wa Bunge kuwa katika ratiba ya bunge, haoni
mahali ambapo kuna nafasi ya wabunge kujadili Muswada wa Marekebisho ya
Sheria ya VAT.(Martha Magessa)
Lugola,
(CCM) baada ya kauli yake, alitishia kukusanya saini za wabunge
kumwondoa Spika Makinda iwapo muswada huo hautaletwa katika Bunge la
Bajeti na zaidi ni kwa ajili ya kufuta misamaha ya kodi isiyo na tija.
Muda
mfupi baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Makinda alitangaza
hatua hiyo ya Bunge kuongeza muda.
"Kwa
mujibu wa kanuni zetu hatuingizi kitu kingine katika Bunge la Bajeti
zaidi ya bajeti, lakini tunaangalia uwezekano wa kuongeza muda baada ya
bajeti kwa siku chache kwa sababu ya mambo yanayotakiwa kufanyika,"
alisema na kuongeza;
"Naambiwa kuwa Serikali inataka kuleta sheria inayohusiana na VAT."
Makinda aliwataka wabunge kusoma vizuri kanuni za Bunge kwa sababu Spika hahusiki kuletwa muswada bungeni.
Katika
hoja yake, mbunge huyo wa Mwibara, alisema nchi inapoteza Sh1.5 trilioni
kwa misamaha ya kodi wakati bajeti ya Serikali kwa mwaka jana ina
upungufu wa kiasi hicho hicho cha fedha.
"Kama
hawajaleta muswada kiofisi, mimi siwezi kufanya chochote lakini
nimesikia kuwa serikali inataka kuleta muswada huo,"alisema Makinda.
Makinda alisema kuwa kuongezwa kwa siku hizo kunalenga kuwawezesha wabunge kujadili ripoti ya migogoro ya ardhi nchini.
Alisema
Kamati ya Bunge iliyopewa kuchunguza migogoro hiyo ilikwenda mbali zaidi
na kuona vitu vingi ikiwemo matatizo yaliyopo katika mfumo.
CHANZO:MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment