Friday 30 May 2014

RACHEL AMUUMIZA WASTARA

...

KIFO cha msanii wa filamu, Rachel Haule kimewaumiza wengi lakini baadhi yao ni wasanii wenzake, Halima Yahaya ‘Davina’ aliyeachiwa hausigeli wa marehemu katika mazingira ya ajabu huku Wastara Juma akiumizwa na viatu na pochi alivyopewa na Rachel kabla hajafariki dunia.
Msaniii wa Bongo Movie Halima Yahaya ‘Davina’ akiwa na simanzi kubwa.
Akizungumza na Ijumaa juzi, Davina alisema alihangaika sana kumtafutia Rachel hausigeli ili atakapojifungua asipate shida lakini siku moja kabla ya kifo, alipompigia simu akitaka ampelekee mtu wake simu haikupokelewa hadi alipopata taarifa za kifo.
“Aliniambia nimtafutie msichana, nikafanya hivyo, wakati najipanga kumpelekea nyumbani kwake nasikie eti kafariki, naumia sana,” alisema Davina.
Naye Wastara alisema: “Nilikutana naye wiki chache zilizopita, nikaipenda pochi yake, akaniambia atanipa. Siku iliyofuata akaniletea na viatu, leo naambiwa hatunaye, mbona hivi vitu vitanitesa sana!”
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger