Watu watano wamekufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama ndani ya Ziwa Victoria.
Kamanda wa Polisi wa Mkoawa Kagera, George Mayungaalisema ajali hiyo ilitokea Mei 23 mwaka huu saa 8 usiku. Boti
ya Mv Kitoko II waliyokuwa wakisafiria kutoka Bugombe kupitia Kasenye kwenda Mganza wilayani Chato, ilizimika ghafla ikiwa katikati ya ziwa.Alisema boti hiyo inayomilikiwa na Mama Chacha aishiye Muganza ,
ilikuwa na abiria hao watano,ambao wote walikufa maji. Maiti
aliyepatikana ni mfanyabiashara raia wa Rwanda, Jane Mlekatete (36)
ambaye mwili wake ulikutwa ukielea. Wengine waliozama ambao
hawajapatikana ni Chikola Filbert (22) mkazi wa Muganza, Mapinduzi
Daud ( 38 )mkazi wa Mwanza, Ashana Suzy waliotambuliwa kwa jina moja
moja, wote wakazi wa Kasenyi na Mavombe (23) ambaye ni mkazi wa
Muganza.Alisema chanzo cha ajali hiyo ni boti kubeba mzigo mkubwa. Kwa
mujibu wa Kamanda, ilikuwa imebeba magunia 210.Chanzo kingine cha
ajali hiyo ni kwamba licha ya kubeba mzigo mkubwa, ilisafiri usiku
wakati kukiwa na upepo mkali na mawimbi yaliyosababisha injini ya
botihiyo kuzimika kabla ya kuzama.
0 comments:
Post a Comment