AMA kweli duniani kuna sarakasi!
Takribani siku kumi tangu alipofariki dunia aliyekuwa ‘kichwa’ kwenye
filamu za Kibongo, Adam Phillip Kuambiana (38), mrembo aliyejitambulisha
kwa jina Mary Njombe amenaswa na nguo za staa huyo wakati mali za
marehemu hazijagawanywa.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu makini, Mary
ambaye ni mkazi wa Magomeni Hospitali, Dar amekuwa akipigilia pamba za
marehemu hasa baada ya jamaa huyo kutangulia mbele ya haki.
“Jamani njooni huku Magomeni Hospitali hapa mtaa wa pili kuna mwanamke anatinga nguo za marehemu Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.
“Jamani njooni huku Magomeni Hospitali hapa mtaa wa pili kuna mwanamke anatinga nguo za marehemu Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu walifanya msako eneo hilo hadi wakamnasa Mary.
Katika mahojiano na gazeti hili, Mary alisema kuwa alikuwa mchumba wa Kuambiana na alichobahatika kubaki nacho ni nguo ambazo alimpatia mara ya mwisho amfulie (zinaonekana pichani).
Katika mahojiano na gazeti hili, Mary alisema kuwa alikuwa mchumba wa Kuambiana na alichobahatika kubaki nacho ni nguo ambazo alimpatia mara ya mwisho amfulie (zinaonekana pichani).
Mary alisema kuwa yeye na Kuambiana walifahamiana tangu mwaka 2006 ambapo alikuwa akimbembeleza kuwa naye.
“Mwaka 2008 ndiyo tulianza rasmi
uhusiano kwani mimi nilikuwa sina mwanaume na yeye hakuwa na mtu hivyo
tulikubaliana na alikuwa akijulikana nyumbani kwetu,” alifunguka Mary.
Mwanadada huyo alisema kuwa yeye na
Kuambiana walikuwa wakikutana kwenye Hoteli ya Grand iliyopo Magomeni,
Dar na mara nyingi alikuwa akimpikia chakula na kumpelekea ‘lokesheni’.
“Nimeumia sana na sijielewi, Kuambiana ameniachia donda kubwa, nakumbuka neno la mwisho aliniambia nimpende sana kwani ipo siku nitamkubuka,” alisema Mary huku akiangua kilio.
“Nimeumia sana na sijielewi, Kuambiana ameniachia donda kubwa, nakumbuka neno la mwisho aliniambia nimpende sana kwani ipo siku nitamkubuka,” alisema Mary huku akiangua kilio.
Alipoulizwa kama kweli nguo hizo ni za
marehemu Kuambiana, alizama ndani akatoka akiwa amevaa pensi na shati la
‘drafti’ alilokuwa anapendelea kulivaa staa huyo ambalo ni maarufu
sana.
Kuambiana alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 17, mwaka huu baada ya kuanguka chooni kutokana na kusumbuliwa vidinda vya tumbo.
Kuambiana alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 17, mwaka huu baada ya kuanguka chooni kutokana na kusumbuliwa vidinda vya tumbo.
0 comments:
Post a Comment