Friday, 23 May 2014

MWONGOZO WA MATUMIZI YA VIWANGO VYA UFAULU 2014/2015

...
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
MWONGOZO WA MATUMIZI YA VIWANGO VYA UFAULU
NA UTARATIBU WA KUTUNUKU MATOKEO YA KIDATO
CHA NNE NA KIDATO CHA SITA
IMETOLEWA NA:
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
S.L.P 2624
DAR ES SALAAM
APRILI, 2014     
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
MWONGOZO WA MATUMIZI YA VIWANGO VYA UFAULU NA
UTARATIBU WA KUTUNUKU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
NA KIDATO CHA SITA
IMETOLEWA NA:
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
S.L.P 2624
DAR ES SALAAM
APRILI, 2014
            
1.0
UTANGULIZI
Ipo mifumo anuwai inayotumiwa na Nchi mbalimbali duniani katika
kupanga viwango vya ufaulu kwa ajili ya kutunuku vyeti kwa watahiniwa
waliofanya mitihani ya Taifa. Hata hivyo, mfumo wenye kutumia Viwango
vya Ufaulu vinavyobadilika (Flexible Grade Ranges) na Viwango vya
Ufaulu visivyobadilika (Fixed Grade Ranges) hutumika zaidi
ikilinganishwa na mifumo mingine. Upangaji wa viwango katika Nchi
zinazotumia mfumo wa viwango vinavyobadilika hutegemea jinsi
watahiniwa walivyofaulu somo husika. Katika mfumo huo, viwango vya
ufaulu huweza kutofautiana baina ya somo na somo na kati ya mwaka
mmoja na mwingine kwa sababu kiwango cha ufaulu hutofautiana baina
ya somo moja na jingine. Aidha, kwa nchi zinazotumia mfumo wa viwango
vya ufaulu visivyobadilika (Fixed Grade Ranges), viwango vya ufaulu
vinavyofanana hupangwa ili vitumike kama kipimo cha ufaulu kwa
masomo yote kwa kila mwaka.
Tanzania ilikuwa ikitumia mfumo wa viwango vya ufaulu vinavyobadilika
(Flexible Grade Ranges) kuanzia mwaka 1973 hadi 2011. Hata hivyo,
kuanzia Mtihani wa Kidato cha Nne 2012, Baraza la Mitihani la Tanzania
liliamua kuanza kutumia mfumo wa Viwango vya Ufaulu visivyobadilika
(Fixed Grade Ranges) kwa madhumuni ya kuwawezesha wadau kujua
viwango vya ufaulu vinavyotumika katika kutunuku matokeo ya Mitihani
ya Taifa.
      
Baraza la Mitihani limeandaa Mwongozo huu ili kuwawezesha wadau
mbalimbali wa elimu kufahamu viwango vya ufaulu vilivyoidhinishwa
kutumika katika Mitihani ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. Aidha,
mwongozo huu umebainisha utaratibu unaotumika katika kutunuku
matokeo ya mitihani hiyo kwa lengo la kuwawezesha wadau wa elimu
kuongeza chachu katika ufundishaji na ujifunzaji ili kufikia viwango vya
juu vya ufaulu vilivyobainishwa na Baraza la Mitihani la Tanzania.
Sehemu ya pili ya Mwongozo huu inafafanua malengo ya Mitihani ya
Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. Aidha, sehemu ya tatu inafafanua
utaratibu wa kutunuku viwango vya ufaulu
na sehemu ya nne ni
hitimisho.
2     
            
2.0
MALENGO YA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE (CSEE) NA KIDATO
CHA SITA (ACSEE)
Malengo ya Mitihani wa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita ni kupima
maarifa, ujuzi na stadi alizopata mtahiniwa za kumwezesha kumudu
mahitaji ya sayansi na teknolojia katika kujitegemea, ikiwa ni pamoja na
kutimiza mahitaji ya
matakwa ya jamii pamoja na mazingira
yanayomzunguka. Aidha, matokeo ya mitihani hii huwezesha mamlaka
mbalimbali za elimu kuchagua watahiniwa kuendelea na masomo katika
ngazi inayofuata ikiwa ni pamoja na elimu ya juu na fani mbalimbali za
masomo ya Utalaamu wa Kazi.
Ili kupata maarifa na ujuzi unaotakiwa katika ngazi ya Kidato cha Nne,
mtahiniwa wa shule (school candidate) anatakiwa kufanya masomo
yasiyopungua saba na yasiyozidi kumi. Kwa upande wa Kidato cha Sita,
mtahiniwa anatakiwa kufanya masomo yasiyopungua manne ambayo
miongoni mwake yapo masomo matatu ya tahasusi. Mtahiniwa wa
Kujitegemea wa Kidato cha Nne anayefanya mtihani kwa mara ya kwanza
anatakiwa kufanya masomo yasiyopungua matatu. Aidha, kwa mtaihiniwa
wa kidato cha sita anayefanya mtihani kwa mara ya kwanza anatakiwa
kufanya masomo yasiyopungua mawili likiwemo somo la General Studies.
3.0 VIWANGO VYA UFAULU NA UTARATIBU WA KUTUNUKU
3.1 Viwango vya Ufaulu
Katika kutunuku vyeti, Baraza hutumia gredi A, B+, B, C, D, E na F ili
kupambanua ufaulu kwa kila mtahiniwa katika Mitihani ya Kidato cha Nne
na Kidato cha Sita. Mchanganuo wa Viwango vya ufaulu vinavyotumika ni
kama inavyoonekana katika Jedwali la 1.
3     
            
Jedwali la 1: Viwango vya Ufaulu katika CSEE na ACSEE
Gredi
A
B+
B
C
D
E
F
Mfiko wa
Alama
75-100
60-74
50-59
40-49
30-39
20-29
0-19
Maelezo
Bora sana (Excellent)
Vizuri sana (Very Good)
Vizuri (Good)
Wastani (Average)
Inaridhisha (Satisfactory)
Hairidhishi (Unsatisfactory)
Feli (Fail)
Mtahiniwa atahesabiwa kuwa amefaulu somo endapo atakuwa amepata
angalau gredi D (alama 30) katika somo husika. Hivyo, kiwango cha juu
cha ufaulu katika somo ni Gredi A ambapo kiwango cha chini cha ufaulu
(Pass) katika somo ni Gredi D. Ufaulu katika Gredi A, B+, B na C utakuwa
ni “Credit Pass” kwa CSEE ambapo kwa ACSEE itakuwa ni “Principal
Pass”.
3.2
Matumizi ya Alama Endelevu (CA) katika Alama ya Mwisho
Wakati wa kupanga viwango vya ufaulu kama ilivyoainishwa katika
Jedwali la 1, uwiano wa alama 30:70 hutumika kukokotoa Alama ya
Mwisho (Final Score); ambapo asilimia 30 ni mchango wa Alama
Endelevu (CA) na asilimia 70 ni mchango wa Alama za Mtihani wa Taifa
(FE). Katika Mtihani wa Kidato cha Nne 2013 na Kidato cha Sita 2014
mchanganuo wa alama 30 za CA ni kama inavyoonekana katika Jedwali
la 2 na 3.
Jedwali la 2: Mchanganuo wa CA katika CSEE
Na.
1
2
3
4
5
Aina ya Mtihani
Mtihani wa Taifa Kidato cha Pili
Matokeo ya Mtihani wa Kidato
cha Tatu – Muhula I
Matokeo ya Mtihani wa Kidato
cha Tatu – Muhula II
Matokeo ya Mtihani wa Kidato
cha Nne – Muhula I
Kazi Mradi / Project
Jumla
4     
     
Alama
15
10
5
30     
Jedwali la. 3: Mchanganuo wa CA katika ACSEE
     
        Na.
     1
        2
        3
     
Aina ya Mtihani
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha
Tano Muhula wa I na II
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha
Sita Muhula wa I
Kazi Mradi / Project
Jumla
Alama
15
10
5
30
Hata hivyo, kuanzia Mtihani wa Kidato cha Nne 2014 na Kidato cha Sita
2015, mchango wa CA wa alama 30 utapatikana kutokana na mitihani
mbalimbali kama ilivyoaninishwa katika Jedwali la 4 na 5.
Jedwali la. 4: Mchanganuo wa CA katika CSEE
Na.
1
2
3
4
5
Aina ya Mtihani
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha
Tatu – Muhula I
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha
Tatu – Muhula II
Matokeo ya Mtihani Mock wa
Kidato cha Nne
Kazi Mradi / Project
Jumla
Alama
10
05
10
5
30
Jedwali la 5: Mchanganuo wa CA katika ACSEE
     
Na.
1
2
3
Aina ya Mtihani
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha
Tano Muhula wa I na II
Matokeo ya Mtihani wa Mock
Kidato cha Sita
Kazi Mradi / Project
Jumla
Alama
15
10
5
30
Muhimu: Katika somo ambalo mtahiniwa hakufanyia Kazi Mradi, alama
za matokeo ya Mitihani ya Mock ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita
itachangia alama 15 badala ya 10 zilizoainishwa katika Jedwali la 4 na 5..     
5     
            
3.3
Utaratibu wa Kutunuku Alama ya Mwisho (Final Score)
Ili kupata Alama ya Mwisho (Final Score), Baraza la Mitihani hukokotoa
Alama ya Mwisho kwa kutumia kanuni ifuatayo:
CFM =
∂1*FEcm + ∂2*CAcm
     
Ambapo;
CFM
∂1
∂2
FEcm
CAcm
- Alama ya Mwisho ya Mtahiniwa
- Uwiano wa Alama katika FE
- Uwiano wa Alama katika CA
- Alama ya Mtahiniwa katika FE (Candidate’s Mark)
- Alama ya Mtahiniwa katika CA (Candidate’s Mark)
Mfano: Iwapo katika somo la Geography mtahiniwa amepata alama 13 katika
Mtihani wa Mwisho (Final Examination-FE) na Alama Endelevu zilizooneshwa
katika Jedwali lifuatalo:
Mitihani ya Darasani
Kidato cha Kidato Kidato cha III Kidato cha IV
II cha III Muhula Muhula wa 2 Muhula wa 1
   wa 1
89 92 93 95
Kazi Mradi
68
Ukokotoaji wa alama ya mwisho ya mtahiniwa huyu hufanywa kama ifuatavyo:
(a) Mchango wa Mtihani wa Kidato cha Pili katika CA ni
(15/30) x 89= 45.5
(b) Mchango wa Mitihani ya Kidato cha Tatu na Kidato cha Nne katika CA ni
(i) Wastani wa alama za Kidato cha Tatu na Kidato cha Nne ni
(92 +93+95)/3 = 93.3
6     
            
(ii)
Hivyo, mchango wa CA katika Kidato cha Tatu na Kidato cha
Nne ni (10/30)x93.3 = 31.1
(c) Mchango wa alama za Kazi-Mradi utakuwa ni 5/30x68 = 11.3
Hivyo jumla ya alama za CA
Kwa kutumia Kanuni CFM =
= 45.5 + 31.1 + 11.3
= 87.9
∂1*FEcm + ∂2*CAcm
na uwiano wa 30:70
Alama ya Mwisho (CFM) ya mtahiniwa huyu ni
CFM = 70/100x13 + 30/100x87.9 ambayo itakuwa ni 35.
Kwa Alama 35, mtahiniwa huyu atatunukiwa gredi D ya ufaulu katika somo la
Geography.
3.4
Madaraja ya Ufaulu
Baraza la Mitihani la Tanzania hupanga ufaulu katika madaraja
mbalimbali. Madaraja hayo hupangwa kwa kutumia mfumo wa Pointi au
mfumo wa Grade Point Average (GPA). Katika mfumo wa Pointi,
mtahiniwa wa Kidato cha Nne hukokotolewa idadi ya pointi zake
alizopata katika masomo saba aliyofanya vizuri na mtahiniwa wa Kidato
cha Sita hukokotolewa idadi ya pointi katika masomo matatu ya tahasusi
(combination) aliyojisajili. Katika mfumo wa GPA, jumla ya pointi alizopata
mtahiniwa wa Kidato cha Nne katika masomo saba aliyofanya vizuri
hugawanywa kwa saba Ili kupata wastani wa pointi alizopata mtahiniwa.
Aidha, kwa watahiniwa wa ACSEE idadi ya pointi walizopata katika
masomo ya tahasusi hugawanywa kwa tatu ili kupata wastani wa pointi
alizopata mtahiniwa katika masomo hayo.
3.4.1
Madaraja katika Mfumo wa Pointi
Madaraja katika mfumo wa pointi hupangwa kuanzia daraja la kwanza
hadi la nne yaani ‘Division One’, ‘Division Two’, ‘Division Three’ na
‘Division Four’ . Aidha, daraja la I-III hubainishwa kwa idadi ya pointi
alizopata mtahiniwa wakati daraja la nne hubainishwa kwa kutumia kigezo
cha mtahiniwa kufaulu angalau D mbili au angalau C moja au zaidi.
Mchanganuo wa madaraja ni kama ilivyoainishwa katika Jedwali la 6.
7     
            
Jedwali la 6: Muundo wa Madaraja kwa Kutumia Pointi (CSEE)
I
II
III
IV
O
POINTI/VIGEZO POINTI/VIGEZO
CSEE ACSEE
7 – 17 3–7
  18 – 24 8–9
    25 – 31 10- 13
      Awe na angalau D mbili au Credit Awe na angalau D mbili au Principal
      Pass moja isiyopungua C. Pass moja isiyopungua C.
Aliyepata ufaulu chini ya D mbili
DARAJA
Aliyepata ufaulu chini ya D mbili
Ambapo pointi kwa kila gredi ni kama ifuatavyo:
A = 1, B+ = 2, B = 3, C= 4, D = 5, E = 6 na F = 7
Mfano:
Kwa mtahiniwa wa CSEE aliyepata matokeo yaliyoainishwa hapa
chini atakuwa na idadi ya pointi katika masomo saba aliyofaulu
vizuri zaidi kama ilivyooneshwa katika Jedwali lifuatalo:
a)
SOMO
Civ.
GRADE
UZITO WA
GREDI
Hist.
A B+
1
Geog.
2
Kisw. English Phy. Chem. Biol. Maths B+ B C C C C E Pointi
2 3 4 4 4 4 6 20
Idadi ya Pointi alizopata katika masomo Saba aliyofanya
vizuri zaidi ni 1 + 2+ 2 + 3 + 4+ 4 + 4 = = 20
Hivyo, kwa Pointi 20, mtahiniwa anatunukiwa matokeo
yenye Division Two.
b)
Kwa mtahiniwa wa ACSEE aliyepata matokeo yaliyoainishwa
hapa chini atakuwa na idadi ya pointi katika masomo ya tahasusi
kama ilivyooneshwa katika Jedwali lifuatalo:
MASOMO
GRADE
UZITO WA
GREDI
Tahasusi (combination)
Ziada
Phy. Chem. Biol. BAM GS
E B+ A D A
6 2 1 5 1
Pointi
9
Idadi ya Pointi alizopata katika masomo ya tahasusi
(combination subjects) ni 6 + 2+ 1 = 9.
8     
            
Hivyo, kwa Pointi 9, mtahiniwa huyu hutunukiwa matokeo
yenye Division Two.
3.4.2
Madaraja katika Mfumo wa GPA
‘Grade Point Average’ (GPA) ni Mfumo wa Kutunuku ambao huonesha
wastani wa pointi alizopata mtahiniwa katika masomo aliyofaulu katika
mtihani wake. Madaraja katika mfumo wa GPA hupangwa katika utaratibu
wa Distinction, Merit, Credit na Pass ambapo daraja la Distinction ni la
ufaulu wa juu zaidi na daraja la Pass ni la ufaulu wa chini. Mtahiniwa
hutunukiwa Gredi A, B+, B, C, D, E au F kutegemeana na ufaulu wake
katika somo ambapo uzito wa alama katika gredi A = 5, B+ = 4, B = 3,
C=2, D = 1, E = 0.5 na F = 0. Mtahiniwa atahesabiwa kuwa amefaulu
somo endapo atapata Gredi D ambayo ni sawa na uzito wa Pointi 1.
Ukokotoaji wa jumla ya GPA ya mtahiniwa hufanyika kwa kuzingatia
masomo ambayo mtahiniwa amefaulu angalau kwa Gredi D na kuendelea
(D, C, B, B+ na A). GPA anayopata mtahiniwa hutokana na wastani wa
pointi alizopata katika masomo saba aliyofanya vizuri zaidi kwa Mtihani
wa Kidato cha Nne au masomo matatu ya tahasusi kwa Mtihani wa
Kidato cha Sita. Aidha, GPA ya mtahiniwa huandikwa katika nafasi moja
ya Desimali ambapo nafasi ya pili ya desimali hukadiriwa katika makumi
yaliyokaribu. Mfano, mtahiniwa mwenye GPA ya 3.15 itakuwa sawa na
3.2 na mtahiniwa mwenye GPA ya 3.14 itakuwa sawa na 3.1.
Muundo wa madaraja kwa kutumia GPA katika Mitihani ya Kidato cha
Nne na cha Sita ni kama ilivyoainishwa katika Jedwali la 7.
Jedwali la 7: Muundo wa Madaraja kwa Kutumia GPA
DARAJA CSEE ACSEE
Distinction 3.6-5.0 3.7-5.0
Merit 2.6-3.5 3.0-3.6
Credit 1.6-2.5 1.7-2.9
Pass 0.3-1.5 0.7-1.6
Fail 0.0-0.2 0.0-0.6
9     
            
3.4.3
Kanuni ya Ukokotaoji wa GPA
(a)
Kanuni inayotumika kukokotoa GPA ya mtahiniwa katika Mtihani
wa Kidato cha Nne ni
Ambapo
p = pointi za masomo saba ambayo mtahiniwa kafaulu
vizuri zaidi
n = idadi ya masomo saba ambayo mtahiniwa amefanya
vizuri zaidi.
Mfano, Ukokotoaji wa GPA kwa mtahiniwa wa CSEE aliyepata
matokeo yaliyoainishwa hapa chini ni kama ifuatavyo:
SOMO
GRADE
UZITO WA
GREDI
Civ. Hist.
A B+
5 4
Geog.
Kisw. English Phy. Chem. Biol. Maths
B+ B C C C C E
4 3 2 2 2 2 0.5
(i) Masomo saba ambayo mtahiniwa amefaulu vizuri ni
   Civics (A), History (B+), Geograpghy (B+), Kiswahili
  (B), English (C), Physics (C) na Chemistry (C)
 ambayo yana uzito wa alama 5, 4, 4, 3, 2, 2 na 2.
(ii) Wastani wa pointi (GPA) alizopata mtahiniwa katika
    masomo saba aliyofaulu vizuri ni (5 + 4 + 4 + 3 + 2 +
   2 + 2)/7 ambayo itakuwa 3.1. Hivyo, kwa GPA ya 3.1,
  mtahiniwa huyu hutunukiwa matokeo yenye Daraja la
 Merit.
(iii) Mtahiniwa aliyefanya masomo pungufu ya 07, ufaulu
     wake hautakokotolewa kwa kutumia GPA na badala
    yake atafaulu katika kiwango cha “Pass” endapo
       atapata angalau Gredi D mbili au C moja.
(b) Kanuni inayotumika kukokotoa GPA ya mtahiniwa katika Mtihani wa
Kidato cha Sita ni
Ambapo
p= pointi za masomo ya tahasusi (combination subjects)
10     
            
n = idadi ya masomo ya tahasusi (combination subjects)
Mfano, Ukokotoaji wa GPA kwa mtahiniwa wa ACSEE aliyepata
matokeo yaliyoainishwa hapa chini ni kama ifuatavyo:
Tahasusi (combination)
MASOMO
Ziada
Phy. BAM GS
B+ A D A
0.5
UZITO WA GREDI
Biol. E
GRADE
Chem. 4 5 1 5
(i) (ii) Wastani wa pointi (GPA) alizopata mtahiniwa
        utakuwa ni (5 + 4)/3 ambayo ni 3.0. Hivyo, kwa GPA
       ya 3.0, mtahiniwa huyu hutunukiwa matokeo yenye
      Daraja la Merit.
(iii)
4.0
Katika masomo matatu ya tahasusi (combination
subjects) ambayo mtahiniwa ameyafanya amefaulu
katika masomo mawili ambayo ni Biology (A) na
Chemistry (B+) yenye uzito wa alama 5 na 4.
Mtahiniwa amepata Gredi E katika somo la Physics
ambalo halitajumuishwa katika GPA kwa kuwa
hakulifaulu.
Mtahiniwa aliyefanya masomo pungufu ya 03, ufaulu
wake hautakokotolewa kwa kutumia GPA na badala
yake atafaulu katika kiwango cha “Pass” endapo
   atapata angalau Gredi D mbili au C moja.
HITIMISHO
Baraza la Mitihani limeandaa Mwongozo huu ili kuwawezesha wadau
kujua viwango vya ufaulu vinavyotumika pamoja na utaratibu wa matumizi
ya Alama Endelevu (CA) katika kutunuku matokeo ya Mitihani ya Kidato
cha Nne (CSEE) na Kidato cha Sita (ACSEE).
Baraza la Mitihani la Tanzania linaamini kuwa Mwongozo huu utakuwa
ni chachu kwa Wadau wa Elimu hususan Walimu na Wanafunzi ya
kuongeza bidii katika ufundishaji na ujifunzaji ili kufikia viwango vya juu
vya ufaulu vilivyoainishwa.
11      

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger