Kujamiana (ama tendo la ndoa) ni moja ya mambo muhimu sana
katika maisha ya mwanadamu. Ni ukweli usiofichika kwamba wengi wetu tungependa kuwa na mwenza ambaye mnaridhishana katika tendo la ndoa. Si hivyo tu, bali tendo hili huleta maelewano katika uhusiano wowote ule.
Lakini, kuna faida zozote za kiafya za kufanya tendo hili? Ndiyo! Zipo faida kadhaa zinazotokana na kujamiana. Katika makala hii, mwandishi wako Dk. Khamis Hassan anajaribu kutueleza faida za kujamiana kiafya kama ambavyo imewahi kuonekana katika tafiti kadhaa zilizofanyika sehemu mbalimbali duniani.

1.
Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo: Wanawake ambao hufika kilele
(orgasm) angalau mara mbili kwa wiki kila wanapojamiana, wana uwezekano
mdogo sana (30% tu) wa kupata maradhi ya moyo tofauti na wale wasiofikia
kilele.
Hii ni kwa vile homoni ya endorphin inayotolewa wakati wa kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na hivyo kumuepusha mtu na magonjwa wa moyo. Aidha kujamiana angalau mara tatu kwa wiki, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo (heart attack) na kiharusi.
Uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo wakati wa kufanya mapenzi ni mdogo sana, ni asilimia 1 tu ya vifo vyote vinavyotokana na mshtuko wa moyo ndivyo uhusishwa na kujamiana.
Aidha, sababu nyingine inayoongeza uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa ambapo huchangia karibu asilimia 75 ya vifo vinavyotokana na kujamiana, na karibu asilimia 90 ya vifo hivi hutokea kwa wanaume wazee.
Uwezekano wa kupata shambulio la moyo wakati wa kujamiana huongezeka ikiwa mtu ana miaka zaidi ya 50, uzito uliopitiliza na matatizo ya afya. Hii ni sawa na kusema unaanza kufanya mazoezi mazito kwa ghafla wakati mwili na umri haviruhusu.

2.
Huongeza ukakamavu wa mifupa: Wanawake waliokoma kupata hedhi
(menopausal women) ambao pia hujamiana angalau mara mbili kwa wiki wana
kiwango kikubwa cha homoni ya oestrogen mara mbili zaidi ya wale ambao
hawajamiani.
Homoni hii husaidia kulinda mifupa na kwa wanawake waliokoma kupata hedhi wakosapo homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa ujulikanao kama osteoporosis.
Homoni hii husaidia kulinda mifupa na kwa wanawake waliokoma kupata hedhi wakosapo homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa ujulikanao kama osteoporosis.
3.Hupunguza
msongo wa mawazo: Kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na shinikizo la
damu na humfanya mtu kupata usingizi mnono. Kufikia kilele ni sawa na
kunywa 2-3mg za dawa ya diazepam (kumbuka diazepam hufanya mwili
kupumzika, muscle relaxant), na hii ndiyo sababu kuu ya kwa nini watu
hupata usingizi mzito baada ya kujamiana.
Watu wanaojamiana huweza kuhimili vizuri msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawafanyi hivyo. Aidha watu wanaojamiana huwa na kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu kuliko wale wasiojamiana.
Pia kuwepo kwa viasili vyaprostaglandins katika shahawa husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Viasili hivi hunyonywa na sehemu za siri za mwanamke. Shahawa pia zina madini ya zinc, calcium, potassium, fructose na protini ambavyo vyote ni muhimu kwa afya njema.

4.
Hupunguza maumivu: Kufikia kilele (orgasm) wakati wa kujamiana ni tiba
ya maumivu. Homoni ya Oxytocin inayotolewa kwa wingi kabla na wakati wa
kujamiana pamoja na viasili vya endorphins hupunguza maumivu ya kichwa,
mgongo, kipandauso, baridi yabisi pamoja na dalili zinazotokea baada ya
kukoma hedhi (post menopausal syndrome symptom).
5.
Hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume:
Wanaume walio na umri wa miaka 50 na zaidi na ambao hujamiana mara kwa
mara wana uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume (prostate
cancer) hali inayotokana na kusafisha tezi dume mara kwa mara wakati wa
kujamiana.
Aidha kutoa shahawa wakati wa kujamiana mara 21 au zaidi kwa mwezi kunahusishwa na uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume wenye umri mkubwa ikilinganishwa na kutoa shahawa mara 4 mpaka 7 kwa mwezi.

6.
Huongeza uwezo wa kunusa: Baada ya kujamiana, kiwango cha homoni ya
prolactin huongezeka, ambayo hufanya seli za ubongo (brain stem cells)
kutengeneza seli mpya katika sehemu inayohusika kunusa na kutambua
harufu (brain olfactory bulb).
7.
Hupunguza uzito na kumfanya mtu kuwa na afya njema: Kujamiana ni
mazoezi mazuri. Wakati wa kujamiana, mapigo ya moyo huongezeka kutoka
wastani 70/dakika mpaka 150/dakika ambayo ni sawa na mtu anayefanya
mazoezi kwa kiwango cha juu. Kujamiana huchoma karibu 200 calories sawa
na kukimbia dakika 15 katika mashine ya tredmill. Mwanamke anayefika
kilele huchoma calories 47 zaidi.
8.
Huongeza kinga ya mwili: Kufanya mapenzi mara moja au mara mbili kwa
wiki huongeza kiwango cha seli za kinga aina ya immunoglobulin A kwa
robo tatu, na hivyo kumkinga mtu dhidi ya mafua na magonjwa mbalimbali.
9.
Kufanya mapenzi huongeza urembo wa mwanamke: Wanawake wanaojamiana
angalau mara nne kwa wiki huonekana kuwa na umri mdogo ikilinganishwa na
umri wao kwa miaka 7 mpaka 12, hii inatokana na ukweli kuwa kujamiana
huongeza homoni ya oestrogen ambayo hufanya nywele za wanawake kuwa na
afya nzuri na ngozi zao kung’aa.
10.
Hudhibiti mzunguko wa hedhi kuwa wa kawaida: Wanawake ambao hujamiana
angalau mara moja kwa wiki (isipokuwa siku ambazo wako kwenye hedhi)
huwa na mzunguko wa hedhi wa kawaida ikilinganishwa na wale ambao
hufanya mapenzi kwa nadra au wale ambao hawafanyi kabisa
11.
Tendo la ndoa huongeza hali ya kujiamini: Ikiwa litafanyika baina ya
wapendao, na tendo lenyewe likawa la furaha na upendo, kujamiana
huongeza kujiamini.
12.
Huongeza ukakamavu katika misuli ya nyonga (pelvic floor muscles): na
hivyo kuzuia mwanamke kupata matatizo ya mkojo au ugonjwa wa kibofu cha
mkojo. Wanawake ambao wamekoma kupata hedhi, kufanya mapenzi mara kwa
mara huondoa tatizo la kusinyaa kwa sehemu za siri za mwanamke (vagina
atrophy) na hivyo kumwepusha na maambukizi katika njia cha mkojo
(Urinary Tract Infection ).
13.
Kufanya mapenzi huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini: Unapojamiana
na kufikia kilele, mzunguko wa damu huongezeka maradufu, hivyo kuongeza
mzunguko wa hewa aina ya oksijeni kwenda kwenye viungo muhimu kama
moyo, ubongo na figo hivyo kusaidia kuondoa uchafu na sumu mbalimbali
mwilini.
14.
Huongeza hali ya kujithamini au kuthamini mwili wako: Hakuna kitu
kizuri kama mtu kutambua ana maumbile mazuri na ya kuvutia, haya yote
hupatikana wakati mtu yupo uchi wakati wa kujamiana na mwenza wake
kumwambia kwamba ana maumbile mazuri na ya kuvutia, hii huongeza hali ya
kujithamini na kujipenda kwa binadamu yoyote.
15.
Husaidia kuishi kwa muda mrefu: Kufanya mapenzi angalau mara mbili kwa
wiki hurefusha maisha yako. Kila unapofikia kilele, homoni aina ya DHEA
(Dihydroepiandrosterone) hutolewa kwa wingi kutokana na raha ya tendo na
kufikia kilele.
DHEA huongeza kinga ya mwili, hurekebisha tishu zilizoharibika (hutibu vidonda), huongeza kiwango cha ufanyaji kazi cha ubongo, huiweka ngozi kuwa na afya bora na hupunguza msongo wa mawazo. Kwa hiyo, kuongeza kufikia kilele kuna uwezekano wa kurefusha maisha yako.

16.
Kujamiana huongeza upendo na msisimko katika mapenzi, kutokana na
kuongezeka kwa homoni ya oxytocin (love hormone), ambayo huleta
mshikamano, uaminifu, na unyenyekevu katika uhusiano au kwenye ndoa.
17.
Huongeza uwezo wa kuzaa au kutunga mimba: Mara nyingi watu huuliza kama
urefu wa uume una uhusiano wowote na uwezo wa kutunga mimba.
Jibu zuri ni hapana! Kufanya mapenzi mara kwa mara huboresha shahawa za mwanamume, huzifanya kuwa katika kiwango kizuri, na kama unataka kupata mtoto, ni bora kufanya mapenzi mara kwa mara sio kutumia shahawa zilizokaa kwa muda wa siku nne.

0 comments:
Post a Comment