Ripota
wa nguvu Simon Simalenga akiwa 104.4 Dodoma amekutana na Wanachuo
kwenye chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo kwenye bunge la bajeti
linaloendelea May 19 2014 Wabunge walipitisha bajeti ya wizara ya elimu
na mafunzo ya ufundi ambayo ni Bilioni 799.2
Ndani
ya saa 24 toka kupitishwa kwa bajeti hiyo taarifa zinapatikana kwamba
kuna uwezekano wa kutokea maandamano ya Wanachuo wa chuo kikuu cha
Dodoma (UDOM) kuelekea bungeni kama hawatopata fedha zao za kujikimu
ambazo wamecheleweshewa kwenye collage yao ya Humanities.
Wanasema
‘hatujazungumza hivi sababu tumepanic, kikawaida chuoni tunatakiwa
kusaini boom kila baada ya siku 56 ambazo ziliisha 26 April 2014 na
mpaka hatujapata taarifa yoyote toka wakati huo kwamba kuna shida gani
imetokea’
Mwajuma
Ally ambae ni Mwanachuo wa UDOM pia amesema ‘niko mwaka wa pili,
tunashindwa kuelewa kwa nini hili tatizo limetokea mpaka sasa hivi
inaonekana sisi tunadharaulika manake hii ni mara ya pili inatokea
humanities lakini vyuo vingine wamepewa mikopo’
Wengine
wanasema ‘Wanaume wenyewe sisi wapiganaji mpaka sasa tunaumia… watoto
wa kike je?’ Mwananchuo mwingine aitwae Upendo amesema ‘hii kashfa ya
watoto wa kike kujiuza kwa Wabunge ni ya kweli kwa sababu boom
likichelewa ni bora nikakae maeneo ya bungeni kwa sababu nikimuelezea
Mbunge nina shida nitalala nae atanipa hela’
‘Ndio
maana Wasichana wengi tunapenda kujiuza, sio kwamba tunapenda kufanya
makusudi ila ni kwa sababu tunacheleweshewa hela na maeneo ya bungeni
ndio tunapendelea kwenda kwa sababu tunajua kule ndio kuna mpunga mwingi
kuliko sehemu nyingine’
Kwenye
ofisi za utawala za chuo hicho Profesa Mbunda akatoa ufafanuzi kwa
kusema ‘kifupi ni kwamba management ya chuo kikuu inafatilia hilo swala,
afisa wake wa juu kabisa wa mambo ya pesa yuko Dar es salaam na
ameahidiwa katika siku tatu hili swala litakua limetatuliwa kwa hiyo
tunaomba Wanachuo wetu wavumilie kwa siku tatu’.
0 comments:
Post a Comment