KUITWA KAZINI 17 Mei, 2014
Sekretarieti ya
Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwataarifu waombaji kazi wa
nafasi mbalimbali waliofanya usaili kuanzia tarehe 04 hadi 30 Machi,
2014 ambao baadhi ya wasailiwa waliofaulu usaili husika mchakato wa
kuwapangiwa vituo vya kazi ulikuwa unakamilishwa. Orodha ya majina yao
ni kama yanavyoonekana katika Tangazo hili.
Aidha, wanatakiwa
kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa katika muda ambao
umeainishwa kwenye barua zao za kupangiwa vituo vya kazi wakiwa na vyeti
halisi (Originals Certificates) vya masomo kuanzia kidato cha nne na
kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.
Barua za
kuwapangia vituo vya kazi zimetumwa kupitia anuani zao. Aidha, wale
ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa
hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba mara
nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa tena.
Kufungua majina na sehemu uliyopangwa BOFYA HAPA(pdf)
0 comments:
Post a Comment