Katibu
Tawala wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Festo Chonya wa pili kulia akimkabidhi
Mwenge wa Uhuru Katibu Tawala wa Wilaya ya Kalambo Bi. Mapinduzi
Severian mara baada ya kumaliza mbio zake wilayani Nkasi mapema leo
asubuhi tarehe 22 Mei, 2014.
Mratibu
wa Mwenge Mkoa wa Rukwa Ndugu Abuubakar Serungwe kulia akitoa neno la
shukurani kwa uongozi wa Wilaya ya Nkasi kwa ushirikiano walioutoa
wakati Mwenge huo upo Wilayani humo.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Festo Chonya wa pili kulia akimkabidhi
Mwenge wa Uhuru Katibu Tawala wa Wilaya ya Kalambo Bi. Mapinduzi
Severian mara baada ya kumaliza mbio zake wilayani Nkasi mapema leo
asubuhi tarehe 22 Mei, 2014.
Mratibu
wa Mwenge Mkoa wa Rukwa Ndugu Abuubakar Serungwe kulia akitoa neno la
shukurani kwa uongozi wa Wilaya ya Nkasi kwa ushirikiano walioutoa
wakati Mwenge huo upo Wilayani humo.
Kiongozi
wa mbio za Mwenge kitaifa Bi. Rachel Kassanda akizindua rasmi wodi ya
wazazi ya Samazi mwambao wa Ziwa Tanganyika Wilayani Kalambo leo tarehe 22 Mei, 2014. Kulia anayeshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Iddi Hassan Kimanta.
Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu
Iddi Kimanta akitoa maelezo mafupi kuhusu kitanda cha kujifunguliza
wazazi kwa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Bi. Rachel Kassanda baada
kuzindua wodi hiyo ya wazazi ya Samazi mwambao mwa ziwa Tanganyika
Mkoani Rukwa.
Sehemu
ya wananchi wengi wa Kijiji cha Samazi mwambao mwa ziwa Tanganyika
Mkoani Rukwa walikusanyika kushuhudia ujio wa Mwenge wa Uhuru kijijini
hapo.
Kwa
wale waliokosa pa kukaa walilazimika kupanda miti na kuhatarisha maisha
yao ili wapate fursa ya kupata taswira iliyo mwanana ya Mwenge wa Uhuru.
Ndugu Enock Nguvumali Mwenyekiti wa Umoja wa Wafugaji Nyuki Kijiji cha Kisumba akishika Mwenge wa Uhuru leo tarehe
22 Mei, 2014. Mapema kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Bi.
Rachel Kassanda alizindua mradi wa kutundika mizinga ya kisasa ya nyuki
katika Kijiji cha hicho.
Wadau
wa Mwenge wa Uhuru ambao pia ni wakuu wa idara katika Wilaya Kalambo
Ndugu Mirunga (kushoto) na Maholani wakijadili jambo muda mfupi kabla ya
kusomwa Risala ya Utii ya Mwenge wa Uhuru kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Wilayani Kalambo.- Na Hamza Temba Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
0 comments:
Post a Comment