Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni jana ilimlipua mbunge kutoka kambi yao, Zitto
Kabwe ikimhusisha na ufisadi wa Sh119 milioni kutoka Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).
Hii ni
mara ya kwanza kwa kambi ya upinzani kumhusiaha mbunge 'mwenzao' na
tuhuma za ufisadi tofauti na kawaida yao ya 'kuwashughulikia' ubadhirifu
katika Serikali.
Zitto,
mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chadema na ambaye pia ni
mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), anadaiwa
kuchota fedha hizo kupitia kampuni ya Leka Dutigite ambayo ina hisa
nyingi katika kampuni nyingine ya Gombe Advisors Limited ambayo Zitto ni
mkurugenzi wake.
Akiwasilisha
maoni ya upinzani bungeni jana kuhusu makadirio na matumizi ya Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mwaka 2014/15, waziri kivuli wa
wizara hiyo, Joseph Mbilinyi alisema Zitto hakutakiwa kuchota fedha hizo
kwa kuwa anabanwa na sheria ya maadili ya viongozi wa umma.
Alisema
Zitto, ambaye katika miezi ya karibuni aliingia kwenye mgogoro na
uongozi wa chama chake, ni mwenyekiti wa PAC, kamati ambayo jukumu lake
ni kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha
za umma katika wizara na mashirika ya umma, yakiwamo Tanapa na NSSF,
hivyo kulikuwa na mgongano wa kimasilahi katika suala hilo.
Tuhuma za Zitto
Katika
hotuba yake, Mbilinyi alisema taarifa za kibenki ambazo kambi hiyo
imezipata zinaonyesha kuwa Desemba 10, 2012, Hifadhi ya Taifa ya Saadani
ilihamisha Sh12 milioni kwenda katika akaunti ya kampuni ya Leka
Dutigite.
"Siku
moja baadaye fedha hizo zilitolewa kwa pesa taslimu kutoka kwenye
akaunti hiyo. Januari 14 na Februari 7, 2013 akaunti ya Leka Dutigite
iliingiziwa Sh28.6 milioni," alisema Mbilinyi.
Sugu alisema fedha hizo ziliingizwa na mtu aitwaye Mchange na kwamba ilipofika Februari 7 zote zilikuwa zimetolewa.
Alisema
Februari 28 mwaka jana, akaunti ya Leka Dutigite iliingiziwa Sh32.3
milioni kutoka NSSF na kwamba siku hiyo hiyo fedha hizo zilitolewa
kwenye akaunti hiyo. Siku nne baadaye shirika hilo lilifanya malipo
mengine kwenye akaunti ya Leka Dutigite.
"Ziliingizwa
Sh46.6 milioni ambazo zilitolewa kutoka kwenye akaunti hiyo kwa mikupuo
miwili. Katika kipindi cha miezi mitatu, kati ya Desemba 10, 2012 na
Machi 4, 2013 kampuni hiyo (ya Zitto) ililipwa Sh119.9 milioni kwa
utaratibu huohuo wa ingiza-toa fasta," alisema Mbilinyi.
Alisema kati ya fedha hizo Sh12.2 milioni zililipwa na Tanapa na Sh79 milioni zililipwa na NSSF.
CHANZO:MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment