MAJANGA! Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na muigizaji Adam Haji ‘Baba Haji’ nusura wazichape baada ya kupishana kauli.
‘Uwanja wa vita’ ulikuwa ni kwenye msiba
wa mwigizaji mwenzao Sheila Haule ‘Recho’, Sinza-Palestina, jijini Dar
ambapo chanzo kilishuhudia mtiti huo, kilidai tatizo liliibuka mara
baada ya Steve Nyerere kumchimba mkwara Baba Haji asijiweke karibu na
Jacob Steven ‘JB’.
Muigizaji mkongwe wa Bongo Muvi, Adam Haji ‘Baba Haji’ (kushoto) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu Recho.
“Hata haikujulikana kwa nini Steve
hakutaka Baba Haji awe karibu na JB, akammaindi ndipo mtiti ulipoibuka,
wakataka kushikana mashati bahati nzuri Mtitu (William) akawaamua,”
kilieleza chanzo.
Akizungumzia sakata hilo baada ya kutulizwa ‘munkari’, Baba Haji alisema anamshangaa Steve kwa kumchimba mkwara asikae na JB pasipo kuwa na sababu za msingi.
Akizungumzia sakata hilo baada ya kutulizwa ‘munkari’, Baba Haji alisema anamshangaa Steve kwa kumchimba mkwara asikae na JB pasipo kuwa na sababu za msingi.
0 comments:
Post a Comment