MSANII wa
filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel amesema hivi karibuni aligongana uso
kwa uso na Ivon Bigilwa ambaye anadaiwa kumchana kwa chupa mkononi na
kesi hiyo inaendelea katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Aunty alisema hayo juzi Jumatatu katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mbele ya hakimu
Agustina Mbando, akikanusha taarifa ya wadhamini wa Ivon, Christopher
Mwaseba na Anthon Mwaseba walioiambia mahakama kuwa mtuhumiwa alikuwa
nyumbani akimuuguza mama yake.
Msanii huyo alisema wadhamini hao
wanaidanganya mahakama kwa kuwa hivi karibuni alikuwa nchini China na
aligongana naye uso kwa uso.
0 comments:
Post a Comment