Msichana mmoja aliyetajwa kwa jina la Halima aliyedaiwa kuwa ni mchumba wa mtu, hivi karibuni alipata aibu ya aina yake baada ya kukutwa amezimika barabarani.
Tukio hilo lilitokea juzikati maeneo ya Kijitonyama jijini Dar ambapo ilidaiwa kuwa, binti huyo akiwa amevalia kimini alishuka kwenye Bajaj na kwenda kwenye hoteli iliyopo maeneo hayo bila kujulikana alikotokea.
Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Stella alisema: “Huyu dada namjua, ana mchumba wake waliwahi kufika dukani kwangu kufanya ‘shopping’. Leo asubuhi alikuja hapa na kuuliza kama atapata maziwa, alikuwa amevaa kihasara, wakati tunaendelea kuongea naye, akaanza kulegea na kuanguka.
“Hatukujua kilichomfanya akose nguvu ila alionekana kama kalewa ndipo tulipomchukua na kumsitiri kwa kanga, ni kama saa moja sasa limepita hajazinduka.”
Waandishi wetu walipofika eneo la tukio walimkuta binti huyo akiwa hajitambui na alipomwagiwa maji ya baridi alizinduka na kusema; “hapa niko wapi, nimeaibika!”
Hata hivyo, wakati akijitahidi kuamka, alianguka tena na kuzimika hadi Polisi wa Kituo cha Mabatini walipofika na kumchukua kwenye gari lao aina ya Toyota Noah ambapo inadaiwa alipofika huko alizinduka tena na akawa chini ya uangalizi wa polisi kwa saa kadhaa.
0 comments:
Post a Comment