Thursday, 29 May 2014

HOFU YATANDA WASAMARIA WEMA WAINGIA MITINI DHAMANA YA WAZAZI WA MTOTO WA BOKSI

...
HATIMAYE wale watuhumiwa wa mtoto anayedaiwa kufichwa kwenye boksi kwa miaka 4 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro kujibu mashitaka ya kula njama na kufanya ukatili dhidi ya mtoto Nasra huku watu waliotakiwa kuwawekea dhamana watuhumiwa hao wakiingia mitini.

Baba wa mtoto Nasra anayedaiwa kufichwa kwenye boksi kwa miaka minne Mtonga Omarafikishwa mahakamani
Watuhumiwa waliofikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi ni Rashid Mvungi (47), mama mlezi, Mariam Said (38) na mume wake Mtonga Omar (30).
Washitakiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mary Moyo, Jumatatu ya wiki hii  na kusomewa mashitaka hayo huku muda mwingi wakionesha kujutia kosa hilo ambalo hawakujua kama ni bomu ambalo litakuja kulipuka.
Muda mwingi, Mvungi akiwa mahakamani hapo alikuwa akiweka mikono juu ya kichwa (angalia picha) jambo lililotafsiriwa kwamba ni kuonesha kujutia tukio hilo.
Watuhumiwa wengine kwenye sakata hilo wakisindikizwa mahabusu chini ya ulinzi wa polisi
Wakili wa Serikali, Sunday Hyera alisema washitakiwa walitenda kosa hilo kati ya Desemba, mwaka 2010 na Mei, mwaka huu katika Mtaa wa Azimio Kata ya Kiwanja cha Ndege, mjini Morogoro.
Wakili huyo alidai kuwa katika kipindi hicho, washitakiwa wakiwa walezi wa mtoto Nasra, walimfanyia ukatili wa kumtelekeza na kumpa malezi akiwa ndani ya boksi na hivyo kumsababishia magonjwa mbalimbali.
Maradhi yaliyotajwa kumkumba mtoto huyo akiwa ndani ya boksi ni utapiamlo, maumivu ya kifua na mvunjiko wa mifupa katika mwili.
Hyera alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama kutaja tarehe ya kuisikiliza.
Hata hivyo, licha ya dhamana kuwa wazi, hakuna mtu aliyejitokeza kuwadhamini washitakiwa hao hivyo kurejeshwa gerezani huku watu wakishangilia kwa kusema kwamba kitendo walichokifanya hawastahili kurejea uraiani.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger