MAKUBWA! Baada
ya kujichora tatuu mbalimbali mwilini mwake, kuonesha amechizika
kimalovee, mwigizaji Lungi Maulanga amechora moja yenye sura ya mpenzi
wake ambaye hakutaka kumtaja.
Akipiga stori na mwanahabari wetu, Lungi
alisema kuwa ana tatuu 12 mwilini mwake ambazo alizichorea pande za
Dubai alipokuwa ameenda kutembea lakini mahaba niue ndiyo yalimtuma
achore hiyo yenye muonekano wa mchumba’ke.
“Tatuu zina maana lakini moja nimemchora
mpenzi wangu na hata nikikutana na mwanaume yeyote anajifanya
ananihitaji ajue kabisa ninaye nimpendae zaidi kwani tatuu hii siwezi
kuifuta,” alisema Lungi ambaye amechafuka tatuu katika maeneo mbalimbali
ikiwemo kwenye titi, paja na kiuno.
0 comments:
Post a Comment