AMA
kweli kifo kisikie kwa wengine kikikufika ndiyo utakijua kilivyo! Mama
mmoja aliyefahamika kwa jina la Ester Shaban (44) amejikuta akirudia
machungu ya kufiwa na mume wake kwa kufiwa na watoto wa kuwazaa kutokana
na kuumwa na mbwa.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, Ester alifika Kibamba-Kwembe, nje kidogo ya
Jiji la Dar na watoto wake watatu akitokea Kahama, Shinyanga ili
kupumzika kwa ndugu yake baada ya kufiwa na mume wake miezi kumi na nne
iliyopita.
Siku ya pili tangu afike watoto wake, Boniface Joseph (4) na Peter Joseph (6) waling’atwa na mbwa sehemu za usoni.
Tukio hilo lilitokea wakati mama yao amekwenda Makondeko, Dar na kuwaacha watoto hao nyumbani bila kuwepo kwa mtu mzima.
Chanzo
kilisema mwanamke huyo alirudi saa mbili usiku na kukutana na mkasa huo
wa watoto wake kung’atwa na mbwa, wakiwa na majeraha usoni.
“Mtoto
mmoja aliyeshuhudia tukio hilo alisema watoto hao ndugu waling’atwa
usoni na mbwa wa mzee mmoja ambaye hata yeye alimkimbiza mchana,”
kilisema chanzo hicho.
Naye
mama wa mtoto huyo akizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa masikitiko,
alisema: “Baada ya kukuta wanangu wamekumbwa na mkasa huo niliwachukua
mpaka kwa mwenye mbwa na kumweleza lakini akakataa kwamba si mbwa wake
japokuwa alionekana kuwa na kigugumizi cha hapa na pale.”
Akaongeza:
“Tulishauriana tuwapeleke Hospitali ya Tumbi (Kibaha) lakini yule mzee
aliyesemekana kuwa ndiye mwenye mbwa akasema yeye hana pesa za kukodi
gari labda tusubiri Jumatatu. Siku hiyo ilikuwa Jumamosi tena saa tatu
usiku.
“Nilipinga, ikabidi kesho yake (Jumapili) tuwapeleke hospitali ya binafsi ya Gati ambapo walichomwa sindano za tetenasi tu.
“Niliwauliza
madaktari kama sindano hizo zinatosha wakasema zinatosha kwani chanjo
niliyoipata mimi wakati wa ujauzito itawasaidia na watoto. Nilishangaa
kwa sababu nasikia mtu akiumwa na mbwa anachomwa sindano za kitovuni
lakini wanangu hawakufanyiwa hivyo.”
Mwanamke
huyo aliendelea kudai kuwa daktari alimtoa wasiwasi kwa kumwambia
vidonda hivyo vitapona asiwe na shaka. Akapewa dawa za kumeza watoto
wake na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Akasema: “Baada ya siku kadhaa, vidonda vilionekana kukauka kwa nje, Kumbe sikujua kwa ndani watoto wangu walikuwa wanaumia pasipo kufahamu. Siku chache mbele Peter akazidiwa.
Akasema: “Baada ya siku kadhaa, vidonda vilionekana kukauka kwa nje, Kumbe sikujua kwa ndani watoto wangu walikuwa wanaumia pasipo kufahamu. Siku chache mbele Peter akazidiwa.
Akawa anatapika damu na kubweka kama mbwa. Ila sikujua cha kufanya, kwa kuwa ilikuwa usiku nilivumilia.
“Ilipofika alifajiri ya saa 10 mwanangu alikata roho. Tulipeleka mwili kwenye mochwari ya Tumbi kwa ajili ya kuuhifadhi.
“Siku
iliyofuata tukiwa mochwari tunauchukua mwili, tulimsimulia daktari
ugonjwa uliomuua mwanangu akasema tumpeleke Boniface (mwanaye mwingine)
ili afanyiwe matibabu. Kumbe kule nyumbani Boniface naye alikuwa
amezidiwa na yuko njiani wanamleta hospitali. Alipofikishwa tu hakukaa
sana akafariki dunia,” alisema mwanamke huyo.
“Moyo
unaniuma sana ila sina namna zaidi ya kumshukuru Mungu kwa yote.
Nilikuja kupumzika na watoto wangu hapa baada ya kifo cha baba yao, sasa
siku nikirudi Kahama nitakuwa peke yangu,” alisema mama huyo na kuanza
kulia.
Mwanamke
huyo pia alisema anawaomba wasamaria wema wamsaidie kwa hali na mali
kwani kwa sasa ni mjane na anahitaji kurudi Kahama ili kupeleka msiba wa
watoto wake.
Kwa yeyote mwenye kuguswa na matatizo ya mama huyu anaweza kumsaidia kwa namba 0767 449758, jina litasoma Stella Shaban.
Kwa yeyote mwenye kuguswa na matatizo ya mama huyu anaweza kumsaidia kwa namba 0767 449758, jina litasoma Stella Shaban.
Marehemu hao walizikwa katika Makaburi ya Kibamba, Dar kwa kupishana siku moja. Mungu azilaze pema peponi roho zao. Amina.
0 comments:
Post a Comment