Haya
niliyapata kutoka kwa mshauri wa masuala ya mahusiano, ndoa na vijana
Frederick Kyara. Hizi ni baadhi tu nakuwekea hapa japo kuna vitu pia
wanawake hawavipendi kutoka kwa wenzi wao wanaume. Nayo ni haya hapa, ungana nami kujadili jambo hili ambalo kwangu nimeona ni changamoto au niseme sikujua.
1. Wanaume hawapendi kuambiwa cha kufanya na wenzi waoMwanamke
unapotaka mwanaume afanye jambo usimwambie alifanye bali fanya kama una
mpa ushauri. Kwamba John hivi kwa nini tusiweke balbu hapa kwenye
korido maana kuna giza kweli. Badala ya hivi wewe John huoni hapa kwenye
korido kuna giza balbu imeungua mwezi sasa hujabadilisha kwa nini? Weka
balbu bwana. Atafanya au asifanye kabisa kwa sababu umemwambia cha
kufanya.
2. Wanaume hawapendi mwenzi mwenye makelele, mlalamishiYeye
ni kulalamika kuanzia Jumatatu hadi Jumapili. Japo wanawake nao
wanasema kuna wanaume walalamishii balaaa. Na wenye gubu wanasusa kula
mpaka kuongea wanawanunia wake zao mmmmh!
3. Wanaume hawapendi mwenzi mchafu Mchafu wa mwili wake na hata nyumbani kwenye suala la kutunza nyumba wanayoishi. Uchafu hufanya mwanamke apoteze mvuto.
4. Wanaume hawapendi mwenzi mbishi Japo na wanawake wanasema wanaume ndio wabishi zaidi. Utampa mwanaume ushauri lakini haufanyii kazi ubishi mwingi.
5. Wanaume hawapendi kuamrishwa na mwenzi wao Mwenzi mbabe anaetoa amri na kumtawala hawataki.
6. Wanaume hawapendi kuhisiwa hisiwa na kusachiwa sachiwaKumpekua
kwenye simu, mifuko ya suruali kwamba unamulika mwizi. Hawapendi, tena
pengine hawajafanya jambo la kuwafanya wahisiwe vibaya.
0 comments:
Post a Comment