Nasikitika kwamba katika hali niliyonayo ya kumwuguza mama yangu naingizwa kwenye siasa za majitaka.
Kampuni ya LekaDutigite inamilikiwa na
wasanii. Gombe Advisors ni kampuni isiyofanya faida (Company limited by
guarantee) na haina maslahi yeyote ya kibiashara.
Wasanii wa Kigoma wamefanya kazi na TANAPA na NSSF, kazi ambazo zinajulikana na zipo.
Leo mpigie simu mfanyakazi yeyote wa
NSSF utasikia kazi ya wasanii hao. Kwa namna yeyote ile hii ni ishara ya
kukosa ubinaadam maana waliyoyasema wanajua sina faida yeyote ya
kifedha Leo wala kesho kwa LekaDutigite na Gombe Advisors.
Kipindi ambacho mama yangu yupo mahututi, tena mjumbe wa kamati kuu ya chama chao, pole ninayopewa ndio hiyo.
Hakuna namna ya kukosa ubinaadamu zaidi ya hivi.
By Zitto Kabwe
0 comments:
Post a Comment