Monday, 26 May 2014

NIKKI WA PILI: SIJAWAHI KUMTUNGIA NGOMA JOH MAKINI

...

UNAPOZUNGUMZIA makundi ya Hip Hop yanayofanya vizuri kwa sasa ni wazi utalitaja kundi moja maarufu kutoka pande za Arusha, Weusi.
Nickson Simon (Nikki wa Pili) baada ya kulonga na Global TV Online.
Kundi hilo linaongozwa na vichwa vitano vikiwemo, Isaac Waziri Makuto ‘Lord Eyez’, Nickson Simon (Nikki wa Pili), George Sixtus Mdemu (G Nako), John Simon (Joh Makini) na Bonta.
Jamaa wana ngoma nyingi ambazo zote zimeweza kushika chati ikiwa ni pamoja na ya sasa ya Gere, kuanzia ngoma hadi video wametisha.
Muongeaji mkuu wa kundi hilo, Nikki wa Pili ambaye juzikati alidondoka katika mjengo wa mastaa (Global Publishers).
Moja kwa moja akasimama mbele ya kamera za Runinga ya Global TV Online kwenye Kipindi cha Mtu Kati na kurushwa hewani kupitia mtandao namba moja Bongo wa www.globalpublishers.info
KIONGOZI WA WEUSI NI NANI?
Weusi haina uongozi isipokuwa ina majukumu. Kama mimi ni msemaji tu katika kundi. Ukiandaa shoo tegemea kuwasiliana na mmoja kati ya Weusi yaani mimi, Bonta, G Nako au Joh.
Hakutakuwa na shida kwa sababu kila mmoja anahusika kama Weusi.
Weusi wakifanya makamuzi wakati wa utoaji tuzo za Kili.
NI KWELI UNAMTUNGIA MISTARI YA KIINGEREZA JOH MAKINI?
Hapana, sijawahi kumtungia kwa sababu Joh Makini anaweza kutunga ngoma hata miye yeye ndiye mwalimu wangu tangu nimekua, amekuwa akinifundisha muziki mpaka nilivyo sasa.
LORD EYEZ MMEMTIMUA KWA AJILI YA MADAWA YA KULEVYA?
Hapana! Lord Eyez tumemsimamisha kazi kutokana na kukiuka kanuni za kundi na wala siyo kwa ajili ya madawa ya kulevya.
MIPANGO IPI IPO NDANI YA WEUSI KWA SASA?
Kwa sasa kila mmoja anatoa ngoma, nimeachia Sitaki Kazi, Joh Makini anakuja na mzigo wake mpya unaitwa See Me, G Nako naye anatoa ngoma yake sambamba na Bonta pia.
Mafansi wategemee shoo nyingi na video za kumwaga. Katikati ya mwezi wa kumi mashabiki wategemee ngoma nyingine kali kutoka kwa Weusi.
KWA NINI ULIIMBA NGOMA YA SITAKI KAZI?
Ni ngoma ya kuhamasisha watu kutengeneza ajira. Kwa Tanzania tatizo la ajira ni kubwa sana na limekuwa likiongezeka kila siku.
Lakini kama mtu atafikiri kujiajiri na kuajiri wengine, atakuwa amefikiria poa sana. Nafikiri nilijaribu kuchalenji idara nzima ya ajira kwa sababu ukifuatilia katika mawizara mengine yanafanya tofauti.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger