RB namba STK//RB/4457/2014 -KUTUMIA LUGHA YA MATUSI inawahusu wanandoa waliodumu kwa zaidi ya miaka 10, waliofunga ndoa kwa mbwembwe nyingi, Nyange na Ruth kisa kikielezwa kuwa ni ticha anayedaiwa kuvunja utatu huo mtakatifu, Ijumaa lina kisa na mkasa.
PAMOJA NA MBWEMBWE NYINGI... TICHA AVUNJA NDOA YA MTU
RB namba STK//RB/4457/2014 -KUTUMIA LUGHA YA MATUSI inawahusu wanandoa waliodumu kwa zaidi ya miaka 10, waliofunga ndoa kwa mbwembwe nyingi, Nyange na Ruth kisa kikielezwa kuwa ni ticha anayedaiwa kuvunja utatu huo mtakatifu, Ijumaa lina kisa na mkasa.
Habari zilieleza kwamba wahusika ni wakazi wa Pugu, Dar.
Kwa mujibu wa habari za mtaani wanakoishi wawili hao wanadaiwa kufikishana kwenye Kituo cha Polisi cha Sitaki-Shari, Dar baada ya mke kumfungulia…
Stori: Haruni Sanchawa
RB namba STK//RB/4457/2014 -KUTUMIA LUGHA YA MATUSI inawahusu wanandoa waliodumu kwa zaidi ya miaka 10, waliofunga ndoa kwa mbwembwe nyingi, Nyange na Ruth kisa kikielezwa kuwa ni ticha anayedaiwa kuvunja utatu huo mtakatifu, Ijumaa lina kisa na mkasa.
Habari zilieleza kwamba wahusika ni wakazi wa Pugu, Dar.
Kwa mujibu wa habari za mtaani wanakoishi wawili hao wanadaiwa kufikishana kwenye Kituo cha Polisi cha Sitaki-Shari, Dar baada ya mke kumfungulia mumewe jalada hilo la kesi baada ya ndoa yao kupigwa kimbunga.
Kuna madai mazito kwamba mke anamlalamikia mumewe kumjali zaidi hawara ambaye anadaiwa naye ni mke wa mtu akiwa ni mtumishi wa serikali yaani mwalimu.
Akisimulia kila kitu kwa gazeti hili, Ruth aliyefukuzwa na mumewe alisema kwamba utatu wake na mumewe uliingia mchanga kitambo bila yeye kujua chanzo kwani hakuwa mfuatiliaji lakini baada ya kufuatilia alibaini kuwa kuna mchepuko kwenye ndoa yake.
“Nilikuwa sijui ndoa yangu inachezewa na mtu gani, baadaye nilinasa mawasiliano ya simu ilibidi nifanye uchunguzi wa kina ili kumbaini mbaya wangu kitu ambacho nilikifanikisha kwa kiasi kikubwa alisema Ruth.
Kutokana na hali hiyo mume wake aliendelea kufanya manyanyaso huku akiendelea na mawasilino ya karibu na mwalimu huyo ambaye pia ni mke wa mtu.
Mama huyo alidai kuwa mume wake amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mtu huyo ambaye ni huyo mwalimu na kusababisha pia ndoa yake kuingia matatani.
Ninachokizungumza ni sahihi kwa sababu hata siku ninamkamata mume wangu alikuwa kwa mwalimu huyo ambapo siku hiyo alimpelekea sukari na matumizi mengine hali iliyosababisha timbwili kubwa, nilifanikiwa kumnyang’anya mume wangu ile mizigo aliyokuwa amepeleka kwa huyo mwanamke.
Mpaka sasa tunavyoongea huyo mwalimu ndoa yake iko matatani kutokana na jeuri aliyokuwa akipewa na mume wangu maana inadaiwa kuwa hata nyumba anayoishi mume wangu ndiye mlipa kodi.
Katika kikao kilichokaa shuleni mwaka jana kwa mwalimu huyo kuhusiana na tukio hilo, mwalimu huyo alikiri kuwa na mahusiano na mume wangu lakini aliahidi kuachana naye mbele ya kikao hicho, cha kushangaza hadi leo bado wanaendelea na mahusiano.
Alipoulizwa mwalimu huyo ambaye ametajwa kwa jina moja la Catherine Rokio Mayengo au Elizabeth Rokio Mayengo kwa njia ya simu kuhusiana na sakata hilo alimwambia mwandishi wetu kuwa namuuliza kama nani.
Mwandishi alijitambulisha na kumwambia anataka kujua hayo yanayosemwa na Ruth Nyange mwalimu yana ukweli gani.
Mwalimu huyo alisema hawezi kuongea na udaku hivyo kama ni kuandikwa habari hiyo iandikwa kadiri mwandishi anavyoweza.
Mbali na hilo mwalimu huyo alimwandikia ujumbe mwandishi wetu unaosema kuwa yeye anamilikiwa na serikali na haogopi kitu au jambo lolote na anajiamini na anapenda watu wanaotumwa kama mwandishi waende Stakishari.
Mwandishi wetu alifanikiwa kumpata mume wa mwalimu huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Evansi na kukiri kuwa huyo ni mke wake wa ndoa lakini hawako naye kwa muda huu.
Kuhusu mke wake kuwa na uhusiano na mtu mwingie, alisema inawezekana maana alianza ukorofi na kuamua kwenda kupanga lakini taarifa zilizopo amepangishiwa na mwanaume ambaye yeye hamjui.
Huyo mwalimu ni mke wangu wa ndoa hata mimi ninashangaa kuacha ndoa yake na kwenda kupanga na kuacha watoto wawili ambao tumezaa wote wakiwa wanateseka kwa kukosa mapenzi ya mama.
Mwandishi wa habari hii alifanya kila mbinu ya kukutana na mlalamikiwa ambaye ni Grey Godwin Nyange lakini ilishindikana na kujibu kwa njia ya simu kuwa habari anazoambiwa hazifahamu labda huyo aliysema hayo ndiye anayejua undani wake.
0 comments:
Post a Comment