Monday, 26 May 2014

RAY C KAMUOKOA MREMBO HUYU AMBAYE VIDEO QUEEN WA NOORAH - ICE CREAM

...

Screen Shot 2014-05-25 at 8.25.14 PMUnaikumbuka nyimbo ya Ice Cream iliyoimbwa na Noorah? Ni nyimbo nzuri iliyotamba miaka iliyopita na kuvuma zaidi baada ya video yake kutoka ambapo ndani yake kulikuwa na Video queen aliyefahamika kwa jina la Doreen.

Taarifa zilianza kusambaa kuwa mwanadada huyo kwa sasa ametumbukia katika tatizo la matumizi ya dawa za kulevya huku akihitaji msaada mkubwa. Screen Shot 2014-05-25 at 8.21.39 PM
Kupita ukurasa wa Instagram mwanamuziki Ray C ambaye nae aliwahi kukumbwa na tatizo hilo akiweka picha yake pamoja na Doreen huku akidai kuwa amempata na amekubali kuanza matibabu kuachana na dawa za kulevya.
Ray C ameandika kupitia Instagram >>> ‘Mungu ni mwema sana!!tena sana!!nilipotangaza kuwa nimefungua taasisi yangu ya kuelimisha jamii kuhusu athari za dawa za kulevya nilipata emails nyingi kuhusu kumsaidia Doreen video queen aliecheza kwenye video ya Noorah iitwayo ice cream!!nilijaribu kumtafuta baada ya kuona picha yake kwenye website ya vibe magazine’
Screen Shot 2014-05-25 at 8.13.30 PM‘Roho iliniuma sana nikamwomba Mungu anisaidie nimpate!! namshukuru Mungu asubuhi ya juzi nikiwa ofisini nikaona email kutoka kwa dada yake Doreen kichwa cha habari kikiwa msaada, nilipoisoma chozi lilinitoka nika reply mara moja nilimuomba anitumie namba yake tuongee nikampigia akaniambia doren hali yake si nzuri kutokana na drugs’
‘Moyoni nikawa nafikiria huyu dada angejua jinsi nilivyomtafuta mdogo wake !!!!!ikawa Kama bahati tukaongea kwa kirefu sana na nikamwambia tukutane kitengo cha dawa Mwananyamala! nilipomuona Doren kwa mara ya kwanza nilifurahi kupita maelezo ila nikawa na wasiwasi kuhusu utayari wake wa kuanza tiba ya methadone, isije ikawa amelazimishwa kuja akaniambia dada yangu nimechoka maisha ya utumwa nisaidie!!’
Screen Shot 2014-05-25 at 8.17.21 PM‘Hicho ndo nilichotaka kusikia nikamwambia kwa uwezo wa Mungu Shetani ameshindwa!!!!!! am soooo happy Doren ameanza tiba ya Methadone!!!wapenzi wote wa bongoflava nawaomba tumwombee mdogo wetu aweze kusimama kwenye tiba na ashinde majaribu ya Shetani na aishi kwa amani bila utumwa wa shetani’
‘God We Trust!!!I love You my lil’ sister….. nawahamasisha wengine huko mliko mwenye ndugu, jamaa au rafiki njoo katika taasisi yetu uweze kusaidiwa! usikubali maisha ya utumwa wa dawa za kulevya, njoo tukusaidie… Ray C Foundation pamoja na kitengo cha Methadone We love you guys, We can help you….”
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger