MASTAA wa Bongo Muvi wamemlilia msanii
mwenzao, Rachel Haule 'Recho' aliyefariki jana saa mbili usiku katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar baada ya kujifungua ambapo mtoto
wake alifariki muda mfupi na baadaye yeye akafariki.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Bongo Muvi,
Steve ‘Nyerere’, mwili wa Rachel utasafirishwa kwenda kwao Songea kwa
ajili ya maziko. Habari nyingine za msiba zitatolewa wakati wowote na
mtandao huu mara tu zinapopatikana.
0 comments:
Post a Comment