Kutokana na mjadala wa bajeti ya wizara
ya mambo ya nje uliokuwa unaendelea , Mbunge wa Nkasi Ndugu Ali Kessy
ameporomosha matusi mazito kwa wazanzibar kuwa ni watu wa hovyo na ambao
kila mara wanalialia tu kuwa wanabaguliwa , wanadai mambo mengi kuliko
uwezo wao na wakati hawachangii hata senti kwenye Muungano na hivyo kama
wanaona wanaonewa waende kwenye nchi yao sio kukaa kwetu.......
Alienda mbali zaidi kusema kuwa Zanzibar
Majimbo ya uchaguzi ni madogo kiasi kwamba ukipigania filimbi wananchi
wote wanakusanyika ila bado wanapewa fedha za mfuko wa Jimbo jambo
ambalo sio haki , na pia hata umeme hawalipi na maji pia .
jambo hili lilimfanya mbunge wa CCM
ndugu Chombo , kuomba muongozo na Kumtaka naibu Spika a mwambie Kessy
kamwe asikanyage Zanzibar , hii ilikuwa baada ya kumuita mwendawazimu ,
na alisema ni bahati mbaya kwa CCM kuwa na mbunge mwendawazimu kama huyu
......
Ndugai muda muda wote alikuwa akicheka , sijui nini maana yake .."...
0 comments:
Post a Comment