INASIKITISHA sana! Stela Mbinga ambaye
ni mke wa mtu, mkazi wa Tegeta - Kontena jijini Dar amepata balaa kubwa
baada ya kuchanwachanwa uso wake kwa viwembe na jirani yake
aliyefahamika kwa jina la Zakia Mohamed.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema
kuwa, Zakia na Stella kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi maisha ya uhasama
na kuringishiana hali iliyojenga chuki miongoni mwao.“Hawa huwa
wanashindana kimaisha. Huyu akifanya hivi, mwingine anafanya vile. Cha
kushangaza huwa wanatishiana hadi mambo ya vyakula, kwamba nani anakula
vizuri zaidi ya mwenzake.
“Sasa juzi Stella alikuwa amekaa
kibarazani wanazungumza na shoga yake, Zakia alipita akawakuta
wanacheka, hata alipokuwa chumbani wakaendelea na vicheko vyao, akahisi
wanamsema na kumcheka yeye, alipotoka akamvaa Stella, kumbe alikuwa na
kiwembe, akaanza kumchana bila huruma,” alisema mmoja wa majirani wa
wanawake hao.
Wasamaria wema walimpeleka Stella Kituo
cha Polisi Tegeta ambapo ilifunguliwa kesi nambari TGT/RB/1969/2014 -
Kujeruhi kisha kukimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala ambako
alishonwa nyuzi 19 usoni na nane kifuani.
Stella akiuguza majeraha.
Akizungumza kwa tabu nyumbani kwake,
Stella alisema: “Amenionea tu, hapa sijisikii vizuri. Nahisi
kizunguzungu na giza kila ninaposimama, pia siwezi kula vizuri chakula
kwani kila ninapotafuna, kichwa kinaniuma sana.”
0 comments:
Post a Comment