FEDHA inaongea!
Mastaa wanaowakilisha Klabu ya Bongo Movie Unity na Shirikisho la
Filamu Nchini (TAFF) wameonesha jeuri ya fedha kwa kuwatunza maharusi,
mwigizaji Vanita Omary na mumewe Paul Mtenda.
Mastaa wa Bongo Movies wakionyesha jeuri ya fedha katika harusi ya msanii Vanita Omary na mumewe Paul Mtenda.
Sherehe hiyo ilifanyika Jumamosi
iliyopita katika Ukumbi wa Mwika, Sinza jijini Dar ambapo pamoja na
zawadi nyingine, maharusi hao waliondoka na shilingi millioni tatu,
fedha taslimu.
Mpango mzima wa kuwamwaga ‘minoti’
uliongozwa na muigizaji Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Mwenyekiti wa Bongo
Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Jacob Steven ‘JB’, Kulwa Kikumba
‘Dude’ na wengineo ambapo mwishoni hesabu ya jumla ilitimia shilingi
milioni tatu.
Kwenye sherehe hiyo, hawakuonesha
utengano, hawakujali kama ni memba wa Bongo Movie au Shirikisho la
Filamu Nchini (TAFF) lililowakilishwa na rais wake, Simon Mwakifamba
ambaye muda wote alionekana mwenye furaha.
Mbali na Steve Nyerere, JB, Batuli na
Dude, mastaa wengine waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na Issa Mussa
’Cloud 112’, Elizabeth Michael ‘Lulu’, William Mtitu, Single Mtambalike
‘Rich’, Yvonney Cherry ‘Monalisa’, Suzan Lewis ‘Natasha’ na wengine
wengi.
0 comments:
Post a Comment