SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amesema ni marufuku kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kufanya shughuli zake ndani ya Bunge la Bajeti.
Alisema
hayo juzi bungeni baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni
Freeman Mbowe kutangaza baraza kivuli la mawaziri na kusema hicho ndiko
kikosi cha ukawa ndani ya Bunge.
Spika Makinda alimtaka
Mbowe kuhakikisha Ukawa inafanya kazi zake nje ya Bunge na si ndani ya
Bunge kwani wanapokuwa ndani ya Bunge wanakuwa ni kambi ya upinzani
bungeni na si vinginevyo.
Pia Spika Makinda alilitaka baraza hilo kivuli kutoa ushirikiano na wabunge wengine ili kufanya kazi ya kuendeleza watu.
Uteuzi huo ulihusisha
vyama vya Chadema, CUF na NCCR Mageuzi ambapo baraza hilo kivuli lina
mawaziri 29 ambapo watashika nafasi za uongozi katika kipindi
kilichobaki kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.
0 comments:
Post a Comment