Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka nyara.
Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar
Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo
tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria
wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi
hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika
kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake
miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa
wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.
CHANZO BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment