Kuiga ni kawaida kwa wengi.Wapo walioiga mambo fulani na hatimaye wakafanikiwa, na pia wapo walioiga vitu flani wakaharibikiwa.Huyu aliiga na akaharibu kila kitu...
Ni
msanii wa siku nyingi katika fani.Alitamba zaidi akiwa Kaole,
na hata mwanzoni mwa ujio wa filamu za Kanumba alizidi tu
kashaini....
Kiasili
ni mweusi japo siku hizi kuna weupe fulani katika ngozi yake
nyororo.Ana sura nzuri yenye mvuto,umbo aslia la kibantu,meno
yake meupe yamepambwa na mwanya mdogo na kufanya iwe fahari
kumuona akitabasamu...
Hana
kashfa ya kuvaa nguo fupi sana ila aliwahi kukumbwa na
skendo kubwa zaidi.Mkumbuke vizuri.Mrefu wa wastani,anajua
kutembea,anaongea kwa mapozi huku akipenda kulamba papi ya
midomo yake. Umemjua???....Hapana, siyo huyo...!!
Huyu
ni mpole kiasili na anapendwa sana na mama yake.Katika
maigizo ana uwezo wa kukufanya uamini unachoangalia ni kitu
halisi.Japo huwezi kumtaja, ila ndani ya wasanii kumi anapaswa
kuwamo...
Na
ingawa mvuto wake umepungua kiasi,ila bado mrembo sana.Lakini
wakati anaigiza Kaole alikuwa mrembo zaidi.Kwa uzuri wake ,
alivuma na kila habari inayohusu mwanaume maarufu na mwenye
pesa
Habari ya kutakiwa na kila mwanaume , wenye rangi na vipato tofauti zilisikika kila kona.Baadhi alitoka nao na wengine haikuwa bahati yao....
Toka
kitambo almanusura aolewe, ila ni miaka ya juzi juzi ndipo
aliolewa.Uzuri wake si wa kutafuta, kila mwenye macho na ngozi
ya kuhisi atautambua....
Mbali
na majanga yote aliyopitia katika maisha yake,mengine yakibaki
kumchafua na watu kudhani hawezi kuolewa na mwanaume yeyote
kabla ya ile bahati ya mtende akaolewa; yeye aliamua kuachana
na ndoa yake kwa kuona aishi katika umaarufu wake....
Mara
kadhaa alikuwa akiwaambia marafiki zake kuwa, mwenye hadhi na
anayetakiwa kuishi kama Wema Sepetu sio Wema bali ni yeye na
wakongwe wengine waliosotea sanaa na kuipigania kama roho zao
na kuilinda kama mboni ya jicho lao.....
Akaona
ndoa sio mahala pake,bila sababu za msngi akaamua kumwambia
mumewe watengane....Japo haikuwa rahisi ,lakini walitengana!!
Cha
kufurahisha ni kwamba bado Wema anaishi kama Wema na bado
yeye haishi kama Wema Sepetu na ndoa haipo tena...Umemjua
ninayemzungumzia?
0 comments:
Post a Comment